Pasaka njema -part 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pasaka njema -part 2

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 21, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Kosa Lilelile; Why?  [​IMG] st1\:*{behavior:url(#ieooui) }
  [FONT= ]Kuna usemi wa kingereza usemao “The more mistakes one makes in life, the smarter one gets in life” ingawa huu usemi hukubalika katika baadhi ya maeneo ya maisha, linapokuja suala la mapenzi au mahusiano huwa kitu kigumu.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Kwenye mapenzi na mahusiano makosa mengi huendelea kujirudia kila leo, wapo wanawake hujikuta kila wanapotafuta wapoenzi huangukia kwa wanaume ambao huishia kuwatesa na kuwaumiza kwa style ile ile. Na wapo wanaume ambao huangukia kwa akina dada walewale ambao huishia kutafuna pesa zao na kuishia.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Wengi tunaamini kwamba mahusiano yanapoenda vibaya yanaweza kusaidia kufungua macho ya muhusika ili siku akimpata mpenzi mpya aweze kujifunza na kutorudia kosa lilelile. [/FONT]​
  [FONT= ]Hata hivyo imekuwa tofauti Kwenye mapenzi kwani wanaume na wanawake wenye njaa ya kupendwa hujikuta wamenasa Kwenye mtego uleule ambao waliukimbia kwa wapenzi wa zamani na kuendelea kuumizwa zaidi.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Mbaya zaidi ni pale ambapo tumeona wanandoa ambao wametoka familia zenye tatizo (wazazi kupigana, kuachana nk) nao wamejikuta wanandoa za aina hiyohiyo.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]MFANO:[/FONT]
  [FONT= ]Jane anaelezea kwamba “John ni mwanaume smart, mwenye mafanikio na ambaye akiingia mahali popote si rahisi usishtuke kwa namna anavyovutia, anasema alikutana naye katika sherehe za ofisi yao na haikuchukua muda wakawa wapenzi hata hivyo baada ya miezi 3 alimuona John ni mwanaume mwenye wivu kupindukia na anaweza kukudhalilisha hata mbele za watu, akaamua kuachana naye.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Baada ya miezi sita akampata kijana mwingine mwenye sifa kama za John na wakapendana na kuwa wapenzi hata hivyo baada ya miezi 2 akajikuta amenasa Kwenye mtego wa mwanaume yuleyule kama John.[/FONT]​
  [FONT= ]Swali la Jane lilikuwa kwa nini kila mara nikipenda mwanaume naangukia kwa mwanaume mwenye tatizo linalofanana, anasema anaogopa kupenda sasa.[/FONT]
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Mwalimu Juma ameshaachana na wasichana wawili ambao wote alipoanza urafiki nao walimtegemea kwa kila kitu kifedha na alipotamka kuoana kila mmoja kwa wakati wake walimruka na kumkimbia.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Jane na mwalimu Juma si wao tu katika kujikuta wanaangukia kwa wapenzi wanaowaumiza mara zote inawezekana hata wewe unayesoma hapa yamekukuta, umejikuta upon Kwenye replay ya kosa lilelile kwa mpenzi wa zamani na sasa lipo kwa mpenzi mpya.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Watafiti wa masuala ya mahusiano wanakiri kwamba namna tumelelewa na familia ambazo zinatulea tangu watoto zina effect kubwa sana katika maisha yetu na namna tunaweza kumtafuta mwenzi wa maisha.[/FONT]​
  [FONT= ]Kuna namna ya asili (natural Instinct) ambayo hutueleza namna ya kutafuta usalama wa kudumu kimaisha na hizi natural instinct hufanya tofauti na ufahamu wetu wa ndani hasa katika suala la mahusiano kwa kutofahamu tunatafuta kutimiza hisia zetu (emotions & feelings) kwa yale tuliona wakati tunalelewa.[/FONT]​
  [FONT= ]Matokeo yake kama ulizaliwa familia ambayo baba na mama walikuwa wanagombana unaweza kuishia kumpata mpenzi mgomvi ambaye atakuwa anakudunda kila siku.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Je, unatakiwa kufanya nini kama unajikuta ni mtu wa kurudia kosa lilelile?[/FONT]
  [FONT= ]Jambo la msingi ni kufananisha sifa za mpenzi wako wa kwanza aliyekuumiza na huyu unataka kuwa naye na tafuta tofauti zake pia na orodhesha vitu ambavyo hupendi vijirudie.[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Kama wewe ni Jane (Kwenye mfano) kwa nini kutafuta mwanaume kwa sababu ni smart au ana mafanikio badala ya mwanaume mwenye sifa tofauti na hizo?[/FONT]​
  [FONT= ]Kwa nini kama wewe ni kama mwalimu Juma (Kwenye mfano hapo juu) utumie fedha kama njia ya kumvuta mwanamke akupende badala ya upendo tu bila kuonesha fedha zako au uwezo ulionao?[/FONT]​
  [FONT= ][/FONT]​
  [FONT= ]Kufanya jambo lilelile kwa njia ile ile si rahisi kupata matokeo tofauti.[/FONT]
  [FONT= ]Tumia ubongo[/FONT]
  [FONT= ][/FONT]
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  BY MBILINYI.BLOGSPOT.COM

