Paul Chagonja atimuliwe Polisi

Paul Chagonja atimuliwe Polisi

sosoliso

Platinum Member
Joined
May 6, 2009
Posts
8,543
Reaction score
9,478
Soma habari hii halafu utaelewa kwa nini chagonja anapaswa kufukuzwa kazi polisi..

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta saidi mwema ametuma kikosi cha maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hiko, kikiongozwa na Mkurugenzi wa operesheni na mafunzo kamishna Paul Chagonja kwenda mjini songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo.
Chagonja akiongea na mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwamo ikulu ndogo na ofisi ya mkuu wa mkoa.
Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze ednapo haoni kkama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.
“maandamano yamani watu wanavamia ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?”
“sijafika huko ndio naelekea lakini yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka waachiwe? Kuweni wazalendo , miswe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka uingereza, hii ni nchi yenu”
Alifafanua kwamba maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano. “lakini siyo maandamano yale, hayakuwa na kibali chochote wahuni tu wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi”
Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema; “ucifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue ovyo risasi za motokwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia, lakini watu wanavamia ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa magari ya polisi, hapo kuna amani kweli?”
Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki na badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza: “kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu”

Source: Mwananchi

Wana jamii hayo ndo maneno ya kiongozi wa kikosi cha kwenda kufanya uchunguzi wa mauaji yaliofanywa na polisi huko songea.. anatetea askari wake hata kabla ya kufika na kufanya uchunguzi..

haki itatendeka kweli..? anafaa kuendelea na wadhifa wake huo..?
 
Mkuu aondolewe awekwe nani yaani jk anamaboga akitoa anaweka matikiti maji,
NIMECHOKA NA KUMPA USHAURI JK BWANA.
KILICHOBAKI NI KUBOMOA TUTAJENGA KESHO!

inawezekana akapatikana juha alie afadhali mkuu.. Imagine ametumwa kwenda kuchunguza.. lkn ameanza kutetea kabla ya kutoa nyayo zake hapa kwenda huko..! ati polisi wamefundishwa na kwa hiyo hawawezi kuua raia.. damn wanakera sana hawa..
 
Mbona alianza kuongea pumba kabla hata hajafika eneo la tukio? Kwani hata kama lilikuwa kundi la wahuni polisi bado wanayo nguvu ya kuua wahuni bila ya sababu za msingi? Sioni kama tuna viongozi tena ila limebaki kundi la wazee wanajitengenezea pensheni.
 
Yes siku hizi jeshi la polisi limekuwa ni mahakama, linatoa hukumu kali kabisa ya kuua wahuni. Mtu akiwa muhuni tu, ni halali ya polisi kumfyatua risasi. Kauli za huyu Bwana ni kituko namba moja kwa mwaka huu wa 2012!!! There are still more to come, keep tuned.

Tiba
 
inawezekana akapatikana juha alie afadhali mkuu.. Imagine ametumwa kwenda kuchunguza.. lkn ameanza kutetea kabla ya kutoa nyayo zake hapa kwenda huko..! ati polisi wamefundishwa na kwa hiyo hawawezi kuua raia.. damn wanakera sana hawa..
mimi nadhani polisi nao wamechoka kwa hiyo wameanza mgomo, na huo ndo mgomo wao nikuua tu mpaka serikali itoke madarakani!
 
Yes siku hizi jeshi la polisi limekuwa ni mahakama, linatoa hukumu kali kabisa ya kuua wahuni. Mtu akiwa muhuni tu, ni halali ya polisi kumfyatua risasi. Kauli za huyu Bwana ni kituko namba moja kwa mwaka huu wa 2012!!! There are still more to come, keep tuned.

Tiba

UMEONA MKUU ADHABU YA WAHUNI NIKUUA TUUU, ndo maana kinondoni mateja wanakula unga hadharani na polisi wanawaangalia tuu nchi hii bana!
 
Soma habari hii halafu utaelewa kwa nini chagonja anapaswa kufukuzwa kazi polisi..

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta saidi mwema ametuma kikosi cha maofisa waandamizi kutoka makao makuu ya jeshi hiko, kikiongozwa na Mkurugenzi wa operesheni na mafunzo kamishna Paul Chagonja kwenda mjini songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo.
Chagonja akiongea na mwananchi jana alisema maandamano hayo hayakuwa ya amani bali ya kihuni kwani yalilenga kuvamia ofisi za serikali ikiwamo ikulu ndogo na ofisi ya mkuu wa mkoa.
Chagonja alikuwa akijibu swali lililotaka aeleze ednapo haoni kkama polisi imetumia nguvu kubwa kutawanya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani.
"maandamano yamani watu wanavamia ikulu, maandamano ya amani watu wanazingira ofisi ya mkuu wa mkoa?"
"sijafika huko ndio naelekea lakini yale si maandamano ya amani. Yaani wahuni wanataka waachiwe? Kuweni wazalendo , miswe kama labda ninyi ni waandishi wa BBC kutoka uingereza, hii ni nchi yenu"
Alifafanua kwamba maandamano ya amani yanafahamika kwani watu hulazimika kuomba kibali na kuweka wazi ajenda ya maandamano. "lakini siyo maandamano yale, hayakuwa na kibali chochote wahuni tu wamejiingiza wanataka kuvuruga nchi"
Mkuu huyo wa operesheni alitetea polisi akisema; "ucifikirie polisi hawana akili. Haiwezekani watu wazima na akili zao wenye mafunzo wafyatue ovyo risasi za motokwa raia. Hakuna askari anapenda kuua raia, lakini watu wanavamia ikulu, ofisi ya mkuu wa mkoa magari ya polisi, hapo kuna amani kweli?"
Alitoa angalizo kwamba ni lazima hata vyombo vya habari, viache ushabiki na badala yake viangalie maslahi ya taifa kwani nchi ikivurugika wao pia hawatasalimika na kusisitiza: "kuweni wazalendo bwana, msifikirie kulishutumu jeshi la polisi tu"

