Paul Makonda kupanda ulingoni kupigana masumbwi na Cheka

Paul Makonda kupanda ulingoni kupigana masumbwi na Cheka

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda anatarajia kupambana ulingoni Agosti 27 mwaka huu na bingwa wa Masumbwi, Francis Cheka katika pambano lililolenga kuhamasisha usafi wa mazingira.

Taarifa ya pambano hilo imetolewa leo jijini Dar es salaam na bondia Cheka ambaye ameeleza kampuni yake ya Cheka Promotion ndio iliyoandaa tukio hilo la uhamasishaji.

Kupitia pambano hilo la 'Kimkakati' Cheka amesema anaamini watakuwa wameunga mkono zoezi la uhamasishaji wa usafi lililotiliwa mkazo na Rais John Magufuli.

Akizungumza pambano hilo, Cheka alisema kuwa huwa anaogopa mtu asiyejua ngumi anayekubali kupanda ulingoni na yeye.

"Siwezi kujua mkuu wa mkoa maandalizi yake ambayo amejiandaa lakini siku zote namuogapa mtu ambaye anaamua mapambano na mtu anayejua ngumi "Cheka alisema

Alisema kuwa baada ya tukio hilo, Kampuni yake itaelekea mikoani pia kuhamasisha mabondia kushiriki katika zoezi la usafi.
 
Back
Top Bottom