Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Machi 16, 2017 Zanzibar imeingizwa rasmi kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya kukubaliwa kwa kura 51 kati ya 54 zilizopigwa na nchi wanachama wa CAF.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa ZFA Ali Bakar ‘Cheupe’ amesema kuwa wachezaji watakaoitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar ni kwa wale ambao Pasipoti zao zimetengenezwa visiwani Zanzibar.
Kwa maana hiyo, wachezaji wote wa Zanzibar ambao Pasipoti zao zimetengenezwa Tanzania bara hawatakuwa na sifa ya kuitumikia Zanzibar Heroes.