PreGE2025 Patrick Kipangula: Waandishi watakaogombea Uchaguzi Mkuu wasijihusishe na Majukumu ya kihabari

PreGE2025 Patrick Kipangula: Waandishi watakaogombea Uchaguzi Mkuu wasijihusishe na Majukumu ya kihabari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imewaagiza Waajiri wa Vyombo vya Habari kuhakikisha kuwa Waandishi wa Habari wanaogombea nafasi za kisiasa wanasitisha utekelezaji wa majukumu yao ya kihabari kwa kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa leo June 21,2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Patrick Kipangula imesema “Kwa kwa kuzingatia uwepo wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu, na kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 12(g) ya Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa (Tangazo la Serikali Na. 775 la tarehe 18 Septemba, 2020).

Aidha, Waandishi wa Habari ambao ni Wagombea wa nafasi za kisiasa wanapaswa kuzingatia kwamba hawajihusishi katika shughuli au majukumu yoyote ya kihabari katika Vyombo vya Habari walivyoajiriwa kwa muda wote wa mchakato wa uchaguzi” “Hatua hii inalenga kuzuia mgongano wa maslahi na kulinda uaminifu wa Vyombo vya Habari mbele ya umma, hususan katika kipindi cha uchaguzi”
images.png

Chanzo: Millard Ayo​
 
Nadhani hivi ndivyo Sheria inavyotaka

Soma,Pia: Patrick Kipangula: Waandishi watakaogombea Uchaguzi Mkuu wasijihusishe na Majukumu ya kihabari

Screenshot_2025-06-22-00-49-56-1.png
 
Sio waandishi wa Habari tu ropo ropo wote machawa wote

Huwezi kutumikia mabwana wawili.

Hawa ni matapeli sema CCM ni chama Cha wauni tu we unawezaje kuwa mgombea wa chama halafu muda huo unaandika Habari au unatangaza Habari redioni na kwenye television?
 
Back
Top Bottom