Paul Makonda: Kuanzia 01.03.2019 kila mtu lazima awe na kitambulisho cha machinga au ajira, kama huna we mhujumu uchumi

Hii ya Vitambulisho vya Machinga,vipi ipo kwenye ilani yao ya uchaguzi..?

Au Sera hazitekelezeki sasa wanarukia rukia chochote ili mradi mambo yaende.

Suluhisho hapa wangewatengenezea Machinga Mazingira rafiki kwa ajili ya shughuli zao,ikiwa ni pamoja na kuwajengea maeneo mazuri yenye miundo mbinu imara.
 
Nchi imeharibika kabisa! Kila mtu lazima atasimamishwa kuulizwa kitambulisho, watu watasombwa! Kuingia ndani ni bure na kutoka lazima wakusanye ela! Hutoki polisi bure hata kama huna kosa!

Tusubiri reaction ya watanzania, wasipotia akili nyakati hizi, basi ni sikio la kufa...
Hivi Segerea na Keko patatosha kweli au pale Jangwani kwa mabasi ya mwendo kasi waweke mahema.
Kwenye familia yangu tupo 10 mfanyakazi mmoja tunayemtegemea. Waje tu tunawasubiri.
 
Mkuu wa mkoa wa dar es salaa amesema kuanzia tarehe 01/03/2019 atahakikisha watu wote wanaokaa dar es salaam wanakaguliwa na lazima wawe na
1.Kitambulisho cha Machinga cha Mheshimiwa rais,
2.Ama Awe na TIN number na Leseni ya biashara
3. Ama kazi maalumu, (ajira) ambayo ina vielelezo

Nje ya hapo mtu huyo atakuwa mhujumu uchumi kama wengine na atafuatiliwa

ANGALIZO
Miji yote dunian huwa ina watu wa aina zote hata ambao hawana ajira maana wapo hata wanaosaka ajira hawajapata,

Pili atasababisha watu kuishi kwa hofu kama enzi za kodi ya kichwa
Hawa vichaa wa kisukuma mbona wanazidi kutuvuruga? Yadhibitiwe
 
Tumesituka wanataka tupambane nao ili wasiondoke madarakani wajifanye nchi haijatulia , hatupambani nao ng'oo, na wakiendelea ya dr. Kilelu yatatokea
 
Hili nalo bashite atafeli kama alivyofeli kwenye mengine. Kisheria sijui nalo hili limekaaje?
 
Tatizo tunajisahau saana,
Mkuu wa nchi alishasema
“MWENYE KUKAA DAR HADI MWEZI WA 7,HUYO NI MWANAUME”

sasa mkumbuke kuwa chochote atakacho kisema lazma akifayie kazi hata kama ni mwaka kesho‍♂️
 
cheti cha msamaha kama alivyokuwa anatoa Askofu Wa Roma eti...
Hii ndiyo muhimu kuliko vyote!! Ukikosa vyote basi uwe na hicho tu!! Mimi mwenyewe nakitafuta kwa ajili ya shughuli zangu zilizo nje ya utaratibu wa kisheria!! Hata ukitaka kufanya ujambazi kwa amani bila bughudha basi wewe kuwa nacho tu!!hicho ni kama cheti cha msamaha wa dhambi!!
 
Sisi wakulima itabidi tutembee na pembejeo za kilimo maana vitu vya kututambulisha havijatajwa hapo

MHU. :10:16
Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana,.....
Mkuu kuna waraka Wa Kilimo unataka kusajili wakulima wote kila wilaya heheheeheeee hakuna pa kutokea nje ntiti ndani ntiti juu nyuki chini nyoka ...shubaaaakengemiti ...
 
Mkuu wa mkoa wa dar es salaa amesema kuanzia tarehe 01/03/2019 atahakikisha watu wote wanaokaa dar es salaam wanakaguliwa na lazima wawe na
1.Kitambulisho cha Machinga cha Mheshimiwa rais,
2.Ama Awe na TIN number na Leseni ya biashara
3. Ama kazi maalumu, (ajira) ambayo ina vielelezo

Nje ya hapo mtu huyo atakuwa mhujumu uchumi kama wengine na atafuatiliwa

ANGALIZO
Miji yote dunian huwa ina watu wa aina zote hata ambao hawana ajira maana wapo hata wanaosaka ajira hawajapata,

