Part VIII: uko wapi rafiki? kuna cha kujifunza hapa!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Dada ako aliingilia mazungumzo kati yangu na mbaya wangu. Alitaka kujua naelekea wapi. Nikamjibu mwenge. akaniomba tuzungumze kwa dakika chache, kabla hatujaachana, kwa sababu anataka kwenda Ubungo kufuatilia vile vitu vyako - mdogo wake, manusra wangu wa ajali. Aliitumia fursa hiyo vizuri na kuniuliza mambo mengi sana. Aliniuliza kuhusu wazazi wangu, aliniuliza kuhusu ninapoishi, naishije? Na kina nani?, aliniuliza kuhusu shule, aliniuliza kuhusu kibarua ninachofanya, nikamwambia mimi ni form 6 leaver, nimeji-tune kuwa mjasariamali kwa kufundisha tuition, Mwenge DSM.

Akaniuliza kuhusu mahusiano, akaniuliza kuhusu wewe, manusra wangu wa ajali! leo tuanzie hapa:
Tumeumbwa tofauti sisi binadamu. Mimi ni miongoni mwa watu ambao, si rahisi kujiachia. Si rahisi kufunguka. Na hasa kama mtu anaetaka nifunguke kwake ni wa jinsia tofauti na ya kwangu, mtoto wa kike. Huwa ni mgumu kufunguka mbele ya wasichana. Hili lilinikuta kwa dada ako pia. Sikukubali kufunguka. Dada ako alitumia uwezo wake wa akili kunishawishi, nadhani alishindwa. Sikufunguka. Nitafungukaje kwa mtu ambae sijajua ana agenda gani na mimi?
Sikujua athari za mimi kufunguka kwa dada wa manusra wangu wa ajali. Kama nitafunguka kuhusu mahusiano, taarifa hizo zitatumikaje? Zitatumika kwa nani? Kama kwa dada mtu ama kwa mdogo mtu, hilo sikuwa na uhakika nalo! Manusra wangu nae, atapokeaje taarifa za mimi kufunguka kwa dada ake, endapo dada mtu ataweka mambo hadharani! Niligoma kufunguka.

Kwa mbali nilishuhudia kila memba wa kile kikundi chetu akidandia gari lake. Yupo aliepanda la Muhimbili – Mabibo. Kuna aliepanda dala dala ya Temeke. Yupo aliepanda gari za Mwenge kupitia Shekilango. Huyu nilishindwa kujua kwa nini hakuambatana na dadako. Kwa kifupi kila mmoja wa watu wako aliondoka na safari yake. Tukabaki sisi. Mimi na dada ako. Sikumbuki ni wakati gani niliskia watu wale, kila mmoja kwa nafasi yake, akiagana na dada ako, kwa kweli sikumbuki. Nilichoona ni wale watu kila mmoja akipanda dala dala lake.

Kwa karibu kabisa, pamoja na makelele ya kondakta, nikaona dala dala lenye maandishi Mwenge-Muhimbili. Nikatumbua macho kuashiria kuwa nina hisia na dala dala lile. Nikiamini hili ni basi sahihi, tena kwa muda sahihi na mimi kujongea kuelekea kibaruani kwangu. Kama mfano wa mtu alieibuka ghafla kutoka kina cha maji, nikajikuta namuaga dadako, nikajikuta namuambia dadako, kumtakia kazi njema, na kwamba tutaonana jioni. Aaaah waapi, dada ako akanshika mkono, akanivuta, akanivuta na safari hii nguvu yake ya kunivuta ilikuwa imeambatana na maneno.

"Kama unaenda Mwenge, basi na mimi naenda huko huko, kama unawahi kibaruani kwako, ni tayari tushachelewa, basi tutachelewa sote!" Mpaka kufikia hapo sikujua ni kipi kimetokea. Nikajikuta mwili wangu na hususani miguu inatii nguvu ya kuvutwa mkono, na dada ako pasi na kuishirikisha akili. Tena maajabu ya mungu, si kwamba alikuwa ananivuta kweli, ni kama alinishika na kunionyesha uelekeo. Kama kumvusha mtoto wa shule bara bara. Huitaji nguvu hapo.

Ni kama vile upewe kazi ya kusukuma gari ambalo tayari lipo ktk spidi 30. Ni mara chache sana nimeshuhudia mwili wa kiumbe mwanadamu ukitimiza wajibu wake pasi na akili kutumika. Hapa sikutumia akili, labda sikuitumia ipasavyo. Miguu yangu ilitii kufanya anachotaka dada, huku akili ikiwa Mwenge, kibaruani kwangu.

Kati kati kulikuwa na purukushani ya kukwepa msururu wa watu wanaoenda na kurudi Muhimbili, wale waliokuwa wanapita pembeni ya maduka ya dawa pale karibu na ule mzunguko wa Muhimbili. Wengine walikuwa wagonjwa maskini, wengine wasindikizaji wa wagonjwa. Kulikuwa na pilika pilika nyingi sana asubuhi ile.

Tuliwapita watu wale huku nimeshikwa mkono. Wapo walioshangaa kwa nini nimeshikwa mkono ingali sina dalili yoyote ya kuumwa, na wala sikuwa mpotea njia, wala sina dalili ya kuwa ni mtu nilietolewa wodini, punde baada ya kulazwa kwa masiku.

Nilikosea. Si kweli. Kumbe wale watu walikuwa hawashangai mimi kushikwa mkono. Hakuna cha ajabu hapo. Walikuwa wanashangaa aina ya kiumbe ambae amenishika mimi mkono. Alienishika mkono ndiye anaeshangaza wapita njia wale. Kwa kawaida, mimi ni miongoni mwa watu ambao ukiwauliza nini maana ya urembo wa mtoto wa kike ama yu aje binti ama msichana mrembo, huwa sina majibu ya moja kwa moja.
Kwangu mimi, binti ama msichana mrembo, awe mweupe, awe mrefu, basi, awe anavaa, kuna tofauti kati ya kuvaa na kujisitiri. Nishatosheka! Vingine vyote ni mbembwe. Dada yako alikuwa na vya zaidi ya hivi nivipendavyo mimi.

Yeye, hata akinuna, bado anatabasamu, kati kati ya meno yake mawili ya mbele, kumeachwa nafasi! Acheke asicheke, kuna vishimo juu ya mashavu yake. Rafiki yangu, dada yako ni mrembo. Sikumbuki katika maisha yangu kama nishawahi kushikwa mkono na kiumbe cha jinsia ya kike, tena anaeweza kusababisha mshangao kwa makumi ya wapita njia barabarani, kwa uzuri wake ambao, nahitaji wiki moja nyingine kumuelezea hapa. Si tu walishangaa, bali pia wapo waliotamani fursa ile waipate wao. Ndio. Waliniona sielekei kuwa na nasaba na Yule bidada, kama ni uhusiano wa kimapenzi basi hata kwa macho ya kipofu ilionyesha wazi wazi kuwa Yule mrembo si mpenzi wangu.

Kwa wanaojua kukadiria, wangeweza kubet kuwa mrembo amepotea njia, na hapo amemuokota mtu, tena asie na muelekeo, wa kumuelekeza njia sahihi. Yalijiri mengi pale njiani, ila ninachokumbuka ni kuwa fahamu zilinirudia baada ya kumsikia dada ako anaagiza chapati moja na mtori.

Ni yeye ndiye alieniuliza "…… wewe unaagiza nini?" Kumbuka hili ni swali ambalo linakuja kichwani mwangu huku nikiwa tayari na burungutu la fikra, nilikuwa nawaza kinachofuata baada ya offer ile! Niliwaza kibarua changu Mwenge! nikaendelea kuwaza, ndani huko nimelazimishwa kurudi mchana, sijakataa wala sijakubali, sasa hapa napo nakalishwa mgahawani, naambiwa niagize kifungua kinywa! Nikawaza, dada alishasema tutachelewa sote kibaruani, kwa nini tuchelewe? Niliwaza sana.

Muda wote wa mawazo haya, nilikuwa nawaangalia watazamaji wanaotuangalia, wale wanaoshindwa kuamini akili yao kuwa Yule mrembo yupo na mtu wa sampuli yangu, kwao ni kama haiwezekani, na kulikuwa na kundi la pili, hili lilikuwa linaonyesha wazi wazi jinsi walivokuwa wananionea wivu mimi kuwa pale na bidada Yule, ambae kwa mara nyingine tena, muumba kaonyesha uwezo wake kwa product hii, kama ni ingizo jipya basi hili limepitiliza!