Source: Mwananchi

Wana jamii hayo ndo maneno ya kiongozi wa kikosi cha kwenda kufanya uchunguzi wa mauaji yaliofanywa na polisi huko songea.. anatetea askari wake hata kabla ya kufika na kufanya uchunguzi..

haki itatendeka kweli..? anafaa kuendelea na wadhifa wake huo..?
Amelewa madaraka huyo anastahili astahafishwe kwa manufaa ya umma, kama kiongozi wa umma anakwenda kwenye uchunguzi alishakuwa na conclusion kwamba walioandamana ni wahuni ni bora asiende
 
Ana akili za panzi! Huwezi ukawaita wananchi wahuni wakati wanakwenda kuwasilisha madai yao ya msingi! Madai ambayo yanatokana na polisi kushindwa kutimiza wajibu wao!

CHAGONJA YEYE MWENYEWE NDIYO MUHUNI!
 
Huyo bwana asiende huko, anamaliza kodi za wananchi buree! Kisha chakachua ripoti kabla hata hafika eneo la tukio
 
Nimesoma habari hii kwenye mwananchi na mpaka sasa nashindwa kumuelewa huyo bwana mkubwa. Kumbuka kwamba yeye ndo anaongoza hiyo timu inayokwenda kufanya uchunguzi huko Songea lakini tayari anakwenda huko akiwa na majibu ya nini kilitokea, kwa nini na nani ni mwenye makosa. Uchunguzi anaokwenda kufanya ni upi sasa? Katika hali ya kawaida ilitakiwa hayo anayoyasema awe ameyapata baada ya kufanya uchunguzi!! Hii kwangu ni kama kuonyesha ni jinsi tunatumia rasilimali chache tulizonazo kuunda tume nyingi zisizokwisha wakati tayari watu wana majibu ya hicho wanachoenda kuchunguza!! Ni aina nyingine tu ya kutengenezeana ulaji.
 
Mkuu aondolewe awekwe nani yaani jk anamaboga akitoa anaweka matikiti maji,
NIMECHOKA NA KUMPA USHAURI JK BWANA.
KILICHOBAKI NI KUBOMOA TUTAJENGA KESHO!

hahaaaa bora matikitimaji kaka...maana tukiwa na hangover unakula kupunguza hangover
 
Inasikitisha kama kweli yeye ndio katumwa kuongoza jopo,IGP Mwema afanye maamuzi ya kuteua mwingine yeye arudi DAR na pia achukuliwe hatua za Kinidhamu
 
Maandamano ya "wahuni" yaliyodhitiwa Kihuni na sasa Mhuni mmoja anayekwenda kuchunguza kaanza kwa kutoa majibu ya Kihuni......

Maelezo yake yanapishana na ya Kagasheki (NW-Mambo ya Ndani). Cha kushangaza waandishi hawakuuliza "Jeshi la polisi linaruhusiwa kuua wahuni"??????
 
Inasikitisha kama kweli yeye ndio katumwa kuongoza jopo,IGP Mwema afanye maamuzi ya kuteua mwingine yeye arudi DAR na pia achukuliwe hatua za Kinidhamu[/QUOTE

Hawezi fanya hivo,,hatuna utamaduni huu,japo kwa wenzetu huko kauli hiyo ilishakuwa kubwa mno ya kumwajibisha mtu! lkn Mwema nae bingwa wa magumashi,, iko wapi report ya tume iliyochunguza uhalali wa Jerry Muro kumiliki Pingu, ile ya vigogo(charlesmkumbo) waliotuhumiwa kupanga njama za kumbambikia drugs mtoto wa mebgi? nk?
 
Inasikitisha sana kuona yule anayetarajiwa kuongoza uchunguzi tayari ametoa hukumu kwa watu waliouawa, eti ni wahuni!!! jamani! unyama huu utaisha lini? kwa nini jeshi la polisi siku hizi linaona raia wa Tanzania hawana thamani!!!
 
he has arleady ruled out then why should he go there?My advice is that wanasongea to refuse giving any assiatance to him because nothing will favour them.
 
Tangu lini mtu form 4 with failure akawa mchunguzi, hata hatua za investigations hazijui ndiyo maana anaanza kuwa bias kabla hajafika eneo la tukio. Ndo polisi wetu hawa, wakija kutibiwa huwa natamani niwaache, lakini hofu ya Mungu ndo inanisaidia. Waache tu adhabu yao Mungu anajua.
All the best ila ajue ndugu zetu wamekufa na polisi lakini pia na mchinjachinja.
 
Yuko biased,hiyo tume imeji disqualify haiwezi tena kufanya investigation,kama ni kula nights waende tu wakatembee,lakini kama ni upelelezi hawafi kwani majibu ya uchunguzi wanaoenda kufanya tayari tunayo
 
Back
Top Bottom