Pasipoti za TZ Bara zapigwa marufuku Zanzibar Heroes

Tofauti Wanzanzibari tu ndiyo wanaruhusiwa kuchukua passport Zanzibar. Now you see it!
Sasa Mzanzibar akichukulia Tanganyika passport ya Zanzibar kunabadili Uzanzibar wake?

Ningekuwa JPM ningekavunja ka Muungano tuishi ujirani mwema kama Kenya tu!
 
Dr Shein passport yake kachukulia Tanganyika na kaweza kuwa rais wa Zanzibar lakini kuchezea team ya Taifa ya Zanzibar hatimizi vigezo vya uraia.
Hahaha hahaha,
haya bhana Zanzibar daima.
 
Kwa hiyo timu ya Znz siku ikicheza wataimba wimbo wao wa Taifa la Znz,he Timu ya Tanganyika inayojiita kwa sasa bila aibu ijajiita Tanzania bara,siku wakicheza wataimba wimbo gani wa Taifa?au kuna wimbo wameuficha wa Tz bara utaanza kutumika?
 
Imechelewa. Hoja binafsi inaandaliwa kwa CAF kuitaka TFF kwacha kutumia jina la Tanzania katika mashindano na badala yake watumie jina lao halali la Tanganyika. Hoja hapa ikitikea Yanganyika kushindiliwa mabao kama kichwa cha mwendawazimu kiwe chao na sio kichwa cha Mtanazania.

Pasipoti sio gamba. Kama ni gamba basi iko sawa na ya Nigeria. Psipoti inayotolewa Zanzibar ina "Signatories" tofauti na ya bara na pasipoti ya upande mmoja huwezi kuongeza muda upande mwengine.

Kumbuka kama siasa haitatibua Zanzibar ina " proffessional " wengi wanachezea timu na madaraja mbambali nchini Uingereza na tayari wana umoja wao. Sasa wala Sembe (DONA) na urojo tutaonana mwambani. Kichwa cha mwendawazimu kitaridhihika.

Sio kweli, na uache kudanganya umma, jina la Tanzania litaendelea kutumika kama kawaida.
 
Kwa hiyo timu ya Znz siku ikicheza wataimba wimbo wao wa Taifa la Znz,he Timu ya Tanganyika inayojiita kwa sasa bila aibu ijajiita Tanzania bara,siku wakicheza wataimba wimbo gani wa Taifa?au kuna wimbo wameuficha wa Tz bara utaanza kutumika?

Kwani China akicheza v Hong Kong zinapigwa nyimbo gani? Au England v Scotland zinapigwa nyimbo zipi?
Au unafikiri Tanzania v Zanzibar ndio itakua mechi ya kwanza kwa nchi zilizo pamoja?
 
Sio kweli, na uache kudanganya umma, jina la Tanzania litaendelea kutumika kama kawaida.
Sikupotoshi kwa vile sina uwezo huo lakini huo ni ukweli. Watu kama yie Wiki tatu nyuma angeambiwa Zanzibar inaomba uwanachama CAF mngeruka na kusema haiwezekani, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya Tanzania,wanajidanganya.

Kweli ilipodhihiri wamerudi Ethiopia vichwa chini kwa kuona haya na aibu. Na hili liko kikaangoni linangojewa kuiva tu.
 
Kwa hiyo pasipoti hizo zitakuwa za kusafiria wakati wa michezo ya CAF tu then nchi zingine watatumia za wapi?
 
Machi 16, 2017 Zanzibar imeingizwa rasmi kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya kukubaliwa kwa kura 51 kati ya 54 zilizopigwa na nchi wanachama wa CAF.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa ZFA Ali Bakar ‘Cheupe’ amesema kuwa wachezaji watakaoitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar ni kwa wale ambao Pasipoti zao zimetengenezwa visiwani Zanzibar.

Kwa maana hiyo, wachezaji wote wa Zanzibar ambao Pasipoti zao zimetengenezwa Tanzania bara hawatakuwa na sifa ya kuitumikia Zanzibar Heroes.
Kuna tofauti gani kati ya pasi ya Tanzania iliotengenezwa Zanzibar na iliotengenezwa Dar?waziri ni yule yule,kamishna ni yule yule,rangi ni ile ile na nembo ni hiyo hiyo.
Haishangazi wazanzibari kuambiwa msubiri Sefu atapewa serikali yake,muda unakwenda nanyi kwa ujuha kama huu wa kushangilia pasipoti mnakenua tu
 
Kwanini kule kuitwe Zanzibar na huku kuitwe Tanzania bara? kama kule kwaitwa Zanzibar basi na huku kuitwe Tanganyika. Na kama huku kwaitwa Tanzania bara basi na kule kuitwe Tanzania visiwani.
Ni Tanganyika hakuna namna mukita jina ndio hilo Tanganyika kwa taarifa zaid mscotish hachezi England passport in ile ile UK
 
Mk
Kuna tofauti gani kati ya pasi ya Tanzania iliotengenezwa Zanzibar na iliotengenezwa Dar?waziri ni yule yule,kamishna ni yule yule,rangi ni ile ile na nembo ni hiyo hiyo.
Haishangazi wazanzibari kuambiwa msubiri Sefu atapewa serikali yake,muda unakwenda nanyi kwa ujuha kama huu wa kushangilia pasipoti mnakenua tu
Mkuu kwenye passport kunasehem imeandikwa pahali ulipozaliwa ukipeleka cheti cha kuzaliwa kama umezaliwa Zanzibar pataandikwa Zanzibar ukipeleka cheti kimeandikwa tabora utajuilikana wewe no mtanganyika ndio tofauti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom