Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 473
- 1,682
Nimemsikiliza pasipo shaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuhusu wachezaji wa Tabora kutumiwa sms za kuombwa wazubae kesho ili timu yetu ya Jangwani ipate matokeo, ni kweli anachosema RC kuwa makosa ya rushwa kumtia hatia mtu ni vigumu sana wakati mwingine kwa sababu anayetoa rushwa anafanya vile kwa mbinu nyingi ili asiingie hatiani, ndio maana mahakama huwa wana msemo wao, proof beyond any reasonable doubt, yaani uthibitisho au ushahidi pasipo shaka yoyote, kwa vyovyote vile mtoa rushwa hawezi kutuma hela kwenye simu anajua atapotea, kwa hiyo anatanguliza meseji ya kukuomba ulegeze ili kesho akiona kweli umelegea basi jioni ndio anakutafuta kwa kukutumia muamala kwenye namba nyingine.
Pia soma: Pre GE2025 - Mkuu wa mkoa wa Tabora atoa ahadi ya milioni 60 kwa Tabora United akiifunga Yanga
Mkuu wa Mkoa wa Tabora ni mtu makini sana, kwanza ni mteule wa kiongozi namba moja nchini, hawezi kuona mkoa wake unashuka kimichezo kwa mambo ya kijinga jinga, Tabora zamani ilikuwa ndio kitovu cha soka, kulikuwa na timu ikiitwa Mirambo, kaka hii timu ilikuwa balaa, sisi tuliokuwepo enzi zile tuliiona hii timu, acheni tu.
Watu wanapambana kusajili wachezaji wazuri ili kuletea mafanikio mkoa, wengine wanashiriki kuzihujumu timu za mikoani ili waonekane wako vizuri, hapana.
Tunaweza kudhani kuwa RC anafanya mzaha lakini kwa level yake kutoa tuhuma zile maana ameongea na wachezaji na amebaini viashiria vya rushwa.
Ally komwe tangu juzi yuko Tabora ameenda na watu wake mapema kabisa kufanya nini kama sio kuleta mzaha katika mpira wetu.Halafu kijana amenikera mno kumdhihaki Mkuu wa Mkoa, mtoto amekosa kabisa adabu, mbona Hersi hamjibu majibu hovyo au kwa sababu anakupa kula, mjinga mkubwa huyu mtoto, amenikera sana.
Nawashauri Tabora chezeni boli lakini leo Utopolo watatoa kafara la ng'ombe 40 huko Tabora wakidai wana sikukuu ya Idd, sio kweli, viongozi wa Tabora kama mnasoma hapa, hilo kafara la damu hilo, majini yao utopolo yanataka furaha leo, na furaha yao ni damu, nawaomba sana kama mna watu wazuri nje ya uwanja wekeni sawa hili jambo, vinginevyo kesho mtakoga mabao mengi sana hapo uwanjani.