Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,230
MWENYEKITI wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Paul Kimiti, amewataka baadhi ya viongozi na wanasiasa kuwa waangalifu katika matumizi ya mitandao ya kijamii, ili kulinda amani na mshikamano wa Taifa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Daily News Digital jijini Dar es Salaam, Kimiti amesema misingi ya uongozi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere, inasisitiza matumizi ya busara na hekima katika kushughulikia changamoto za kitaifa, badala ya kutumia majukwaa ya mitandao kujibizana au kulaumiana.