PreGE2025 Paul Makonda: Kuna kakundi nimekapiga spana. Acha wakahangaike kuroga, mi sirogeki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,690
Mkuu wa Mkoa wa Arusha mesisitiza kuwa hana woga wa vitisho wala hofu ya ushirikina, akisema wazi kuwa hata wale wanaojaribu kuloga hawawezi kumtikisa.

Akizungumza kwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa Mkoa wa Arusha,, Makonda amesema anasimamia maendeleo ya mkoa wake bila kuyumbishwa na vitendo vya kifisadi au hila za watu wasiopenda uwajibikaji na washirikina.

Makonda amebaini kuwa katika ofisi yake, kulikuwa na watumishi waliokuwa wakifanya ujanja ili kujinufaisha kifedha, ikiwemo kudai malipo ya ziada (cha juu) kutoka kwa wakandarasi. Hata hivyo, amewachukulia hatua wote waliohusika na kusafisha mfumo huo wa ulaji.

“Lakini kwa nini walikuwa wanafanya hivyo? Ilikuwa ni ulaji! Kila mtu mmoja akiitwa, akisaini ule mkataba, anaacha hela. Nimeshawapiga spana, wamenyooka! Sasa hivi jengo linaenda ghorofa ya tano... Sasa kale ka kundi kote nimekasafisha, nimekang'oa pale. Acha wakahangaike kuloga kule—lakini mimi silogeki! Ninachotaka ni maendeleo ya Mkoa wa Arusha,” amesema Makonda.

kulogana, ulozi, uganga na uchawi?!
Ndio vimemfikisha hapo
Acha apige kazi ndugu Makondakta
 
Kuuongelea tu mambo ya ulozi mara kwa mara ni ishara kuwa ni mshiriki mkubwa.
 
Back
Top Bottom