Papa Francis (VATICAN), ana ushawishi gani Zanzibar?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Out of Curiosity!

Imeripotiwa katika vyombo vya habari leo kuwa Maalim Seif, anayedai kuwa alipokwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana, amemuomba Papa Francis kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa mvutano unaoendelea visiwani humo.

Nimejiuliza tu Papa au Vatican ina uwezo au ushawishi wowote katika kuingilia siasa za Zanzibar?!

==============
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Benedict XVI kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.

Chanzo:
Nipashe
 
Out of Curiosity!

Imeripotiwa katika vyombo vya habari leo kuwa Maalim Seif aliyepokwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana, amemuomba Papa Francis kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa mvutano unaoendelea visiwani humo.

Nimejiuliza tu Papa au Vatican ina uwezo au ushawishi wowote katika kuingilia siasa za Zanzibar?!
Hii ni kama wale walioenda ICJ
 
Mkwamo wa kisiasa Zanzibar watua rasmi kwa Papa vatican.Hatua hiyo imechukuliwa na Maalim Seif.Baada ya kumwandikia Papa barua na kumweleza hali ya kisiasa ya Zanzibar
Kwa kumshirikisha Papa Fransis Maalim ameendelea kuonyesha nia yake njema kwa Zanzibar na kiu kubwa ya kuutatua mgogoro huu.Heshima nyingi kwako Maalim
 
Out of Curiosity!

Imeripotiwa katika vyombo vya habari leo kuwa Maalim Seif aliyepokwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana, amemuomba Papa Francis kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa mvutano unaoendelea visiwani humo.

Nimejiuliza tu Papa au Vatican ina uwezo au ushawishi wowote katika kuingilia siasa za Zanzibar?!

CUF Wanacheza karata zao za kisiasa kimataifa na ndani vizuri na kidiplomasia.
  • kwanza tukubali CUF walishinda Uchaguzi wa Zanzibar ila CCM hawataki kuondoka madarakani
  • pili ijulikane Vatican ina uhusiano mzuri na CCM Na ina ushawishi wake kupitia Kanisa lake Tanzania
  • Papa Francis ametokezea kuwa champion wa usawa, haki sehemu zote duniani. Hata Palestine amei tambua kama nchi
  • CUF imezungumza na karibu Balozi zote ziliopo Tanzania....hata zile ambazo hazijali siasa za ndani kama China , UAE
  • Ni Maalim ndie pekee ameanzisha jitihada binafsi kwa niaba ya CUF kuleta suhulu na kutaka maamuzi ya wananchi yaheshimie. ukumbuke CCM hawakua na nia wala sababu ya mazungumzo . Kikwete aliandikiwa na kupigiwa simu na Maalim akakacha mpaka ikaripotiwa na media ndio akajitoa kimaso maso kumkaribisha Maaalim ikulu kupiga picha na kutoka kauli ya ajabu ati amemwagiza mkuu wa majeshi akutane na Maalim!!!
  • CUF Kimeweza kuwashawishi wananchi kuwa na subira na wasichokozeke.
  • Maaalim amehudhuria mazungumzo ikulu znz na CCM inaonekana wazi kwamba hawako tayari kumpa Maalim haki yake sio tu uchaguzi huu bali hata wa marejeo. kwao wao lazima washinde wao .
ni wazi suala hili sasa limefika ukingoni na Maalim anamuomba Papa amshawishi bila ya shaka Magufuli awe mkweli na atende haki. Jitihada hizi zinatosha kutoa salamu kuwa CUF wamefanya kila liwezakanalo kutafuta haki kwa njia ya amani lakini imeshindikana. Na CCM inaandaa uchaguzi haramu bila ya shaka uchaguzi huo kuna kila dalili utaleta shari kubwa mabayo haijawahi kutokea huko znz ..
  • CUF Hawatashiriki na Pemba 95% ni CUF bila ya shaka watazuia kufanyika uchaguzi huo hivyo Pemba hawatashiriki kwa njia zote kumchagua Sheni
  • Kuna uwezekan wa kufanyika maandamano siku ya uchaguzi hivyo watu wengu wa Unguja kujifungia ndani kuepusha shari. Na hali ikiendelea uchaguzi huo wa marudfio hautofanikiwa kwani kuna uwezekano watu watao jitokeza ikawa chini ya asilimia 40 ya wale walio ipigia CCM mwezi October 2015. ambao hawatazidi watu 50,0000.
  • hii itakua aibu ya mwaka na upotevu wa pesa ingawa CCM Bila aibu wao watajitangazia wameshinda.
  • tutegemee kurudi kwenye vurugu na hasama na uchumi kuangaka na vitu kupanda na maisha kuwa magumu sana.
sasa CUF yakitokea haya itakua imejivua lawama kwani imefanya juhudi kubwa kutaka CCM waache tamaa ya kutawala bila ya ridhaa. CUF Itakua imenawa mikono ...Lawama zote zitakuwa CCM .Ikiwa kuna mauaji , haki za binadamu na mambo ya Kushtakiwa mahakama ya kimataifa CCM wajitayarishe
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Benedict XVI kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.

Chanzo:
Nipashe
 
Last edited by a moderator:
Mmmmmh ila CCM ni noma sana, yani hawana tofauti na Nkurunzinza sema Watanzania ni watu wapole tu na wasiopenda makuu
 
Ukiangalia kwa umakini tabia za ajabu ajabu za wanasiasa wa Tanzania kiwa ni pamoja na Zanzibar ambao ndani ya ccm ni chuki, majigambo na fitina huku wanaojiita wapinzani wakijawa na usaliti uliopindukia. Hapo ndio utagundua kwamba Seif ni mtu mwenye busara kubwa sana na na anatoa mchango mkubwa katika stability ya Zanzibar, siku akiwa hayupo ndip wengi tutajua hilo.
 
Maalimu Seif sasa amwangukia Papa Benedict uchaguzi Z'bar.
Na Waandishi wetu
14th January 2016
B-pepe
Chapa
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Benedict XVI kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana ambayo gazeti hili imefanikiwa kuona nakala yake, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua kama mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.

CHANZO: NIPASHE
Papa Benedict??
 
Zanzibar kuna waitaliano wengi sana, yaani Italy na Zanzibar wana uhusiano Mzuri ktk utalii. Ndio maana kuna hotel za waitaliano nyingi kule kuliko bara. Huenda maalim katumia Njia hiyo kwakua wana uhusiano wa karibu.
 
Out of Curiosity!

Imeripotiwa katika vyombo vya habari leo kuwa Maalim Seif, anayedai kuwa alipokwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka jana, amemuomba Papa Francis kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa mvutano unaoendelea visiwani humo.

Nimejiuliza tu Papa au Vatican ina uwezo au ushawishi wowote katika kuingilia siasa za Zanzibar?!

Kama Pope ameweza kuisaidia Jamii ya watu wa Central Africa waliopigana kwa sababu ya chuki za dini zao hata Zanzibar anaweza,maana ni neutral person kw aupande wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom