Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
SERIKALI imeonyesha jitihada kubwa katika kupambana na ugonjwa wa malaria ambapo maambukizi yanatajwa kwamba yameshuka kutoka asilimia 18 kwa mwaka 2007/2008 hadi asilimia 10 mwaka 2011/2012.
Lakini pamoja na kupungua kwa maambukizi hayo, takwimu zinaonyesha ugonjwa huo bado ni tatizo kubwa katika vijijini ikilinganishwa na maeneo ya mjini ambapo maambukizi ya maeneo ya vijijini ni asilimia 10.7 na mjini ni aslimia 3.4
Kupungua kwa maambukizi hayo kunatajwa kwamba ni kutokana na mwamko ambao wananchi wameupata wa kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na mbu waenezao malaria, mwamko ukionekana kuwa mkubwa zaidi mijini kuliko vijijini.
Soma zaidi hapa=> Pamoja na kupungua kwa maambuki, Malaria bado tatizo kubwa vijijini | Fikra Pevu