Part-7: TISS Bado safari ngumu

Part-7: TISS Bado safari ngumu

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Mada hii imejikita ktk kushauri kizalendo nini kifanyike ili kuliokoa taifa lisizidi kutopea kwenye umasikini wa kutupwa unaolikabili taifa kwa sasa.

Idara ya usalama ina wataalamu wa nyanja zote wenye uwezo mkubwa kiakili pia, baadhi yao ni ma genius.
Idara hii iache kutumika kisiasa, bali itumike kulinda maslahi ya watanzania wote wenye vyama tofauti na dini tofauti.
Wanasiasa wakianza kuitumia Idara ya usalama kwa maslahi yao ya kisiasa na siyo nchi hatima yake huwa ni mbaya sana.

Kwa hiyo ni bora idara ikacheza mazingaombwe kuhakikisha nchi inakuwa na katiba nzuri kwa ajili ya watu wote na vizazi vyote vijavyo na siyo kulilinda genge la watu wachache kwa faida yao.

Hayati Baba wa taifa, Mwl Nyerere aliwahi kuonya endapo chama tawala kitaingiliwa na matajiri basi huo ndo ilikuwa mwisho wake ,watu wenye pesa walikimbilia chama tawala ili kulinda maslahi yao, siyo kwa sababu wanaipenda CCM, la hasha, bali kwa sababu wakienda upinzani biashara zao zipo hatarini.

Idara imeacha taifa liwe la watu wanaoimba mchana na usiku kusifia chama tawala na viongozi wake badala ya kuimba uzalendo juu ya nchi yao.

Wakenya waliokuwa wakiimba kusifia KANU badala ya Kenya zaidi ya miaka 32,leo KANU iko wapi? Lakini Kenya yao ipo.

Hata CCM inayotawala leo itapotea na kutoweka, na hata CHADEMA ikitawala nayo itakuja kupotea na kutoweka, Lakini Tanzania inadumu milele yote.

Idara ina watu wenye weledi mkubwa wanaojua jinsi ya kuifanya Tanzania isiwe ya makundi ya watu vichaa wanaoshinda mitandaoni kutukana na kukejeli kila anayekosoa Serikali bali wawe watu wamoja wenye uzalendo uliotukuka juu ya taifa lao.

Bado naendelea kuamini kuwa TISS ina uwezo wa kufanya kazi Kama MOSSAD au CIA ikitaka.

Kipi kinashindikana? ni TISS hii hii iliweza kuzuia hujuma kibao za Serikali ya kibaguzi ya makaburu dhidi ya Tanzania.
Ni TISS hii hii, iliendesha operesheni za ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa.

Basi na sasa isimame juu ya ustawi bora wa Tanzania, maana kuna chuki kubwa mno za kisiasa miongoni mwetu.
Kuna mtu mmoja akaniuliza, "ulitaka TISS wajenge viwanda ?".

Lilikuwa swali zuri mno japo la kimbumbumbu.

Nilikaa kimya na sasa najibu hapa.

Tulikuwa na viwanda takribani 400,na moja ya viwanda hivyo kilikuwepo cha kusindika nyama ya ng'ombe, cha viatu, nguo, matairi na n.k.

65% ya viwanda vilivyokufa Tanzania vilikuja kufufukia Kenya, tafsiri yake ni kwamba, Usalama wa Taifa wa Kenya, KNIA walifanya yao huku TISS yetu ikiwa imelala, na Kiwanda cha mwisho kuhamia Kenya ni cha General Tyres, yaani ajira zinakufa Tanzania kisha zinawafufukia Wakenya.

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania, nashukuru Mungu tena dakika za mwisho TISS walistukia mchezo vinginevyo VodaCom nayo ilikuwa inakufa na ingekuja kufufukia Kenya

Inaendelea

Mnahangaika sana na TISS wenu hawa, huwa nasema wakwetu wanafanya kazi kama polisi, wanajua mambo yakiishatokea sio kabla. Sasa wakikurupushwa utasikia tulikuwa na taarifa.

Nakumbuka ubalozi wa marekani huwa wanawataarifu raia wake waliopo nchini kupitia website ya ubalozi wao kuhusu hali ya usalama wakiwa nchini mwetu.

Apo utamsikia waziri eti waje wajieleze, badala kuwashukuru na kutafuta namna ya ku share taarifa nao ili mchanganye na matope yetu, mna taka kushindana.

Anyway endeleeni na mjadala huwa sisomi mijadala ya kiusalama.
 
!
!
Zamani Na Mimi Nilikuwa Naamini Hivyo Kwamba Jamaa Wana Uwezo Na Upeo Mkubwa Sana. Baadae Nikaja Kuambiwa Kuna Nafasi Fulani Fulani Huwezi Pata Kama Wewe Sio Mtu Wa Kitengo.

Nikimwangalia Dingilai, Bashite, Happy Mro Gwambo Jafu Na Wengine Kama Hao Nadhani Nadharia Ya Kuwa Na Upeo Na Uwezo Mkubwa Tuiondoe. Angalau Kwa Sasa.
 
Mkuu leo nikupongeze umeshuka nondo nzuri sana za kizalendo. Mchango wangu TISS mjue kabisa hapa watu wanachangia kwa nia nzuri tu ya kuboresha nchi yetu, sasa basi viongozi wote wa ngazi zote ambao hawana sifa, weledi, busara, hekima muwatoe ili kulinda heshima ya taifa hili. Pili viongozi wote wa ngazi zote wenye utata wa uraia wao mfanye hivyo hivyo.

Tatu viongozi wote wa ngazi zote wenye matatizo ya afya ya akili muwatoe njia mnazijua. Nne mhakikishe kuwa maliasili zote za nchi zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote sio kikundi cha watu wachache wa CCM.

Tano mhakikishe kuwa mali za umma ziko salama, sio viongozi wasio waadilifu wanafanya embezzlement of public funds, tumieni njia za kijasusi kuzuia haya hata kama ni indirect mnatibua dili. Sita hakikisheni maisha ya watanzania wote yako salama pamoja na tofauti zao za kisiasa, uonevu usiwepo haki itendeke kwa raia wote, kama kuna kiongozi hatendi haki huyo hafai mnajua cha kufanya.

Saba hakikisheni pesa na mali zote za watanzania zilizoibwa na viongozi wakubwa zinarudi kwa wananchi. Nane ili Nchi ipate maendeleo hakikisheni nchi inapata viongozi waliochaguliwa kihalali na Wananchi, yaani mhakikishe waliochaguliwa kwenye uchaguzi halali ndio wanapata madaraka. Kwa sasa hayo tu baadaye nitaongeza.
 
Hawa hawa wanaoacha watu wanatia kokoto kwenye magunia ya Korosho
au tunawazungumzia wengine? Halafu mfanyabiashara utegemee arudi tena Tanzania?
Haya sasa wamerudi wahindi peke yao kwenye Mnada wa Korosho na mpaka leo hajajulikana
aliyetia Tani kadhaa za kokoto kwenye gunia za korosho, Bandarini hakuna USALAMA?
 
una TISS imara, una mahakama dhaifu, una bunge dhaifu, una ofisi ya CAG dhaifu, una PCCB dhaifu, una polisi wenye akili za kikoloni, una wanahabari makanjanja, una mahakama dhaifu, una chama tawala cha kikomunisti kinachoweka maslshi ya chama mbele kuliko hata ya nchi, kisha juu ya yote hayo una rais mungu mtu anayejifanya mjuvi wa kilakitu!
sahau maendeleo, uimara wa taifa unatokana na taasisi zake pamoja na mfumo mzuri wa kuwajibishana! mzee mkapa ndio rais pekee wa enzi hizi aliyeamini katika taasisi imara.
 
Tatizo tiss wenyewe ni ccm, ndio maana wanagombea vyeo kupitia ccm, sasa unategemea nini hapo, zaidi ya kuilinda ccm, matokeo yake wanazidi kuibomoa nchi, maana ccm kimekuwa kichaka cha wezi wanaoiibia serikali,

tiss wamejazana katika kila idara za serikali na wao ndio wakuu maboss huko, lakini cha kushangaa huko kuna wizi wa kutupa,
Inasikitisha kitendo ambacho ndicho ilitakiwa kiwe chachu ya maendeleo ya nchi, chenyewe ndio kimekuwa chachu ya kudolola kwa nchi katika nyanja zote, ndio mashitaka ya umma yote yamefirisika, na uchumi pamoja na democracy imedolola.
 
Jamani nchi hii inevurugwa kabisa! Hata hao TISS wamevurugwa kabisa na kupoteza mwelekeo siku nyingi!

Angalia wanavyohangaika kushiriki katika vikao vya kutafuta ushindi wa CCM wakati wa uchaguzi!!

Wao pia kwa sasa wanaamini ni watu kutumwa tu na kuagizwa cha kufanya na watawala! Tena watawala wenye hitilafu vichwani!
 
TISS ya sasa ni tawi la uvccm, haina tena watu intelligent kama zamani bali imejaza makada ndio maana hali.iko hivi
 
Na ndio wanaotumiwa kuiba kura na ufisadi mkubwa.
Jamani nchi hii inevurugwa kabisa! Hata hao TISS wamevurugwa kabisa na kupoteza mwelekeo siku nyingi!

Angalia wanavyohangaika kushiriki katika vikao vya kutafuta ushindi wa CCM wakati wa uchaguzi!!

Wao pia kwa sasa wanaamini ni watu kutumwa tu na kuagizwa cha kufanya na watawala! Tena watawala wenye hitilafu vichwani!
 
