Pata kufahamu makundi manne ya tabia za binadamu kisha jitathimini wewe uko katika kundi gani

Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria
hizo ni:-
Kategoria hizo 2 zipo wapi mkuu? Au ndio introvet na extrovet?
 
Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni:-

1. MELANCHOLIC

Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo:

  • Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
  • Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
  • Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
  • Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
  • Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
  • Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo
  • Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewaWanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo) Wakata tamaa wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
  • Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyaoNi wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
  • Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe-Wana busara na hekima nyingi-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
2. PHLEGMATIC
  • Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
  • Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
  • Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
  • Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
  • Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
  • Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
  • Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
  • Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)-Si watu wanaojali muda na ratiba
  • Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
  • Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
  • Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
  • Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
  • Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
  • Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.
3. SANGUINE
  • Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
  • Ni wacheshi sana
  • Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
  • Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
  • Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
  • Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
  • Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
  • Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya
  • Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
  • Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
  • Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
  • Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
  • Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
  • Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
  • Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
  • Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
  • Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
  • Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
  • Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
  • Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
  • Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa.

4. CHOLERIC
  • Wana uwezo wa kawaida kiakili
  • Ni wa wakali na wakaidi
  • Hawana huruma wala unyenyekevu
  • Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
  • Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
  • Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa-Watu wasiokata tamaa mapema
  • Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
  • Kundi la watu wenye nguvu nyingi
  • Ni madikteta
  • Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
  • Watu wa kulipiza visasi-Watu wa vitendo kuliko maneno
  • Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
  • Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
  • Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
  • Hawajui kubembeleza
  • Hawaongei wala kucheka ovyo
  • Si watu wanaopenda suluhu na amani
  • Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
  • Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
  • Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
  • Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc
BAADA YA KUJITAFAKARI WEWE , EMBU TAFAKARI TENA KIONGOZI WAKO WA TAIFA YUKO KWENYE KUNDI GANI?
Aiseee..kundi la tatu...naona lina lenga kbsa maisha ya mtu hapa...🤭
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom