Panya kutoa milio na sauti za ajabu usiku wa manane

Kim Il Kwon

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,219
1,034
Salaam wakuu,
Ni siku ya tatu hapa chumbani kwangu kila ifikapo mida ya saa nane mpaka kumi usiku kuna panya ananikosesha amani kabisa. Anatoa milio na sauti za kutisha mithili ya mtu mwenye sauti nene na koo lilolegea akikoroma. Mwanzoni (usiku wa kuamkia juzi) nilikurupushwa toka usingizini na purukushani na heka heka za huyu kiumbe wa ajabu, alikua akirukaruka na kushangilia kama shabiki wa yanga siku simba inafungwa. usiku wa jana kama kawaida ya huyu panya alifanya yake, nikaamka kimya kimya nikammlika ghafla kwa tochi ya simu, duh nilishangaa alikua kasimamia miguu ya nyuma tu. kutokana na kupigwa taa gafla akazubaa nikampiga teke asee alikopotelea mpaka sasa sielewi. Mpaka naandika uzi huu ni kwamba ni nusu saa tu imepita kiumbe yule yule alikua anatumbuiza, tena this time round alikua jirani na kitanda changu. Hiki kiumbe kinaninyima amani kabisa. Nifanyeje?
Cc: mshana jr jichawi Mzizi mkavu Maisha popote
 
Atakua anakaribia kuzaa huyo amini maneno yangu mkuu ukimchelewesha mpaka kesho utakuta amesha mwaga vitoto zaidi ya 10,
 
mkuu ushahusisha na ushirikina?
huyo muwekee sumu, au mlie timing, hapo ulipompiga teke inawezekana aliangukia mahala ila akazuga kimya ili usimmalizie, panya wajanja kama mtu vile
 
Back
Top Bottom