Papa Francis: Nitakufa baada ya miaka miwili au mitatu

Papa Francis: Nitakufa baada ya miaka miwili au mitatu

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
papa+px.png
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu.

"Suala hili naliona kama neema tu ya Mungu kwa watu wake. Najaribu kutafakari kuhusu dhambi zangu na makosa yangu, siwezi kujivuna. Najua kwa sababu hali hii itadumu kwa muda mchache. Miaka miwili au mitatu nitakuwa nimeondoka na kwenda nyumbani kwa baba," alisema.Papa Francis (77), pia alizungumzia uwezekano wa kustaafu endapo atahisi kwamba afya yake hairuhusu kuendelea na kazi.

Utamaduni wa kuachia madaraka ndani ya kanisa hilo linalotajwa kuwa na waumini wengi duniani uliasisiwa upya mwaka jana na mtangulizi wake, Papa Benedict XVI aliyeng'atuka kutokana na matatizo ya kiafya.Pamoja na kwamba Papa Francis hajawahi kuzungumza hadharani kuhusu ni lini pengine anaweza kufariki dunia, lakini baadhi ya vyanzo vya habari kutoka Vatican vinasema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuhusu siku zake chache zilizosalia duniani.

Wachambuzi wa masuala ya kiimani kwa nyakati tofauti walisema huenda kiongozi huyo ana tatizo la kiafya ambalo halijawekwa wazi.Wakati hayo yakiendelea taarifa za ndani zinabainisha kwamba kiongozi huyo aliwahi kutolewa pafu moja baada ya kuathirika wakati akiwa kijana nchini Argentina.

Source: Mwananchi Publications
 
Uhai na Umauti vipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu (SW), hakuna anaejua saa ngapi atakufa, siku gani atakufa, mwezi gani atakufa na mwaka gani atakufa. Asubuhi Njema.
 
May God bless him.
Nachelea wakristu wa kisasa wasijesema ana pepo wa mauti...hawajui kuwa duniani tuko safarini na kwamba kwa kufa ndipo tunazaliwa katika uzima wa milele.
 
Uhai na Umauti vipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu (SW), hakuna anaejua saa ngapi atakufa, siku gani atakufa, mwezi gani atakufa na mwaka gani atakufa. Asubuhi Njema.
 
Ukifa umekufa, hata walie wangapi ukifa yako yameisha utasubiri siku Yesu akirudi kwa wenye haki wataenda kumlaki mawinguni, wadhambi watalala na baada ya miaka 1000 watahukumiwa kwa kuchomwa moto
 
Philippians 1:21-24
21) For to me to live is Christ, and to die is gain.
22) But if I live in the flesh, this is the fruit of my
labour: yet what I shall choose I wot not.
23) For I am in a strait betwext two, having a
desire to depart, and to be with Christ: which is
far better:
24) Nevertheless to abide in the flesh is more
needful for you
 
Papa hajatabiri kufa kwake,amesema general observation ya nabii mussa toka zaburi ya 90.
Anajua ana miaka 77 hivyo baada ya miaka mitatu atakuwa na miaka 80.
Psalms 90: 10 The length of
our days is seventy years-- or eighty, if we have
the strength; yet their span is but trouble and
sorrow, for they quickly pass, and we fly away.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom