The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 828
- 2,108
Kama ilivyo kwa maeneo mengi duniani, nchini Rwanda kuna vipindi vinne vya majira ya mwaka; Kipupwe, Kiangazi, Vuli na Masika. Kipindi cha Masika huanzia mwezi Machi, Aprili hadi Mei, mvua humwagika sana na aghalabu husababisha maafa. Ardhi hugeuka tope, mito na vijito hutiririsha maji kwa wingi. Lakini Masika ya mwaka 1994 yalijaza mito kwa maji na damu pia.
Ilikuwa saa 2:20 usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, ndege ya shirika la Ubelgiji C-130 Hercules, iliyokuwa ikipaa kila wiki, ikiwa imebeba kikosi cha askari wa umoja wa Mataifa cha UNAMIR, ilisubirishwa angani ili ndege ya Rais iweze kutua kwanza katika uwanja wa ndege wa mjini Kigali.
Ndani ya ndege hiyo ya Rais walikuwamo;
1.Juvénal Habyarimana, Rais wa Rwanda
2.Cyprien Ntaryamira, Rais wa Burundi
3.Bernard Ciza, Waziri wa kazi wa Burundi
4.Cyriaque Simbizi, Waziri wa mawasiliano wa Burundi.
5.Meja Generali Déogratias Nsabimana, Mkuu wa utumishi wa jeshi la Rwanda.
6.Meja Thaddée Bagaragaza, Mkuu wa kikosi cha "maison militaire" cha Rais wa Rwanda.
7. Kanali Elie Sagatwa, mjumbe wa sekretarieti maalum ya Rais wa Rwanda na mkuu wa baraza la kijeshi la Rais wa Rwanda.
8. Juvénal Renaho, mshauri wa masula ya kigeni wa Rais wa Rwanda
9. Dr. Emmanuel Akingeneye, Daktari binafsi wa Rais wa Rwanda
10.Jacky Héraud, Rubani (raia wa Ufaransa)
11.Jean-Pierre Minaberry, Rubani msaidizi (raia wa Ufaransa)
12.Jean-Michel Perrine (Injinia wa ndege, raia wa Ufaransa)
Wakati ikijiandaa kutua, makombora mawili ya kurushwa kutoka ardhini yalikatisha maisha ya watu hao 12 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo aina ya Jet-Dassault Falcon. Kombora la kwanza likipiga ubawa mmoja wa ndege na kombora la pili likapiga mkia, kisha ndege hiyo ikiwa inawaka moto iliangukia kwenye bustani ya ikulu ya Rais.
Tukio hilo likawa mwanzo wa machafuko yaliyopelekea mauaji ya wanyarwanda zaidi ya laki nane (800,000) kwa siku mia moja pekee. Maana yake kila siku walikufa watu 8000.
Wanamgambo wa kihutu, walioitwa "Intarahamwe" wakisaidiwa na wanajeshi wa kihutu walitumia silaha za Jadi kuwaua watu wa kabila la Watutsi. Madhania yao yakiwa kwamba, Watutsi wamemuua Rais Habyarimana; muhutu.
Mbinu za kiintelijensia zilizosukwa kwa ustadi mkubwa zilitumika kuifanya Rwanda kuwa uwanja wa damu. Kuwapiganisha kwa makusudi Wahutu na Watutsi ili kuharibu mfumo wa kimaisha wa nchi, na hivyo kujinyakulia utawala kwa wepesi.
Hapo mwanzo.
Miaka ya 1950 palitokea vurugu za kikabila zilizopelekea watu wa kabila la kitutsi kukimbilia nchi za jirani hasa Uganda, Tanzania na Zaire. Moja kati ya familia zilizokimbilia Uganda ilikuwa familia ya mtoto Paul Kagame, iliokuwa ikiishi huko Tambwe, kusini mwa Rwanda.
Miaka ya 1980s, Paul Kagame akiwa na umri wa kati ya 15-18 alijiunga na kikosi cha kijeshi kilichoongozwa na Yoweri Museveni. Ni kikosi hiko cha Museveni kilichoungana na majeshi ya Tanzania kumng'oa Idd Amin Dada wa Uganda mwaka 1979.
Baada ya Idd Amin kukimbia Uganda, Milton Obote aliyekuwa mafichoni Tanzania, alirudi Uganda na kuwa Kiongozi huko. Lakini Museveni alianzisha mapambano yaliyoitwa "Ugandan Bush War" mwaka 1981 hadi 1986 kwa lengo la kumng'oa Obote. Ni katika Mapambano hayo ambapo vijana mahili wa kitusi, Paul Kagame na Fred Kagyirwa walijiunga kumpigania Museveni.
