R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
Paul Kagame alizaliwa Oktoba 23, 1957, ni rais wa sita wa Rwanda akichukua madaraka mwaka 2000 wakati rais aliyekuwa madarakani wakati huo, Pasteur Bizimungu, alipojiuzulu.
Kagame hapo awali alikuwa kiongozi wa kundi la waasi kabla ya kushuhudiwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, na aliteuliwa kuiongoza Rwanda baada ya kuwa Makamu wa Rais na Waziri wa Ulinzi tangu mwaka 1994 hadi 2000.
Kagame anatoka katika familia ya Kitutsi inayopatikana kusini mwa Rwanda. Akiwa na miaka miwili, yalitokea mapinduzi nchini mwake na kuhitimisha utawala wa Kitutsi uliodumu kwa karne nzima; familia yake ilikimbilia nchini Uganda na alisalia huko hadi ujana wake.
Mwaka 1980, Kagame alipigana katika jeshi la uasi lililokuwa chini ya Yoweri Museveni (rais wa sasa wa Uganda), na alikuwa mmoja wa maofisa wa jeshi la Uganda baada ya ushindi uliomuweka madarakani kama mkuu wa nchi Museveni.
Kagame alijiunga na Jeshi la Rwandan Patriotic Front (RPF) wakati huo wakipigana msituni na kuivamia Rwanda mwaka 1990; Fred Rwigyema aliyekuwa mkuu wa jeshi hilo aliuawa vitani na Kagame kuchukua uongozi.
Mwaka 1993, RPF ilikuwa ikitawala eneo kubwa la mipaka ya nchi ya Rwanda ingawa bado walikuwa hawana madaraka kamili.
Kuuawa kwa aliyekuwa rais wa Rwanda, Juvenalis Habyarimana, ndio ulikuwa mwanzo wa mauaji ya kimbari ambapo wapiganaji wa Kihutu inakadiriwa waliwaua Watutsi wapatao 500,000 hadi milioni moja (inaelezwa hata baadhi ya Wahutu pia waliuawa).
Kagame aliingilia kati vita hii ya wenyewe kwa wenyewe, aliibuka mshindi na kuhitimisha mapigano yale.
Akiwa Makamu wa Rais, Kagame aliongoza jeshi la kitaifa na kusimamia utawala wa sheria wakati maofisa wengine wa jeshi wakisimamia ujenzi wa Rwanda mpya.
Askari wengi wa RPF inaelezwa walikuwa wakiendesha mauaji; bado haijawekwa bayana kama Kagame aliamrisha mauaji haya au la, na kwanini hakusimamisha mauaji haya kwa sababu uwezo alikuwa nao?
Makambi ya wakimbizi wa Kihutu yalifunguliwa DRC na nchi nyingine jirani ingawa yalikuwa chini ya waliosemekana kuwa ndio wahusika wa mauaji yale ya kimbari na kuendelea kuleta hofu nchini Rwanda.
Majeshi ya RPF yalishambulia makambi haya na kuyafunga baadhi na kuwalazimisha wakimbizi kurudi nyumbani mwaka 1996, ingawa hali ya usalama haikuwa nzuri sana kipindi hicho.
Kama sehemu ya tatizo la uasi, Rais Kagame anatajwa kufadhili makundi mawili ya waasi DRC.
Vita ya kwanza ya msituni iliyosimamiwa na Wanyarwanda na Waganda kwa pamoja kati ya mwaka 1996 na 1997 ilimsimika rasmi Laurent-Desire Kabila kama rais wa nchi akichukua nafasi ya dikteta Mobutu Sese Seko na kuibadilisha jina nchi kutoka Zaire kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Vita ya pili ya msituni ilipiganwa mwaka 1998 dhidi ya rais Kabila na kwa ushirikiano ule ule wa Rwanda na Uganda walifanikiwa kumngoa madarakani, baadaye mtoto wake Joseph, alitawazwa kuongoza taifa hilo kubwa katika Afrika ya Kati.
Joseph aliingia madarakani baada ya kuuawa baba yake, ambapo baraza la wazee kwa kutumia hekima liliona kama atawekwa mtu mwingine kutawala kulikuwa na uwezekano serikali hiyo isidumu.
Kwa hiyo ni busara za wazee ndizo zilizomweka madarakani Joseph Kabila.
Hata baada ya Joseph kutawazwa inaelezwa vita ya chini kwa chini ya makundi kadhaa ya uasi iliendelea hadi uliposainiwa mkataba wa amani mwaka 2003.