Kwa wewe ambae hukubahatika kumuona kiumbe huyu, na kwa ninavojua kizazi chenu ni kizazi cha kidadisi, kwako kumuona kiumbe nilie nae hapa ilikuwa ni ushaidi na observation tosha kuwa baba Mungu ametoa trial version ya toleo jipya la wanadamu wa jinsia –ke!

Kanuni yangu ya kuficha madhaifu yangu panapo watu wa jinsia kinyume na yangu, nikaikumbuka, nikajitutumua, nikaagiza supu tu na chapati mbili. "Eeeenhe bwana ……, pole kwanza kwa heka heka zote hizi. Samahani, kuna vitu naomba kuviskia kutoka kwako, kwa nini Elizabeth alikuita? Alikuwa anataka nini kutoka kwako? Na ilikuwaje ukakaa sana? Naomba unambie, nini kilikuwa kinaendelea pale wodini baada ya kuitwa na Elizabeth?"

Sikuwa huru. Kichwani tayari nilikuwa na mzigo wangu, na huyu nae alikuwa ananitwisha mzigo mwingine. Nilichoka. Ilikuwa lazima nichoke, ni kama kufanya mtihani wa supplementary ambao maumivu yake kabla hata ya matokeo ni sawa na kusema "refa wao, uwanja wao, na mpira wa kwao! Nimeumia," nilitafuta mchawi wangu, nisimpate. Labda ile ajali. Labda jioni ya siku ya tukio ningetulia Buguruni nyumbani yasingenikuta ya kunikuta kama haya, yasingenifika haya yanayonifika hapa. Aaaaah, nilikosea kujiunga na shule ya bweni ya wavulana kwa masomo ya juu ya sekondari, niliwaza. Labda muonekanao wangu. Mtanashati, asilimia kubwa ya kipato changu kilienda ktk mavazi. Labda huruma yangu, labda kihere here.

Kwa kifupi nilikuwa mtu mwenye msongo wa mawazo, wewe ungeniona ungejua dhahiri shahiri, mtu huyu hayupo duniani wala ahera. Mbili haikai, tatu haikai, tano ilishakatika kabla hata game haijaanza. Kilichofuata ilikuwa ni kutoa maelezo ambayo kama ungekuwa karibu wala usingepata tabu kung'amua kuwa msimuliaji anasimulia story iliyohaririwa, tena kwa kukurupuka. Sikuweza kusema ukweli, kuwa nimealikwa kurudi wodini pale mchana, tena pasi na sababu ya kurudi iliyo wazi.

Yale maswali yakajirudia. Safari hii kwa utulivu wa hali ya juu sana, utulivu unaomuaminisha msikilizaji kuwa muualiza maswali ana kitu moyoni. Hukijui tu. Aliniuliza kuhusu wazazi wangu, aliniuliza kuhusu ninapoishi, naishije? Na kina nani?, aliniuliza kuhusu shule, aliniuliza kuhusu kibarua, aliniuliza kuhusu mahusiano.

Rafiki yangu, hatimaye niliamini ndani ya nafsi yangu kuwa ile hatari niliokuwa naiogopa mbele ya wanausalama wale wa jana, ilikuwa ni moja ya hatari ndogo sana kuliko hatari ninayoikaribia hapa. Naiona hatari inanijia. Niliamini hii ni hatari. Wenyewe mna msemo wenu - usione vyaele ......! Ana mwenyewe huyu. Binti mrembo. Binti mrembo tena si wa umri wangu, si wa kariba yangu! Na ndio maana nawashangaza wapiti njia! Mrembo na Form six leaver wapi na wapi? Si tu mrembo, ni mrembo na ajira yake? Wazazi, kazi, mahusiano! Kwa nini anasisitiza kujua vitu hivi vitatu kutoka kwangu? Kama sikaribii hatari nakaribia nini hapa?

Mapenzi. Ndio vijana wengi tunapenda vitu vizuri. Lakini basi huwa tunaangalia na vitu vizuri vyenyewe. Ni kama vile bidada ananilazimisha kufanya mtihani usio wa level yangu. Binadamu tumeumbwa na mitihani kweli, ila hii mingine mbona kama uonevu. Sikufunguka. Akanielezea kuhusu familia yenu. Akanieleza kuwa yeye ndiye amekuwa muangalizi wako mkuu kwa hapa DSM. Na kwamba mama yupo mkoani. Pia, mama ameskia kuhusu hili tukio, anajiandaa kuja kumuona binti yake. Eti, mama ana hamu ya kumuona msamariamwema aliemuokoa binti yake kutoka ktk hatari ya kifo. Akaongea mambo mengi sana.

