Paschal Mayalla - Sasa upo kwenye reli ya Uandishi wa Habari ni si uchawa tena

Paschal Mayalla - Sasa upo kwenye reli ya Uandishi wa Habari ni si uchawa tena

Full Blood Picture

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2021
Posts
3,890
Reaction score
7,889
Umeongea kwa ufasaha, utulivu na hoja zenye mashiko, jambo linalodhihirisha si tu uwezo wako wa kujieleza bali pia upeo wako wa kufikiri kwa kina. Ni wazi kuwa umejiandaa kwa umakini mkubwa; umechambua mada kwa ustadi na kuwasilisha ujumbe kwa namna ya hali ya juu sana. Mtiririko wa mawazo yako ulikuwa mzuri, lugha uliyoitumia ilikuwa kisomi hasa na yenye mvuto, na mifano uliyotoa ilisaidia kuifanya hoja iwe rahisi kueleweka na kukubalika.
View: https://www.youtube.com/watch?v=cuG7jB7SbAY

Endelea kung’ara na kuleta mijadala yenye tija kwa jamii, kwa sababu mchango wako una nafasi muhimu katika kukuza uelewa na kujenga fikra chanya. Umerudi kwenye kiwango chako cha mwandishi mwenye uzoefu mzuri japokuwa hapo nyuma ulilegalega na kuwa chawa fulani. Nashukuru sasa uchawa umeisha. Ni wazi kwamba wewe sasa si mtu wa uandishi njaa tena.
 
🤣🤣akipelekwa mahakamani utatoa msaada
 
Back
Top Bottom