  Hivi ni Mara Ngapi?  [​IMG]
  SWALI:
  Samahani sana kwa swali langu, ila kwa kweli napenda kufahamu hivi ni mara ngapi wanandoa wanatakiwa kuwa na tendo la ndoa (sex) kwa wiki au mwezi ?
  Kwani kila mtu ninayemuuliza ananipa jibu lake na kidogo inanichanganya, na wakati huohuo mume wangu kuna siku anakuwa mkali na mchungu hata kama sijakosea kitu chochote.
  Msaada wako kaka Mbilinyi!
  ____________________________
  MAJIBU:
  Dada asante sana kwa swali zuri ambalo linawakilisha wanawake na wanaume wengi katika ndoa hasa wale ambao hufika mahali wakajikuta hawaridhiki na mwenendo mzima wa suala la sex katika ndoa zao.
  Naamini umeuliza hili swali kwa sababu ni swali muhimu linalohusu ndoa yako.
  Kumbuka jambo la msingi katika swali lako (bottom line) ni kwamba kawaida (mara ngapi sex iwe kwa siku, wiki au mwezi) ni suala la wewe na mume wako kuzungumza, kuelewana na kukubaliana au wewe mwenye binafsi kufika mahali ukafahamu kwamba mume wako na wewe kila mmoja ana hamu ya kimapenzi kiasi gani kwa siku au wiki au mwezi kwa maana kwamba kumfahamu mwenzako uhitaji wake na kila ndoa duniani ipo tofauti kwa maana kwamba wengine hufanya sex kila siku, wengine kwa wiki mara 1 au 2 au 3 na wengine kwa mwezi mara 1 au 20 na wengine hata wakifanya sex kwa mwaka mara 1 wanaona sawa tu.
  Unanikumbusha mama mmoja aliyelalamika kwamba mume wake anamtaka sex mara 10 hadi 15 kwa siku iwe mchana au usiku hadi akaomba kujirudi nyumbani kwao kwa wazazi kwani amechoka na mwanaume wa aina hiyo, tuache hayo!
  Kujihusisha na sex mara kwa mara kwa wanandoa hutokana na afya, emotions, kubadilika kwa maisha, stress, depressions, migogoro, kufiwa na kazi na uchumi hata watoto nk na kiwango cha kuhitaji sex hakiwezi kuwa sawa au juu maisha yote kwani kuna uhusiano mkubwa sana kati ya sex na akili.
  Kama mume wako ni mkali (grouchy/irritable) inawezekana hormones zake za testosterones zimepanda sana zinahitaji release na njia muafaka kwake ni wewe kuwa available (kumpa sex).
  Inawezekana huko kazini boss anamkalia sana mume wako kiasi kwamba akirudi nyumbani anahitaji mwanamke ambaye anaweza kumfariji na kumpa caring na attention kubwa kwake.
  Ndoa ni kufanya kila kitu pamoja, kuelewana, kuzungumza na kuwasha moto wa kimapenzi ili kila mmoja aridhishwe kimapenzi na wewe ni mwanamke ambaye ni halisi kwa ajili yake.
  Hivyo unahitaji kuwa mwangalifu kusoma namna upepo unavuma hapo nyumbwani, ukiona ana dalili kwamba anakuhitaji kimapenzi unahitaji kuwa available bila kujali mnafanya sex mara ngapi kwa wiki, kwani suala la msingi si mara ngapi kwa siku au wiki bali kunaridhika au kuridhishwa kiasi gani na mume au mke wako.
  Wewe ni mwanamke na una advantage kubwa kwani ni rahisi sana kumsoma mume wako na pia hata kama alikuwa hataki sex na wewe unahitaji bado ni rahisi sana kuwasha umeme (kumfanya awe stimulated) na kuhakikisha Mr. happy wake anashawishika kukubali ombi lako kwani kwa urembo wako na uzuri wako hakuna kisichowezekana.
  You are a woman beautifully and masterfully created.
  Siku njema
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Waoo!Ukweli wa ukweli huo,akinadada mlio kwenye uhusiano zingatieni hayo,mtayafanya mahusiani/ndoa kuwa na amani
   
 4. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante pdidy,
  MWENYE MASIKIO NA ASIKIE NA MWENYE MACHO NA AONE.........
   
 5. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  uko sahihi kaka, maisha yangu binafsi yameguswa na maneno yako, na hivi sasa niko ktk mchakato wa kutafuta mwenza , kimsingi nimejua kosa langu ninini, NAKUSHUKURU SANA UMENISAIDIA.[​IMG]
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Duh ni kitini cha ukweli sana.
  Natamani ningekuwa nimeoa ghafla hahahahaha lol
   
Loading...