digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,901
- 14,368
Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda leo February 18 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davulaglu, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof.Elizabeth Kiondo, Mstahiki Meya kutoka Uturuki, Wawekezaji na Wafanyabiashara zaidi ya 40 wa Uturuki waliokuja kuchangamkia fursa za uwekezaji wa viwanda DSM.
RC Makonda amewahakikishia Wawekezaji hao kuwa Serikali ya Mkoa wa DSM itawapatia ushirikiano wa kutosha wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza ili kutimiza malengo ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
RC Makonda amewaeleza wawekezaji hao kuwa DSM inajivunia kuwa na amani na utulivu pamoja na fursa ya uwepo wa Bandari, Uwanja wa Ndege na miundombinu yote muhimu ya kuvutia uwekezaji "nitawapeleka Wawekezaji Kigamboni wakajionee maeneo yaliyotengwa kwa uwekezaji"
Balozi Ali Davutaglu amemuhakikishia RC Makonda kuwa Uturuki itazidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo na wamemualika RC Makonda kwenda kutembelea Uturuki.
Watu kama hawa lazima wapingwe na watu wasiopenda Maendeleo,Viva my bro Makonda
Sent using Jamii Forums mobile app