Pata kitabu kipya "Dokta John Magufuli: Safari ya urais, mafanikio na changamoto"

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
5188-dokta-john-pombe-magufuli.jpg

Heri ya mwaka mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, "Dokta John Pombe Magufuli: Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake" sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016.

Kitabu hiki cha Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.
Kadhalika, utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.

Sura ya kwanza inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.

Sura ya tatu inaelezea fursa alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika kipindi cha kampeni na uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua uimara wa mwanasiasa huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika kila uchaguzi. Kwa uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu yaliyopelekea urahisi kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu Lowassa, sambamba na mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.

Sura ya nne inajadili changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla wakati wa kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na UKAWA walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.

Sura ya tano inajadili urais wa Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya mwisho inajadili changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa mapendekezo.

Nimejitahidi kadri nilivyoweza kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia uchaguzi huo kwa karibu. Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa 'niliisapoti CCM na Dokta Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono UKAWA na Lowassa.' Naomba kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha kiitikadi bali kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.

UTAKIPATAJE?

Bei ya kitabu sasa ni Shilingi 4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba 0744-313-200 jina JOHN ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina CHRISTINE JOHN MANONGI
 
Vijana wa lumumba mnajitutumua lkn ndio hivyo tena chama hakiwaoni zaidi ya kabuku7.
 
Mi nakiitaji na niko tayar kukinunua ila sihishi Dar es Salaam, Je? Nakipataje?
 
Ni mafanikio gani ambayo muandishi anaweza kuwa ameyaonyesha ndani ya huu muda mfupi tu ambapo hata rais mwenyewe hawezi kusimama jukwaani akasema ameyapata!
changamoto ni nyingi mno kwenye masuala ya msingi ambayo yangekuwa ni kipimo kwa mwanchi wa kawaida,masuala kama ya elimu bure ambapo bado kuna maeneo wazazi wanalalamika kutozwa pesa za chakula kama ilivyotokea siku chache bagamoyo.
Majibu yanayohitaji utumbuzi bado ni mengi kwenye vyombo vingi vya kutoa huduma kwa jamii kama vile HAKI,ULINZI NA USALAMA,bila kuach kwenye AFYA,bado mahospitali hayana dawa na vifaa tiba na maslahi duni kwa wafanyakazi wa sekta hiyo.
"MATAJIRI"WATUMISHI WA UMMA na kipato cha utata wako wengi,pato la taifa na thamani ya shilingi bado ni jipu.
Bei ya nishati ni kikwazo kwa maendeleo na kadhalika.
Sioni kwanini muandishi amekimbia kutaja mafanikio wakati Rais amechujua ofisi juzi tu hajatimiza hata nusu mwaka kwa safari ndefu ya moaka mitano
 
Hilo nalo jipu....huyu muandishi anataka kupiga hela tu ....siajabu hatari masolex Hana taarifa ya ukuwepo wa kitabu hichi

Ovaaa
 
Mpongezeni mwenzenu kwa kutumia akili yake na kuja na kitu kama hiki.

Wekeni Siasa pembeni.

Pengine yeye ndie Mtanzania wa kwanza kutoa kitabu hicho, na kuna wengine watakaofuata mkondo, wakatoa Vitabu vyao kivingine kuhusiana na Rais Magufuli.

Mwandishi wa Kitabu hongera sana
 
Back
Top Bottom