Ieleweke pia Museveni alianza mapambano yake tangu mwaka1972, akitumia ardhi ya Tanzania kama maficho. Lakini September 1972 vikosi vyake vilishindwa vibaya, na baadae Octoba mwaka huohuo, Makubaliano ya Mugadishu yalimfanya atulize majeshi yake katika ardhi ya Tanzania baada ya Tanzania kulaumiwa na jumuia ya kimataifa kwa kumuifadhi. Akahamia huko kusini mwa Uganda lakini baadae alirudi tena Tanzania.
Mwaka 1985, Lt General Tito Okello alimpindua Milton Obote, lakini miezi michache baadae, tarehe 29 january, 1986, Museveni, aliapishwa kuwa Rais baada ya viongozi wa serikali na wa jeshi la nchi kuanza kujiuzulu huku vikosi vyake vya Popular Resistance Army (PRA) vikizidi kusonga kutokea kusini na kusini magharibi mwa Uganda.
Akiwa madarakani Museveni alimfanya Paul Kagame kuwa mkuu wa intelijensia ya kijeshi katika jeshi la Uganda huku Fred Gisa Rwigyema akiwa naibu waziri wa ulinzi.
Fred Rwigyema.
Huyu alizaliwa akiitwa Emmanuel Gisa, mnamo Tarehe 10 Aprili 1957 huko Gitarama kusini mwa Rwanda. Mwaka 1960 familia yake ilikimbilia nchini Uganda kwa namna ileile iliyoikimbiza familia ya Paul Kagame, vurugu za wahutu. Huku wote Wakiwa na umri wa miaka mitano mwaka 1962 Paul Kagame na Emmanuel Gisa walikuwa watoto marafiki huko katika kambi la wakimbizi la Nshungerezi, Ankole - Uganda.
Lakimi mwaka 1970, Emmanuel Gisa alipotelea kusikojulikana.
Kutoweka kwa rafiki na kufiwa na Baba yake Paul Kagame kulimfanya apate tatizo la mafadhaiko. Lakini angalau baada ya muda alizoea na kuanza rasmi kufikiri namna ya kurudi Rwanda.
Mwaka 1976 Emmanuel Gisa aliibuka, wakati huu akiwa na rafiki aliyeitwa Salim Saleh. Lakini jina halisi la rafiki huyu lilikuwa Caleb Akandwanaho kaguta Museveni. Mdogo wa Yoweri Museveni aliyekuwa nchini Tanzania akiongoza vikosi vya kijeshi vya Front of National Salvation (FRONASA). Emmanuel Gisa aliamua kujiunga na kaka huyo wa rafiki yake, na akiwa nchini Tanzania alianza kujiita Fred Rwigyema. Akiwa Tanzania chini ya Yoweri Museveni, alipata kuwa mmoja wa wapiganaji waliosaidia FRELIMO kule nchini Msumbiji.
Baadae, Rwigyema alijiunga tena na vikosi vya Uganda National Liberation Army (UNLA) vilivyoshirikiana na vikosi vya Tanzania kumng'oa Idd Amin. Kisha alijiunga na National Resistance Army (NRA) chini ya Museveni.
Akiwa madarakani katika nafasi ya Naibu waziri wa Ulinzi nchini Uganda, tangu mwaka 1986, Rwigyema alianza harakati za kuwandaa watutsi waliokuwa nje ya Rwanda kurudi kwao. Kufikia mwaka 1990 alikuwa ameunda kikosi cha Rwanda Resistance Force (RPF), kikosi cha watutsi kilichojiandaa kuwarudisha watutsi nchini kwao.
Serikali ya Burundi ilimlaumu sana Museveni kwa kuwapatia Paul Mugabe na Fred Rwigyema (Emmanuel Gisa) vyeo vikubwa na kuwapa nafasi ya kuandaa mapinduzi nchini Burundi. Lakini lawama hizo zilichagiza mchakato wa kuunda uasi dhidi ya serikali ya Rwanda.
Octoba 1, 1990, Rwigyema aliongoza uvamizi nchini Burundi, akitumia vikosi vya RPF. Lakini alikufa siku mbili au tatu tu baada ya uvamizi.
Mwanahistoria Gerald Prunier anaandika kwamba, Taairifa za awali zilisukwa kuonesha kwamba Rwigyema aliuawa kwa risasi iliyokuwa ikiranda randa, wakati wa mapambano. Lakini taarifa za baadae zinatanabaisha kuwa Rwigyema aliuawa na kamanda wa chini yake, Peter Banyingana.
Wakati hayo yakitokea, Paul Kagame alikuwa nchi Marekani kwenye mafunzo zaidi ya kijeshi na kiintelijensia katika chuo cha Fort Leavenworth.
Ndipo aliporudi na kuiongoza RPF kama kikosi cha waasi kikiweka kambi katika milima ya Virunga, magharibi mwa Uganda.
