Pancha kwenye upande wa tairi

Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Wakuu nimefuatilia kwenye mtandao inasemekana tairi likipata pancha yeyote kwenye sidewall sio vizuri kuiziba.
Wajuzi hebu tusaidie pancha ya kama kwenye picha hapo tunatupa tairi.
20200622_142019.jpg
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,744
2,000
Inawezekana,mimi kuna tairi langu moja la Goodrich lilikuwa bado kabisa na kashata zake nzuri,lilichanika pembeni,sikujua hata nilikanyaga nini,nikalipeleka kwa fundi kuziba akanitolea nje vibaya akasema kuwa haliwezi kuzibika,basi sikuwa na ujanja nikaliacha,labda ngoja waje wajuzi watoe ufafanuzi...
 
Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
737
1,000
Si vema na pia si salama kwa safari ila kuna mbadala wa hilo.Kuna dawa fulani inaitwa OKO sijui kingereza chake hiyo inafaa sana kuzibia pancha na matundu ya matairi ili mradi tairi liwe zima si kipara au la kuchonga.Nunua hiyo kuliko kuziba na utambi.
 
Proffesor

JF-Expert Member
Aug 13, 2014
1,752
2,000
Wakuu nimefuatilia kwenye mtandao inasemekana tairi likipata pancha yeyote kwenye sidewall sio vizuri kuiziba.
Wajuzi hebu tusaidie pancha ya kama kwenye picha hapo tunatupa tairi
Wataalamu wanasema Ni rahis sana kupasuka mkuu especially kwenye jua kali ... ni vyema kununua tairi mpya...
 
Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Inawezekana,mimi kuna tairi langu moja la Goodrich lilikuwa bado kabisa na kashata zake nzuri,lilichanika pembeni,sikujua hata nilikanyaga nini,nikalipeleka kwa fundi kuziba akanitolea nje vibaya akasema kuwa haliwezi kuzibika,basi sikuwa na ujanja nikaliacha,labda ngoja waje wajuzi watoe ufafanuzi...
Shukrani mkuu, nimekusoma
 
Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Si vema na pia si salama kwa safari ila kuna mbadala wa hilo.Kuna dawa fulani inaitwa OKO sijui kingereza chake hiyo inafaa sana kuzibia pancha na matundu ya matairi ili mradi tairi liwe zima si kipara au la kuchonga.Nunua hiyo kuliko kuziba na utambi.
Inabidi nitafute hiyo oko, ila kwa sasa kimeshakosa amani.
 
Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Wataalamu wanasema Ni rahis sana kupasuka mkuu especially kwenye jua kali ... ni vyema kununua tairi mpya...
Shukrani mkuu, elimu ya matairi ni hafifu hapa kwetu. Mafundi wa mtaa wanasema haina shida ila kila nikifungua mtandao naona vitu vya ajabu ajabu
 
rasulimohamed

Senior Member
Jul 12, 2019
117
250
Wataalamu wanasema Ni rahis sana kupasuka mkuu especially kwenye jua kali ... ni vyema kununua tairi mpya...
Hyo OKO sio nzur sana kwa matair mapya, nilishuhudia jamaa alinunua matair mapya zen akatia OKO na alikuwa na safar ya mwanza, huwez amin zilipasuka zote njian tena tairi mbili kwa pamoja, sema kwa bahat nzur zile tair mbili alizo toa alizi beba na ndo zikamsaidia kumalizia safar zake
 
wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
4,514

Na hushauriwi kununua tairi mbpya then ukaanza nazo safari ndefu hapo hapo at least zipigiwe misele kwanza ya hapa na pale ya kutosha.
 
Master C mimd

Member
Sep 26, 2019
44
125
Hyo OKO sio nzur sana kwa matair mapya, nilishuhudia jamaa alinunua matair mapya zen akatia OKO na alikuwa na safar ya mwanza, huwez amin zilipasuka zote njian tena tairi mbili kwa pamoja, sema kwa bahat nzur zile tair mbili alizo toa alizi beba na ndo zikamsaidia kumalizia safar zake

Hiyo dawa niliwahi weka kwenye mipira hii ya kuchezea udundaji wake tu ulibadilika, haikuwa inadunda vizuri kama ilivyokuwa kabla ya kuweka hiyo oko
 
RugambwaYT

Verified Member
Jan 11, 2014
1,254
2,000
Hyo OKO sio nzur sana kwa matair mapya, nilishuhudia jamaa alinunua matair mapya zen akatia OKO na alikuwa na safar ya mwanza, huwez amin zilipasuka zote njian tena tairi mbili kwa pamoja, sema kwa bahat nzur zile tair mbili alizo toa alizi beba na ndo zikamsaidia kumalizia safar zake
Haifai kabisa. Huwa inakauka na kujikusanya sehemu moja. Inaharibu wheel balance. Ukiwa safari gari litakuboa aise. Hayo madude hayafai.
 
RugambwaYT

Verified Member
Jan 11, 2014
1,254
2,000
Wakuu nimefuatilia kwenye mtandao inasemekana tairi likipata pancha yeyote kwenye sidewall sio vizuri kuiziba.
Wajuzi hebu tusaidie pancha ya kama kwenye picha hapo tunatupa tairi. View attachment 1486031
Kama tairi bado zima kuna jamaa wanaweka kiraka cha moto. Linapiga kazi viruzi tu. Linaweza maliza maisha yake. Japo kwa usalama, ukiziba ni bora likatumika mjini tu. Kwenye safari sio uhakika saana.
 
Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Kama tairi bado zima kuna jamaa wanaweka kiraka cha moto. Linapiga kazi viruzi tu. Linaweza maliza maisha yake. Japo kwa usalama, ukiziba ni bora likatumika mjini tu. Kwenye safari sio uhakika saana.
Toa location mkuu
 
RugambwaYT

Verified Member
Jan 11, 2014
1,254
2,000
Toa location mkuu
Niliziba nikiwa safarini Mwanza. Ila hilo tundu kwenye tairi lako ni dogo saana. Wala hakuna haja ya kiraka cha moto. Hapo ilifaa kuliziba kwa kiraka kinachowekwa ndani ya tairi, kile cha gundi, sio hicho cha uzi. Kingeshika viruzi saana. Mie balaa lilinonikuta sio la kitoto. Ndio ikabidi waweke hicho kiraka cha moto.
21022017805.jpg
 
fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,685
2,000
Niliziba nikiwa safarini Mwanza. Ila hilo tundu kwenye tairi lako ni dogo saana. Wala hakuna haja ya kiraka cha moto. Hapo ilifaa kuliziba kwa kiraka kinachowekwa ndani ya tairi, kile cha gundi, sio hicho cha uzi. Kingeshika viruzi saana. Mie balaa lilinonikuta sio la kitoto. Ndio ikabidi waweke hicho kiraka cha moto.
View attachment 1488198
Hapo unatembea na tiketi ya kifo,trust me hasa kama unasafari ndefu.
 
Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
642
1,000
Niliziba nikiwa safarini Mwanza. Ila hilo tundu kwenye tairi lako ni dogo saana. Wala hakuna haja ya kiraka cha moto. Hapo ilifaa kuliziba kwa kiraka kinachowekwa ndani ya tairi, kile cha gundi, sio hicho cha uzi. Kingeshika viruzi saana. Mie balaa lilinonikuta sio la kitoto. Ndio ikabidi waweke hicho kiraka cha
Mkuu hilo lilitembea safari ya mkoa.
Au lilikuakwa route za mjini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom