tramadol
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 5,383
- 4,323
Zikiwa zimepita siku 91 tangu Rais John Magufuli apige marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini Nje ya nchi bado hatima ya suala hilo haijafahamika.
Hata hivyo uamuzi huo haujaathiri mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama kwa kutoendelea kutekeleza miradi ya jamii.
Meneja wa mgodi huo Stewart Hamilton amesema wataendelea kutekeleza miradi hiyo bila kujali mgogoro uliopo kati yao na Serikali.
Akikabidhi vifaa vya ujenzi wa bweni la wasichana ktk Sekondari ya Mwendakulima Meneja huyo alisema miradi itatekelezwa yote kwasababu haina uhusiana na suala la makinikia.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kukamilisha miradi ya wanainchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kati ya migodi 4 iliyopo kanda ya ziwa Buzwagi ni mgodi mdogo lakini ndiyo unaofanya mambo makubwa ya maendeleo Katika wilaya hiyo.
Chanzo:Mwanainchi