Parking Chini Ya Maghorofa Tuchukue Tahadhari Sana Wandugu.

MzaramoTz

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
1,829
2,986
Salaam kwenu wakuu.

Natoa tahadhari sana tunapotaka kuegesha magari tuweke sehemu iliyo salama wandugu

Hivi punde tu kuna jamaa aliegesha gari aina ya Prado maeneo ya Kariakoo karibu na stendi ya daladala za Msasani kwenye linalouza ice cream hizi za Azam, zikaanguka tiles mpaka kwenye na kuvunja kioo cha gari.

Sasa sijajua sheria hapo inasemaje kuhusu kufidiwa ni gharama yake mwenyewe kama haijakatiwa bima au ni mwenye jengo au hawa wanaokatisha tiketi za maegesho...? Wajuzi mtatuambia katika hilo.

Nikasema nitoe tahadhari kwa kushea na nyinyi wandugu mchukue tahadhari mnapoegesha magari muegeshe sehemu iliyo salama.

IMG_20190620_105412_1.jpg
IMG_20190620_105351_3.jpg
IMG_20190620_114016_0.jpg
 
MangoFarm kulikuwa na ujenzi? Hizo tiles zimedodndoka kutoka jengo linalojengwa?

Hapana mkuu RRONDO hakuna ujenzi ni jengo ambalo limeshamalizika na kuanza muda tu zaidi ya mwaka au miaka hivi.

Ila hizo tiles zimeanguka kutokea ukutani nafkiri cement waliyochapia haikuwa na nguvu-mgandisho ya kutosha mkuu. Zimechoka kwa hiyo zimebanduka toka juu ghorofani mpaka kwenye kioo cha gari mkuu.
 
Nchi ya Singapore ina sheria kali sana kuhusiana na kutupa vitu ghoforani, aidha kwa bahati mbaya au makusudi. Fine yake si mchezo.

Natumai hizo sheria zikiwepo pia hapa nchini zitasaidia sana. Ila tatizo inaweza kuwa nimezungukwa gharama sana kwa sababu itahitaji walau camera kuthibitisha mtu aliyetupa kitu husika mkuu.
 
Hapana mkuu RRONDO hakuna ujenzi ni jengo ambalo limeshamalizika na kuanza muda tu zaidi ya mwaka au miaka hivi.

Ila hizo tiles zimeanguka kutokea ukutani nafkiri cement waliyochapia haikuwa na nguvu-mgandisho ya kutosha mkuu. Zimechoka kwa hiyo zimebanduka toka juu ghorofani mpaka kwenye kioo cha gari mkuu.
Apambane na mwenye jengo alipe.
 
Hapana mkuu RRONDO hakuna ujenzi ni jengo ambalo limeshamalizika na kuanza muda tu zaidi ya mwaka au miaka hivi.

Ila hizo tiles zimeanguka kutokea ukutani nafkiri cement waliyochapia haikuwa na nguvu-mgandisho ya kutosha mkuu. Zimechoka kwa hiyo zimebanduka toka juu ghorofani mpaka kwenye kioo cha gari mkuu.
Hatari sana nimejaribu kuvuta picha ingekuwaje icho kigae kingempata mpita njia loh!
 
Hatari sana nimejaribu kuvuta picha ingekuwaje icho kigae kingempata mpita njia loh!

Daaaah aisee madhara makubwa sana yangetokea mkuu. Mi nafkiri angeweza hata kuzimia kama sio kufa kabisa mkuu.

Ni hatari sana kwa kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom