barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa "dhambi na makosa yaliyotekelezwa na Kanisa na waumini wake … ambao walitekwa na chuki na ghasia" wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda.
Alikuwa akiongea baada ya kukutana na Rais Paul Kagame mjini Vatican.
Ombi lake la msahama limetokea baada ya ombi la Rwanda Novemba mwaka jana kwa Vatican kuomba radhi kutokana na mchango wa mapadri wa kanisa Katoliki na baadhi ya viongozi wake wakati wa mauaji hayo ya mwaka 1994
Kwa mujibu wa Vatican Radio, Papa pia "ameelezea nia yake kwamba kutambua udhaifu huu wa kanisa kipindi hicho, ambao, uliathiri sana sifa za Kanisa, kunaweza kuchangia 'kutakaswa kwa kumbukumbu' na kuendeleza, kwa matumaini na uaminifu, amani siku za usoni."
Wakati wa mauaji hayo yaliyodumu siku 100, Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa kadiri waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo yalitekelezwa hadi katika makanisa ambapo watu walikuwa wamekimbilia kutafuta hifadhi.
Papa Francisko kwa niaba ya Kanisa aomba msamaha kwa mauaji ya kimbari - Radio Vatican