Papaa Msofe Arudisha kiwanja alichotapeli

Clarity

JF-Expert Member
Jul 6, 2010
1,583
2,082
Taarifa Habari ya saa mbili ITV imemuonyesha Mjane aitwae Devotha akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa kiwanja alichotapeliwa na Msofe
 
kile kiwanja cha kinondoni mbezi beach kilichokuwa kwenye mgogoro kati ya papa msoffe na bi.Devotha mulay, hatimie haki imetendeka baada ya papa msoffe kuamua kuachia kiwanja leo 11/11/2011 kama alivyokua kagizwa na serikali.mia
 
Naofia usalama wa mama devotha mie namshauri auze hicho kiwanja atokomee sehemu isiyojulikana maana msofe lazima amuue
 
Hakuna lolote,
labda auwawe yeye kwa sumu ya panya, tena akinywa supu ya ngumi pale leaders kesho asubuhi.
Naofia usalama wa mama devotha mie namshauri auze hicho kiwanja atokomee sehemu isiyojulikana maana msofe lazima amuue
 
Ni Msofe huyu member wa JF? Au wana uhusiano wa majina tu !?
Hapana si huyu member wa JF!! Ni yule kiboko ya investors wa kichina anawapiga kuanzia kopa feki mpaka kuwakodisha magodown ambayo hana miliki nayo jamaa ni kiboko na serikali inatambua hilo
Nampongeza huyo mama kwa kukomaa nae lakini ndio ajiangalie kwani jamaa ana mtandao wa kimafia sidhani kama ameachia kiroho safi
 
Leo haki imetendeka kwa serikali ya magamba mbele ya mwenye hela ajabu kwelikweli, ningesema ni kwavile pinda kaingilia lakini sio mbona lilesuala la jeri muro alisema hukumu yakd ifanyike mapema mwisho wake muda umeenda sana na jeri kuishia kutimuliwa kazi kabla ya kujulikana kama ni mwalift au la
 
Hata mimi nimeona huyo mama akishukuru, aangalie asije akashindwa kuikalia maana jamaa situmaini kama atakuwa ameiacha kwa roho nyeupe kabisa,
 
Leo haki imetendeka kwa serikali ya magamba mbele ya mwenye hela ajabu kwelikweli, ningesema ni kwavile pinda kaingilia lakini sio mbona lilesuala la jeri muro alisema hukumu yakd ifanyike mapema mwisho wake muda umeenda sana na jeri kuishia kutimuliwa kazi kabla ya kujulikana kama ni mwalift au la
Alikosea step nadhani ameingia cha kike! na kwa kuwa maza amekomaa,hakuna haki yoyote wangapi wanateseka kwa staili hiyo.
 
Huyo Mama ni jasiri. Angezubaa kidogo, kiwanja kingetwaliwa kimabavu!
Lakini wako Watanzania wengi sana Mitaani wenye matatizo ya kudhulumiwa kama Mama Devotha.
Nani awasaidie Masikini hawa Yarabi? Maana haya Matapeli yana jeuri kubwa mno ya Pesa. Jumlisha na zile kauli "maafisa wote wako mfukoni"
 
Hivi serekali yetu inataka kutufundisha nini? Yaani waziri wa mambo ya ndani anasuluhisha kesi ya Ardhi na waziri wa Ardhi mwenye kofia ya Professor anashindwa! Nilidhani mama Tibaijuka au Professor Tibaijuka kama anavyofahamika ndiye angelivalia njuga suala hili kutetea mjane lakini kumbe na yeye amenunuliwa na mafisadi. Kwani huyu Marijani Msofe ni nani hasa mpaka anatapeli watu wengi hivi hachukuliwi hatua yoyote. ITV wanasema eti ameambiwa arudishe kiwanja alichoiba, ndio sheria zetu zinavyosema?
 
Back
Top Bottom