Kila mtu anapokuwa amebanwa lazima atafute utetezi hata kama ni wa uongo, hapo Chizi anatapatapa tu ukweli unabaki palepale, ATCL kulikuwa na ubadhirifu mkubwa saana, Miaka Ishirini iliyopita kulikuwa na ndege kubwa zaidi ya tano,Leo hii shirika hoi, Loh tumechoka kudanganywaa!!!
Aliyekuwa mtendaji mkuu wa ATCL ameibuka na kusema kwamba Dr Mwakyembe alidanganya umma kutokana taarifa alizopewa kuwa ni za uongo na zisizokuwa na ukweli wowote.
Kwa mfano uniform ziligharimu dola 18,000 tu na sio dola 50,000 kama alivyosema mwakiembe, Bwana Chizi alisema pia tatizo ni kwamba kuna watu hawajui chochote kuhusu sekta ya anga lakini wanajidanganya kuwa wanajua mbele ya umma.
Chanzo: The Guardian on Sunday
Mkuu mwalimu wako wa kiingereza ana laana, yaani maelezo yanajitosheleza na hadi gharama ya unit imeelezwa bado hujaelewa na unabisha...
Ninashauri sio lazima kuchangia mada kama hujaelewa, haya mambo ya aviation ni ya kitaalam, nyie mliotokea shule za kata kaeni pembeni wataalam walumbane.
Nenda jukwaa la lugha kajifunze kiingereza au hire a translator
chizi weweSi ajabu anaitwa chizi....utatumiaje dola 18,000 kushona nguo ambazo zaweza shonwa kwa batiki za hapa hapa na hata Millioni 2 isifike.....
chizi wewe
je unajua ni yunifomu ngapi na kwa staffs wangapi??
Unajua bei ya batiki wewe kima?
Hata kama hivyo ndivyo alivyosema, bado kuna tatizo kubwa sana hapo.
USD 18,000 X 1500=Tsh. 27,000,000 kwa unifomu moja! Milioni 27 kweli kwa nguo moja?
Hajaweza bado kuniweka kwenye kundi la watu wa kumuamini na sana sana ananiongezea machungu tu ya PAYE niliyokatwa mwezi uiopita.
chizi wewe
je unajua ni yunifomu ngapi na kwa staffs wangapi??
unajua bei ya batiki wewe kima?
Chizi anafahamu sana anachokifanya, ameharibu akubali, aondoke akapumzike.Mwakyembe amezungumzia gharama ya uniforms ni $49,900, tena amesama wazi. lakini chizi kwa usanii wake na huyo mwandishi wanazungumzia bei ya uniform ni $18,000. bei na gharama ni vitu viwili tofauti, sasa sitegemei CEO apindishe tafsiri kati ya bei na gharama.
hao precision air walinunua uniform kwa bei kati ya $ 200 na $ 600 kwa kila mmoja. ATCL hata kama wangenunua kwa bai kama ya precision air, gharama ya ATCL kwa uniform zao bado ni juu , kwani wao (ATCL) walituma wafanyakazi wao kwenda kununua na walitumia siku 45 huko, so maisha yao huko yanaingia ktk gharama ya uniform.je precision air nao walituma watu china kwa siku 45?, kama wangefanya hivyo, si precision air ingeshakufa?. chizi ni mtu mzima ameharibu akubali. baadhi ya waandishi wetu nao ni waandishi uchwara, wana ripoti bila kuchunguza na kutafsiri wanacho ripoti
Mwakyembe ni mpenda misifa, msiomjua nawapa pole.