RPF ya Kagame ilikuwa changamoto kwa serikali ya Rwanda ya Rais Habyarimana lakini, RPF hiyo haikuwa Tishio kubwa. Kwa mitindo ya vita ya Misituni, Guerrilla War, ilivamia na kushambulia ndani ya Rwanda mara kwa mara. Wakati mwingine iliweza kutwaa baadhi ya maeneo na kuyamilki. Muungano wa vyama vya siasa mwaka 1992 huko nchini Rwanda ulipelekea Paul Kagame asitishe mapambano na kuanza Mazungumzo huko Arusha, Tanzania. Lakini januari ya mwaka1993, Wahutu wenye msimamo mkali wa nchini Rwanda walianzisha vuguvugu la kutaka kuwadhuru na kuwadhibiti Watutsi. Hali hiyo ilipelekea Kagame kusitisha mazungumzo na kuanzisha upya mapambano yaliyofanikiwa kwa kutwaa eneo kubwa la kaskazini mwa Rwanda. Ndipo mazungumzo yalipoanza tena mjini Arusha na Agosti 1993 makubaliano ya amani ya Arusha (Arusha Accords) yalifikiwa. Kikosi cha kutunza amani cha umoja wa Mataifa (United Nations Assistance Mission for Rwanda/UNAMIR) kilifika rasmi mjini Kigali na Waasi wa RPF wakiongozwa na Kagame walipewa ofisi katika jengo la Bunge mjini Kigali.
Ndipo ilipowadia siku hiyo ya Tarehe 6 Aprili 1994. Taarifa za wazi hazisemi ni nani aliyehusika na mauaji hayo ya kihistoria. Pengine jua lilipochomoza mashariki, asubuhi ya siku hiyo Marais hao wa Rwanda na Burundi, kama binadamu wengine walipanga mikakati yao ya baadae. Lakini jua halikuwahi kuchomoza tena machoni mwao. Mwanahistoria Gérald Prunier anadokeza kwamba Wahutu wenye msimamo mkali ndiwo waliopanga mapinduzi yale baada ya kuona Rais Habyarimana akifanya maridhiano na watutsi. Prunier anaendelea kwa kudai kuwa mauaji ya watutsi yaliyofuata yalikuwa tayari yamepangwa na Wahutu wenye msimamo mkali. Hoja yake inajitetea kwa matukio yaliyofuata ambapo kiongozi wa kamati ya kijeshi, Kanali Théoneste Bagosora alitwaa madaraka na kuanza kupanga mauaji ya watutsi na wahutu wasio na msimamo mkali. Viongozi wote wa kiserikali waliokuwa wahutu wasio na msimamo mkali waliuawa ndani ya masaa 24, akiwamo aliyekuwa waziri mkuu Agathe Uwilingiyimana (Madame Agathe), waziri mkuu wa kwanza na wa mwisho mwanamke nchini Rwanda.
Siku ya pili, Wanamgambo wa kihutu, Intarahamwe walivamia jengo la Bunge kwa lengo la kuwaua watu wa RPF, lakini RPF walipambama na kufanikiwa kuwashinda. Paul Kagame alikwisha kimbia pembeni ya Rwanda na huko alianzisha mapambano dhidi ya wanamgambo wa kihutu. Kanali Bagorosa aliomba mazungumzo lakini Kagame alikataa kwa kudhani ulikuwa ni mtego. Kwa muda wa siku 100, Watutsi wapatao 500,000 na wahutu wasio na msimamo mkali wauawa.
Mwaka 2006, Jaji Jean-Louis Bruguiére wa ufaransa alimtaja Paul Kagame kama Injinia wa mauaji ya marais Habyarimana na Ntaryamira. Mwaka 2008, Jaji Fernando Adreu wa Uispaniola alikazia pia kuwa Kagame na RPF walihusika katika tukio la kuitungua ndege ile iliyobeba marais wa Rwanda na Burundi.
Miaka 24 baadae, tunaweza sema Rwanda inasonga. Lakini maswali bado ni mengi yanayohitaji majibu ya kuziba matobo kwenye kurasa za historia.
Kwanini Kamanda Peter Banyingana alimuua Mkuu wake, Fred Rwigyema?
Je ni Kweli Paul Kagame alihusika katika mauaji yale ya marais wa Rwanda na Burundi?
Uwepo wa vikosi vya umoja wa mataifa (UNAMIR) ulisaidia nini wakati wa mauaji ya watutsi?
Je! Lilikuwa tukio la kupangwa na taasisi nyingi zikiwemo za kimataifa?
Vipi kuhusu Mustakabali wa Rwanda baada ya Kagame?
Tukio hilo, hatahivyo limekuwa funzo kubwa nchini Rwanda. Wanaintelijensia katika baadhi ya nchi za kiafrika wamejaribu/ wanajaribu kuchochea matukio kama ya Rwanda ya April 1994 ili kurahisisha utawala wa watawala.
Makovu yake hayatafutika kwa karne nyingi.