Pastor Shepherd Bushiri, wife arrested for 'fraud & money laundering'

Utapeli ni ile hali ya mtu kutumia maneno laini na matamu na kujifanya kutaka kumsaidia huyo mtu ilihali Yule anaejifanya kutaka kumsaidia moyoni mwake anakuwa na Mawazo yenye hila kama vile kutaka kumwibia mtu!
Utapeli ni ulaghai!
Tofauti ya tapeli na jambazi ni kuwa Tapeli anatumia maneno matamu na laiini kumwibia mtu wakati jambazi anatumia nguvu kumwibia mtu!
Lakini wote ni wazi tu!
Lengo Lao ni moja!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe mkristo? km y7esu angekuwa anawahimiza wafuasi wake wamtolee Mungu then hizo mali angekuwa anazfnta za kwake angekuwa tajiri kiasi gan? hawa wachungaji wa leo wanaojilimbikizia mali kutoka kwa waumini wao wanafuata mfano wa yesu yupi maana yesu hakuwa hvyo, ni nabii gani ambaye aliwahi kutajirika na kwa kukusanya mali za wafuasi wake? ww unasema tumtolee mungu bt mwsho wa siku ww ndio unakua bilionea je unaweza kueleza ni kivp waliotoa walimtolea mungu km si uongo, ona sasa anakamatwa kufny fraud
 
Kwa hiyo unamhukumu kwa sababu yeye ni mwafrika au?? Umeshawahi kumsikia Prophet Lukaku?? Unajua ukwasi alionao?? Somo lako ati kwa nini atumie mali zake anunulie magari na madege sidhani ka unamfanyia mema. Kwa nini umwambie alichokipata asikitumie atakavyo??
Sijawahi kuzipata hizo hela lakini, siku Mungu atanifungulia mlango nadhani utanichukia. Nasema, unamhukumu kwa sababu sio wewe umeshika hicho kijiko cha dhahabu. We ungetisha
 
Sina moyo wa kubishana ila ungetaka kuelewa ungeelewa. Yesu hakuhitaji mali kwani zilikuwa ni zake. Tena alijua zilipo. Unakumbuka alipoulizwa kodi alimtuma wapi Petro kuichukua hiyo kodi??
Nasema hivi;
Yule ni mtumishi wa Mungu wake. Mwambieni tajiri wake yaani aliye muajiri amshughulikie.
 
Nimecheka sana Mkuu. Niliwahi kupelekwa hapo wakati fulani na moja ya mtu wangu wakaribu. Siku ya kwanza nikawa sielewi na yeye akawa ananiambia utaelewa tu. Hapa ni pazuri sana. Nikasema ok. Ila hata miezi miwili haikupita niliacha. Naona ibada ya kibinadamu zaidi na siyo ki Mungu.. tunamtukuza sijui g(G) wa Major one ambaye simjui ni Mungu au mungu yupi. Wakianza kumnyenyekea huyo kiongozi wao sasa... nilikuwa nachoka rohoni.
Niseme tu kwamba makanisa kama haya yana waumini wao.... ndiyo kama uliowaona. Pale wanafundishwa Miujiza... ila ukiwauliza mistari ya Biblia ni changamoto.. bado uvaaji wao sasa... Niliona juzi kiongozi wao kaandika kuwajibu Haters ni aibu kwa Kiongozi anayelisha kondoo elfu.... elfu. Hawa ndiyo wanafanya Ukristo na Jina la Yesu linatukanwa na kudhihakiwa. Mungu awape macho ya rohoni waweze kuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa mkuu hamna haja ya kugombana kisa tuna mitazamo tofauti
 
Anguko lao huja kwa haraka....

Jr
 
Halafu si ajabu hata hujawahi kumwona huyo Bushiri ka mimi. Wala sina haja ya kwenda kumwona pia.

Tulia mkuu Nenda kampigie magoti yule msela Bushir huku ukimuita eti 'dadiiiiiiiiiiiiiiii',hahah


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…