Sio kwa TISS hii ilojaa makada na vijana wapumbavu.
Vijana hawa wa taasis hii nyeti kila kukicha tunakutana nao mitaa huku, tukiwa bar wakilewa kidogo basi wanaanza kututisha wanatoa tuvitambulisho vyao na vipistol wakitutisha unajua mi ni nani!
Imagine unaweka matumaini yako kwa agent ambae akinywa balimi moja anaanza kutuletea fujo.
Its tragic!
 
Mkuu leo nikupongeze umeshuka nondo nzuri sana za kizalendo. Mchango wangu TISS mjue kabisa hapa watu wanachangia kwa nia nzuri tu ya kuboresha nchi yetu, sasa basi viongozi wote wa ngazi zote ambao hawana sifa, weledi, busara, hekima muwatoe ili kulinda heshima ya taifa hili. Pili viongozi wote wa ngazi zote wenye utata wa uraia wao mfanye hivyo hivyo.

Tatu viongozi wote wa ngazi zote wenye matatizo ya afya ya akili muwatoe njia mnazijua. Nne mhakikishe kuwa maliasili zote za nchi zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote sio kikundi cha watu wachache wa CCM.

Tano mhakikishe kuwa mali za umma ziko salama, sio viongozi wasio waadilifu wanafanya embezzlement of public funds, tumieni njia za kijasusi kuzuia haya hata kama ni indirect mnatibua dili. Sita hakikisheni maisha ya watanzania wote yako salama pamoja na tofauti zao za kisiasa, uonevu usiwepo haki itendeke kwa raia wote, kama kuna kiongozi hatendi haki huyo hafai mnajua cha kufanya.

Saba hakikisheni pesa na mali zote za watanzania zilizoibwa na viongozi wakubwa zinarudi kwa wananchi. Nane ili Nchi ipate maendeleo hakikisheni nchi inapata viongozi waliochaguliwa kihalali na Wananchi, yaani mhakikishe waliochaguliwa kwenye uchaguzi halali ndio wanapata madaraka. Kwa sasa hayo tu baadaye nitaongeza.
Chifu Kabikula umeongea yale yale yaliyopo moyoni mwangu.
Hakuna heshima kubwa kama kuwa kiongozi kitaifa kwenye eneo flani,ama hata ngazi za mkoa na wilaya.
Unapotoa uamuzi mbaya,ama ukaongea vibaya mbele ya jamii inaliaibisha taifa.
Mamlaka iliyopo ikichelewa kutoa uamuzi wa uwajibikaji pia ni aibu kwa taifa.
Uongozi ukitoa uamuzi kwa kukurupuka ama kwa upendeleo pia ni shida.
Watu wanapopotea wasijulikane walipo na bila taarifa ni tatizo kwa taifa.
Watu wa idara waanapoacha kuchukua uamuzi kwa mambo haya ya kuuana mchana na hadharani,watu wanakosa matumaini kwa idara na kwa taifa.
Ni jambo jema kama mnachukua hatua za mapema ili kulinusuru taifa.
 
una TISS imara, una mahakama dhaifu, una bunge dhaifu, una ofisi ya CAG dhaifu, una PCCB dhaifu, una polisi wenye akili za kikoloni, una wanahabari makanjanja, una mahakama dhaifu, una chama tawala cha kikomunisti kinachoweka maslshi ya chama mbele kuliko hata ya nchi, kisha juu ya yote hayo una rais mungu mtu anayejifanya mjuvi wa kilakitu!
sahau maendeleo, uimara wa taifa unatokana na taasisi zake pamoja na mfumo mzuri wa kuwajibishana! mzee mkapa ndio rais pekee wa enzi hizi aliyeamini katika taasisi imara.

Asante kwa mchango wako...
 
!
!
Zamani Na Mimi Nilikuwa Naamini Hivyo Kwamba Jamaa Wana Uwezo Na Upeo Mkubwa Sana. Baadae Nikaja Kuambiwa Kuna Nafasi Fulani Fulani Huwezi Pata Kama Wewe Sio Mtu Wa Kitengo.

Nikimwangalia Dingilai, Bashite, Happy Mro Gwambo Jafu Na Wengine Kama Hao Nadhani Nadharia Ya Kuwa Na Upeo Na Uwezo Mkubwa Tuiondoe. Angalau Kwa Sasa.
Nakubaliana na wewe kwangu nafunga mjadala
 
!
!
Zamani Na Mimi Nilikuwa Naamini Hivyo Kwamba Jamaa Wana Uwezo Na Upeo Mkubwa Sana. Baadae Nikaja Kuambiwa Kuna Nafasi Fulani Fulani Huwezi Pata Kama Wewe Sio Mtu Wa Kitengo.

Nikimwangalia Dingilai, Bashite, Happy Mro Gwambo Jafu Na Wengine Kama Hao Nadhani Nadharia Ya Kuwa Na Upeo Na Uwezo Mkubwa Tuiondoe. Angalau Kwa Sasa.
ND nani hao umewataja
 
Back
Top Bottom