Pamoja na kauli ya Pinda wapinzani wanyimwa miradi ya maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na kauli ya Pinda wapinzani wanyimwa miradi ya maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sosoliso, Apr 16, 2012.

 1. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Licha ya waziri mkuu, Mh. Mizengo Pinda kudai Serikali inatoa fedha za maendeleo bila ya ubaguzi wa itikadi, hali ni tofauti kwa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kutokana na Madiwani wa CCM kutaka kata zinazoongozwa na upinzani zisipewe miradi mipya ya maendeleo..

  Mh. Pinda alilazimika kutoa majibu hayo baada ya kuulizwa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Mh. Freeman Mbowe kutokana na kauli zilizowahi kutolewa na Mawaziri waandamizi kama vitisho kwa wananchi kuwa wakiwachagua wapinzani hawatapata maendeleo..

  Kamati ya Madiwani baada ya uchaguzi iliweka misimamo wa kutopitisha fedha za ujenzi huo, huku wanafunzi wakilazimika kukaa zaidi ya miezi saba nyumbani mpaka ujenzi ulipokamilika kwa michango ya wazazi na wadau wa elimu. Pia katika kikao cha bajeti cha Madiwani kilichoketi katikati ya wiki iliopita, Madiwani ambao wengi wanatoka CCM walipendekeza miradi ya ujenzi wa barabara kata za Nyansurura na Machochwe, zinazoongozwa na upinzani ziondolewe na badala yake zipelekwe kata za Madiwani wa CCM..

  Madiwani wa CCM waliazimia kwenda kumuona Waziri wa elimu na ufundi na Katibu mkuu wa CCM, kuwashtaki wataalam waliopitisha ukarabati wa shule iliyo chini ya upinzani..

  Source: Mwananchi

  My Take:
  Bado tuna safari ndefu sana kufikia demokrasia..
   
 2. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao madiwani wa ccm wanaopinga kata za upinzani kupewa miradi ya maendeleo siku zao za kuendelea kukaa Halmashauri unahesabika watatolewa na umma kwa njia ya kura 2015.
   
 3. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  upo sawa kabisa.
   
 4. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,928
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Pinda si lolote mbele ya mikakati ya ccm, hovyo kabisa kumbuka aliwahi kumwambia fedhuli Mkapa kuwa hataki ubunge anataka abakie na kazi yake ndani ya ikulu maana ni mwoga kupoteza ajira, so yuko radhi kuongea uongo ili kazi yake idumu.
   
 5. k

  kwamagombe Senior Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama hali ipo hivyo basi ni hatari sana kwa demokrasia tz, nashauri sana viongozi wetu wawe makini na hoja zao hasa za kutopeleka maendeleo maeneo yanayoongozwa na upizani, watu washindane kwa sera ha hoja
   
 6. m

  matawi JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  shhhhhh msiwashtue magamba tunakuja kuwaadhibu kama tulivy0fanya arumeru
   
 7. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Shirtsitedness! Viongozi wengi ndio akili yao, hivi unafikiri mtu kama magufuri anawaza nn akilinimwake? Ni ***** tuu!
   
 8. broken ages

  broken ages Senior Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ikiwa haya yasemwayo yana ukweli nawashauri hao madiwani na serikali kwa ujumla kubadilika kwani hii ni hatari zaidi kwa ccm kwani wananchi wanaonyimwa miradi wakigundua sababu hizi za kiitikadi ni kwamba wataichukia sana na zaidi ccm watakosa imani kabisa na hicho chama watakijengea chuki ambayo madhara yake ni makubwa kuliko ilivyo sasa..
   
Loading...