Patroli, dizeli, mafuta ya taa bei juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Patroli, dizeli, mafuta ya taa bei juu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)


  Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za aina zote za mafuta za jumla na rejareja zitakazoanza kutumika kuanzia leo, ikiwa ni siku mbili tangu matumizi ya kanuni ya zamani ya ukokotoaji wa bei ya mafuta kuisha.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Ewura jana, kutokana na kanuni hiyo mpya, kuanzia leo jijini Dar es Salaam, bei ya rejareja ya petroli itakuwa Sh. 1,956 wakati bei ya dizeli itakuwa Sh. 1,977 na bei ya mafuta ya taa itakuwa Sh. 1,963 kwa lita.

  Katika bei ya jumla, petroli itakuwa Sh. 1,881.92, dizeli (Sh. 1,903.04) na mafuta ya taa (Sh. 1,888.59).
  Miongoni mwa mambo muhimu yaliyomo kwenye kanuni hiyo mpya, ni pamoja na tozo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

  Tozo hiyo imeongezeka kutoka dola za Marekani 8.30 hadi dola za Marekani 10 kwa ujazo wa tani moja, pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

  Pia Ewura itaendelea kuchapisha bei kikomo kwa wafanyabiashara wa jumla na rejareja na kwamba taasisi zote zinazotoza tozo kwenye kanuni hiyo, zitalazimika kutoza kwa mujibu wa maagizo ya kanuni hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...