Ndani ya mtima wangu, sikuwa na hamu ya kumuona mama wala baba yako. Yalionikuta baada ya kukusaidia kutoka ktk ajali ile yanantosha. Sitaki tena kukutanishwa na mtu wa nasaba na wewe. Tayari kichwa kinaniuma. Manusra wangu wa ajali, kanipa kazi ya kufikiria kichwa changu. Dada ako nae, niko nae hapa anafanya yake. Kichwa bado hakijapoa naambiwa mama ameskia kuhusu tukio na anataka kumuona, uso kwa uso huyo msamariamwema wa bintiye. Nimechoka.

Na mimi kama mwanga aliepotea njia vile, hawezi kwenda wala kurudi, muda wote nilikuwa namsubiria dada ako agusie suala zima la mahusiano kwa upande wake. Nilitaka aseme kitu, afunguke. Kama angesubiri nimfungukie angesubiri sana, akili yangu haikuwa huko. Nilitaka, aseme kama ameolewa ama laaah? Aseme kama ameshajibinafsisha ama!

Mungu wangu. Dada ako akabadili mtindo wa ukaaji pale mgahawani. Mwanzo tulikaa kama vile watu wakaavyo katika siti ya dala dala, ile siti ya watu wawili, lakini sasa amekaa tunatazamana. Nikaona ile min skirt ya gold ikipanda juu. Wakati akikaa huku akiilazimisha kuishusha chini, ni kama vile alitaka nijue anajisitiri na maungo yake ya chini, ana heshima, japo ukweli wa moyoni mwake alikuwa anasema "weeee nae…….., si uangalia huku basi, lugha ngumu sawa, basi hata picha huoni!

Namna tulivokaa na dada sasa hivi, ilikuwa haina kificho kwamba mada inayofuata ni nzito, mada muhimu na ni nyeti kuliko mada zote tulizokwisha zungumza mimi na yeye, tangu tufahamiane.

Nitakuwa nanyi tena Alhamisi, panapo majaaliwa!

Munkari, Foundation, dawa yenu, Blessed
naomba mnisaidie kuwaita heart, likud, kijana leo, vaislay, lin, mwekundu, g click, ikhwaan, tutsi gal, prospa, mokoyo, masonda, ram, watu8 na the boss! beb v

Last edited by a moderator:
vipi slim walikuteka ukatuacha kwenye mataa nijibu ndo nianze kusoma story
 
slim5 mbona keyboard yako leo inaandika kwa madoido hivi...

Kuza kuza kidogo hii font
 
Last edited by a moderator:
hahahaha slim kaniudhi anataka kutegeka kwa dada mtu tena mi nampenda ampindue mpenzi wa eliza bhana hahaha haya jisevie hapo lol
slim5 ni mwindaji hodari, hana papara wala haraka...

Hakynani mwisho wa siku atakula tetere na mayai yake teh teh teh!!!

Chezeya kutazama hazina zilizo ndani ya kimini sketi cha gold???
 
mi nimekuja mwenyewe maana nilikuwa nasubiri huu mlolongo., daa alhamis tunakusubiri mkuu maana kama nakuona vileeeeeeeee
 
Mkuu hiyo font hebu kuza kidogo,au bado uko kwenye mauzauza moja haikai tano ishachomoka kitambo!?
 
naomba mnisaidie kuwaita heart, likud, kijana leo, vaislay, lin, mwekundu, g click, ikhwaan, tutsi gal, prospa, mokoyo, masonda, ram, watu8 na the boss!
[aah mbona hiki ni ktabu sasa]
 
Mmmmmh slim5
Usinambie ulijisevia Dada MTU hahaha bwana alhamis mbali Fanya Fanya hata kaj5 bas!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mmmmmh slim5
Usinambie ulijisevia Dada MTU hahaha bwana alhamis mbali Fanya Fanya hata kaj5 bas!!!!!

aaaah! aaaah!aaaah!aaaah!aaaah!poa poa, kuna vimajumkumu hp ofisini vinantinga this wk, nikiweza J5 ntaruka hewani Munkari!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom