Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi - Ikulu ya Marekani yaandaa sherehe nzito!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Wiki hii kote ulimwenguni Wakristo watasherehekea Pasaka. Pasaka ni sikukuu kubwa kwa Wakristo kwa sababu ni siku ya kuadhimisha tukio muhimu sana katika imani ya Kikristo — kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu. Bila Pasaka, hakuna Ukristo. Ndiyo sababu Wakristo huiona Pasaka kuwa ni siku kuu ya kipekee kuliko Krismasi.

Nchini Marekani, wiki hii inatambulika kuwa ni Wiki Takatifu(Holy Week). Mwaka jana Rais Mstaafu, Joe Biden aliiadhimisha wiki ya Pasaka kwa kutoa tangazo la kuwatambua watu waliobadili jinsia!! Rais Trump amepindua uchafu huo na kuipa heshima wiki hii kwa kuandaa matukio makubwa ya kuadhimisha Pasaka.

Wiki hii, Jumatano jioni, wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani watakuwa na "Dinner" nzito ya Pasaka. Alhamisi itakuwa siku ya maombi na kumwabudu Mungu kwa wafanyakazi wote wa Ikulu ya Marekani. Siku hiyo wafanyakazi hao watapata pia nafasi ya kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa Wahubiri mbalimbali.

Jumapili iliyopita, Rais Trump aliahidi kuilinda imani ya Kikristo mashuleni, katika Jeshi na katika maeneo yote ya kazi. Alisisitiza pia kwamba ataendelea kulinda uhuru wa kuabudu katika nchi hiyo.

Rais Trump haoni aibu kumtangaza Yesu na yuko tayari kuujulisha ulimwengu wote kuhusu imani yake.

Baada ya kuanza muhula wake wa pili, Rais Trump alianzisha "White House Faith Office" kupitia agizo la kiutendaji tarehe 7 Februari 2025, akiwa na lengo la kuyasaidia mashirika ya kidini na ya kijamii katika juhudi za kuimarisha familia za Marekani na kulinda uhuru wa kidini. Ofisi hii ndiyo inayoandaa sherehe kubwa za Pasaka, Ikulu ya Marekani, mwaka huu.

Wewe je, umeandaa nini kusherehekea Pasaka? Karibu nyumbani kwetu ule vinono!

Grace and peace to you this Easter season. God bless you abundantly.
 
Ngoja nikufafanulie vizuri, kwanini Pasaka ni sikukuu kubwa(muhimu) kuliko Krismasi. Pasaka ndiyo kiini cha Injili na msingi wa tumaini la wokovu kwa Wakristo. Pasaka ni siku ambayo Yesu alishinda kifo na dhambi. Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu, lakini hakubaki kaburini — alifufuka siku ya tatu. Hii inaonyesha kuwa kifo na dhambi havina mamlaka tena juu ya wale waliomo ndani ya Kristo (Warumi 6:9-10).

Kufufuka kwa Yesu kunatuhakikishia tumaini la uzima wa milele. Kama Yesu asingefufuka, Wakristo wasingekuwa na uhakika kwamba watapata uzima wa milele (1 Wakorintho 15:17-20).
 
Yesu asingefufuka, kifo chake msalabani kingekuwa tukio la huzuni tu. Lakini sasa Pasaka inaifanya Injili kuwa habari njema ya kweli.

Wakristo huamini kwamba kwa kufufuka kwa Kristo, wao pia wamefufuliwa kiroho kutoka katika kifo cha dhambi. Pasaka ni ukumbusho wa kuzaliwa upya, na mwanzo wa maisha mapya katika Kristo (Warumi 6:4).

Nakutakia heri ya Pasaka na baraka za Mungu ziwe juu yako!
 
Marekani pasaka wala sio public holiday, kazi kama kawa! Hiyo sherehe nzito umeionea online? Au umehadithiwa?
 
