Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!

Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti hilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"

Gazeti hilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.

Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.

HOJA.

Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?

Hapa naomba nieleweke, hata watumishi wa idara nyeti walianza kufatilia gazeti hilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.

Kwanini walifuatilia, kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100% ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.

Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?

Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.

Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?

Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.

Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.

Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.

Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure."

======

Mkuu Hufi Leo, kwanza sikujitokeza kujibu tuhuma hizi kwa kuzipuuzia tuu kuwa kwa vile huu ni uongo na uzushi, uongo mwingine na uzushi ukiuupuuzia tuu utayeyuka na kupita tuu kama upepo hivyo nilipuuza kwa matumaini ni upepo tuu na utapita. Lakini leo baada ya kifo cha mama yake, nimeona nisiendelee kunyamaza hivyo ndio nimejotokeza leo na kukujibu in points format.

Hatua yangu ya kwanza, ni kutuma Salaam maalum kwa rais Magufuli.

Kisha nikawaka hoja zako in points format ili kujibu kila hoja
  1. Hukuna uthibitisho kuwa ni andiko langu lilipelekea jarida hilo lifuatiliwe, hakuna uthibitisho wowote kuwa sasa jarida hilo linafuatiliwa na hakuna uthibitisho wowote kuwa Eric Kabendera ndie mwandishi wa makala mimi nilizokuwa nazileta humu.
  2. Mimi sina uthibitisho wowote kuwa watu wa Idara nyeti walianza kufuatilia jarida lile baada ya bandiko langu humu jf, lakini kwa vile hata sisi humu jf hatujuani nani ni nani, its good to know that na pia sikuwahi kumjua mwandishi wa makala zile, I'm now learning from you.
  3. Kwenye makala zangu nilikiwa naweka kila cha kweli na cha uongo, niliukubali ukweli na kuupinga uongo na sio kwa lengo la kujipendekeza kwa Msukuma mwenzangu. Kazi ya mwandishi wa habari ni kusema ukweli na kuandika ukweli, mimi ni mkweli, msema kweli na mwandika ukweli bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au kumchukiza nani.
  4. Naendelea kusisitiza sikuwahi kumjua mwandishi ni nani, ila hata ningemjua, as long as anachoandika ni kweli, bado nisinge muita mwandishi yoyote kumuonya kwa kazi yake yoyote bali bado ningeendelea kukosoa au na mimi kuandika makala zangu kwenye magazeti yangu ninayoandikia. Hapa nilipo kuna waandishi wengi critical tunafahamiana na kuheshimiana, andiko lolote linajibiwa kwa andiko na sio kwa kuitana.
  5. Hii ni personal opinion, kuna watu wenye roho za kishetani ambao wanafurahia binaadamu wenzao wanapopata matatizo, very unfortunately mimi sii miongoni mwa watu wa kundi hili, wanaonijua wananijua na wanaonisoma, wananisoma.
  6. Kwavile tangu mwanzo sikujua kama ni Eric Kabendera wala sikujua nini kitatokea, pia hili sikulijua.
  7. Hili sii kweli.
  8. Ungeliweka hilo andiko
  9. Waandishi wa habari hawawezi kulifanya hili.
  10. Nimeunga mkono rai yako.
Nampa pole sana Eric Kabendera kwa mapito anayopitia.
 
Ha ha ha ha ha, Pascall Mayalla Mungu anakuona eti. Wakati bwana Erick Kafrag akipambana kutoa shombo zake kupitia gazeti la Mabeberu wewe ulikuwa busy kuzipandisha shombo zake kwa mbwembwe na nakishi za kutosha humu jamvini. Ona sasa mwenzako yuko nyavuni. Mungu anakuona bro.
 
Hili linatoka moyoni mwangu, KAMA KUNA MTU MKABILA, MKABILA, ALIYETUKUKA NI Pascal Mayalla, A Tribalist and defined as : an advocate or practitioner of strong loyalty to one's own tribe or social group.

Pascal haoni doa lolote katika Jiwe, anamuona kama malaika Gabriel! Huyu naye akiwa Rais uwaja wa ndege utajengwa chooni kwake (if that could be possible anyway, he can dare do that!).

Mayalla namuheshimu sana enzi zake kabla ya Jiwe, sasa siye kabisa.
 
Pascal was making the article popular. Kumuingiza kwenye huo ushetani ni kumuonea kwa kwel
Pascal Mayalla ni "Panya" smart sana ajuaye vyema kung'ata huku akipuliza.

Binafsi naheshimu uamuzi wake wakuzileta humu JF Makala Zile za lile Jarida kwa minajili kwamba alikuwa akimtetea Mkulu dhidi ya aliouita "Uongo na Matusi Yao kwa Mh. Rais" ingawa kwa hakika alikuwa ndio anafanya jukumu la kusambaza articles husika kwani kupitia Yeye wapo Wana JF wengi ndio walikua wanasoma hizo articles, at the same time he exaggerated a lot.
 
Mkuu to be honest haujaonyesha Ushahidi wenye nguvu wakuweza kutushawishi na kutuaminisha kwamba "Pascal is behind the scene " naomba kusanya Valid and Tangible evidences kinyume na hapo itakuwa ni tuhuma tu ambazo hazina mashiko.
 
Back
Top Bottom