johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Ni katika mjadala wa waandishi kwenye kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari.
Pascal anasema bajeti ya nchi inatakiwa kuwasilishwa kitaaluma lakini juzi waziri wa fedha Dr Mpango ametumia muda mwingi katika kusifu ukilinganisha na kuifafanua bajeti.
Mwandishi Moses Methew alimpinga Pascal kwa madai kuwa Dr Mpango alizitumia vizuri dakika 60 za mwanzo hivyo hakuna ubaya wowote kutumia dakika 135 zilizobaki kusifiana.
Moses amesema hata Pascal Mayalla mwenyewe katika dakika 10 alizopewa kwenye mjadala huu ametumia dakika 7 katika kusifu na mgeni wake kamwachia dakika 3 tu.
Katika kujibu Pascal amedai yeye husifu kimantiki siyo kama wafanyavyo wale Mataga na wala hatafuti Uteuzi kama rafiki zake wa Jf wanavyomzushia.
Mwisho mwandishi Moses Methew amevilaumu vyombo vya habari na bunge kwa kutumia muda mwingi kujadili mambo binafsi na faragha za Mbowe.
Amesema inasikitisha kuona bunge zima linajadili " maisha binafsi " ya Mbowe kana kwamba Mbowe ndio bajeti ya serikali.
Chanzo: Star tv
Maendeleo hayana vyama!