Marekani Krismasi ni kubwa kuliko Pasaka.
My friend Nyani Ngabu soma title kwa utulivu.
Ngoja nikufafanulie: Sijasema Pasaka ni sikukuu kubwa Marekani. Nimesema Pasaka ni sikukuu kubwa kuliko Krismasi, na Ikulu ya Marekani wameandaa sherehe nzito(kuadhimisha siku hiyo).

Nimefafanua kwanini Pasaka ni sikukuu kubwa katika Post #2.
Nadhani wewe unaangalia idadi ya watu wanaoisherehekea Krismas ukilinganisha na wanaosherehekea Pasaka.
 
Ukiwa uko Marekani msimu wa Krismasi huwezi kuuepuka.

Pasaka kama wewe si muumini yaweza kuja na kupita bila hata kujua!
Rais Trump ameliona hilo. Ndio sababu anataka kurudisha hadhi na heshima ya Pasaka. I presume hiyo Easter dinner TV zote kubwa wataonyesha.
 
Utakuta mtoa mada hata boda hajawahi vuka, akienda mbali sana jua yupo TUNDUMA
Wewe nguvu yako ni majivuno?

Mimi sina tabia ya kupiga tarumbeta nikivuka boda. Majivuno niliyatupa shimoni baada ya kuokoka.

Methali 16:18
"Kiburi hutangulia maanguko, na roho ya kujivuna hutangulia kushushwa."

Luka 18:14
"Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa; naye ajishushaye atakwezwa."
 
Gal 3:1
 
Wiki hii kote ulimwenguni Wakristo watasherehekea Pasaka. Pasaka ni sikukuu kubwa kwa Wakristo kwa sababu ni siku ya kuadhimisha tukio muhimu sana katika imani ya Kikristo — kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu. Bila Pasaka, hakuna Ukristo. Ndiyo sababu Wakristo huiona Pasaka kuwa ni siku kuu ya kipekee kuliko Krismasi.

Nchini Marekani, wiki hii inatambulika kuwa ni Wiki Takatifu(Holy Week). Mwaka jana Rais Mstaafu, Joe Biden aliiadhimisha wiki ya Pasaka kwa kutoa tangazo la kuwatambua watu waliobadili jinsia!! Rais Trump amepindua uchafu huo na kuipa heshima wiki hii kwa kuandaa matukio makubwa ya kuadhimisha Pasaka.

Wiki hii, Jumatano jioni, wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani watakuwa na "Dinner" nzito ya Pasaka. Alhamisi itakuwa siku ya maombi na kumwabudu Mungu kwa wafanyakazi wote wa Ikulu ya Marekani. Siku hiyo wafanyakazi hao watapata pia nafasi ya kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa Wahubiri mbalimbali.

Jumapili iliyopita, Rais Trump aliahidi kuilinda imani ya Kikristo mashuleni, katika Jeshi na katika maeneo yote ya kazi. Alisisitiza pia kwamba ataendelea kulinda uhuru wa kuabudu katika nchi hiyo.

Rais Trump haoni aibu kumtangaza Yesu na yuko tayari kuujulisha ulimwengu wote kuhusu imani yake.

Baada ya kuanza muhula wake wa pili, Rais Trump alianzisha "White House Faith Office" kupitia agizo la kiutendaji tarehe 7 Februari 2025, akiwa na lengo la kuyasaidia mashirika ya kidini na ya kijamii katika juhudi za kuimarisha familia za Marekani na kulinda uhuru wa kidini. Ofisi hii ndiyo inayoandaa sherehe kubwa za Pasaka, Ikulu ya Marekani, mwaka huu.

Wewe je, umeandaa nini kusherehekea Pasaka? Karibu nyumbani kwetu ule vinono!

Grace and peace to you this Easter season. God bless you abundantly.
Huo ni mtazamo wao, haukulazimishi nawe kuiona kuwa sikukuu kubwa
 
Back
Top Bottom