Pili atasababisha watu kuishi kwa hofu kama enzi za kodi ya kichwa
Nchi hii inaendeshwaje na nani?
Walio na macho waliisha kuona hatari ya kutokea haya na hatma ya utawala bora wa sheria.
Waliosoma historia ya Ujerumani watakumbuka Hitler alivyopanda madarakani kwa ushabiki na baadaye kuitawala kwa staili yake. Marehemu Baba wa Taifa, Mwl J. K. Nyerere aliwahi kutoa hadhari kwa kusema kuwa kiongozi hapaswi kulala na mkewe, wakota, wakabuni, na kukubaliana lipi la kuamka nalo la 'kuwapelekeshea' watu. Mtanzania ana haki ya kujua kesho yake itakuwaje. Aidha, kiongozi akiwanya anaowaongoza wapumbavu, basi anakosa sifa za kuongoza; ataongoje wapumbavu?
Lipo hili la kuwalazimishia watu vitambulisho vya Machinga kwa nia ya serikali kupata mapato. Hilo liko wazi. Je, njia hii ni halali?
Njia kuu za mapato ya serikali ni kodi na ada mbali mbali. Misingi yake ni huduma zinazotolewa kwa watumiaji na walipaji. Ubunifu wa TRA na mamlaka mbali mbali zinazohusika na kutoza kodi na ada kwa ajili ya kuingizia serikali mapato uko wapi?
Aidha, pamoja ya "maboresho" ya njia za ukusanyaji kodi (EFD,nk.), uchumi na biashara nchini vimeshuka. Mfanyabiashara anajua kuwa kitu muhimu kwake ni "turnover"; ni mara ngapi shilingi yake itaingia na kutoka, siyo bei kubwa itakayoifungia pesa yake ndani.
 
Mkuu wa mkoa wa dar es salaa amesema kuanzia tarehe 01/03/2019 atahakikisha watu wote wanaokaa dar es salaam wanakaguliwa na lazima wawe na
1.Kitambulisho cha Machinga cha Mheshimiwa rais,
2.Ama Awe na TIN number na Leseni ya biashara
3. Ama kazi maalumu, (ajira) ambayo ina vielelezo

Nje ya hapo mtu huyo atakuwa mhujumu uchumi kama wengine na atafuatiliwa

ANGALIZO
Miji yote dunian huwa ina watu wa aina zote hata ambao hawana ajira maana wapo hata wanaosaka ajira hawajapata,

Pili atasababisha watu kuishi kwa hofu kama enzi za kodi ya kichwa
Hebu nenda kalipe kodi badala ya Kuwa unalia hajasema wakazi amesema wafanyabiashara wenye turnover ya chini milion 4 au wamachinga. Sasa nikuulize wakazi wote wa Dar ni wamachinga? Tufanye kazi na kulipa kodi hutaki rudi kijijini ukalime.
 
Naona umekuwa Wa kwanza kulipwa buku 7000 leo. Hongera
 
Nchi imeharibika kabisa! Kila mtu lazima atasimamishwa kuulizwa kitambulisho, watu watasombwa! Kuingia ndani ni bure na kutoka lazima wakusanye ela! Hutoki polisi bure hata kama huna kosa!

Tusubiri reaction ya watanzania, wasipotia akili nyakati hizi, basi ni sikio la kufa...
Mimi nafikiri waacha watu wanyooshwe mpaka wanyooke maana tunaposema ccm ni la kutaifa waelewe maana yake nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna waraka Wa Kilimo unataka kusajili wakulima wote kila wilaya heheheeheeee hakuna pa kutokea nje ntiti ndani ntiti juu nyuki chini nyoka ...shubaaaakengemiti ...
Nia ya kuwasajili wakulima ni nn?Mkulima yupi asiyeulikana kijijini kwake? Na hili linagharimu pesa pesa "Ubunifu" huu hauna mantiki. Zipo tawimu za sensa, wapigakura, na vitambulisho vya taifa. Ikaja sheria ya takwimu. Hofu ya takwimu mbadala inakujaje kama "hazipikwi"? Haieleweki kama mradi wa vitambulisho vya taifa bado uko hai! Inasemekana wajanja walipiga pesa za mradi.
Aidha, pengine pesa zilizotengwa kwa ajili hiyo zilihamishiwa kwingine maana matumizi makubwa ya fedha yasiyofuata kanuni za bajeti iliyoptishwa na bunge yanapangiwa Magigoni, si hazina tena. Wabunge wetu hawathubutu kuuliza ila wapo "sharp" kwa mishahara ya Tundu Lssu. 1.5trl/- zilipoulizwa wakaja na neno uchochezi.
 
Back
Top Bottom