Pamoja na Azam kushusha bei za vifurushi, kuna kitu hatujakielewa wateja wenu

KASULI

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
599
669
Azam tv kwa kifupi wameamua kushusha zaidi vifurushi vyao kutoka 10000 kwa mwezi hadi 8000 kwa mwezi channel zaidi ya 55

Pure kutoka 18000 hadi 13000 kwa mwezi
Channel zaidi ya 60

Plus kutoka 23000 hadi 20000 kwa mwezi
Channel zaidi ya 90

Na hapo hakutakua na malipo ya ziada ya baadhi ya channels kama ilivyokua mwanzoni mfano wasafi ilikua ikilipiwa yenyewe kwa package yake but sasahivi ukilipa hiyo 8000 mathalani inakua na hizo wasafi unazipata

Halafu huku local channel ni bure na wameamua kuondoa yale ya Malipo ya Nyongoza kwa Channel kama Wasafi Tv.

Shida yangu na ambayo naona ni shida ya watu waliowengi ni Je, tutaendeleaa kupata channel vile vile kama Zaman kwa bei mpya, yaan wale wa Azam Pure tuliokuwa tunalipa tulikuwa tunapata Channel kama Azam sports 1 & 2 HD?

Kama hilii ni tofauti basii wapenzi wa mpira tutakuwa tumedhurumiwa mnoo yaan kutokaa ts 18,000/= mpaka 20,000/=

Angalau wangetusogezea ts 15000/= ili tuendane na uchumi wa kati.

Naomba kuwasilisha.
 
Tena wangepandishs viwe Kama DSTV ,sisi tuko uchumi wa kati tutalipa bila wasiwasi.
 
Kama hizi habari nizakweli bas PONGEZI ZIWAENDEE MANAGEMANT NZIMA YA AZAM MEDIA HUU NDIO UZALENDO WAKWELI nazan sasa azam wanataka kila mtanzania aweze kuona ligi ya nyumbani akiwa sebleni kwake ..wabarikiwe sana mana wengine kila uchwao wanapandisha bei zavifurushi
 
Wanajitahidi nmetoka kuchek Chelsea vs Newcastle, Simba vs coastal saiv nko nachek Hoffenheim vs Stuttgart
 
Kama hizi habari nizakweli bas PONGEZI ZIWAENDEE MANAGEMANT NZIMA YA AZAM MEDIA HUU NDIO UZALENDO WAKWELI nazan sasa azam wanataka kila mtanzania aweze kuona ligi ya nyumbani akiwa sebleni kwake ..wabarikiwe sana mana wengine kila uchwao wanapandisha bei zavifurushi
Ligi ya home utaicheki kwa 20,000 na sio 18,000

kama jana uliangalia uzinduzi wa ule mzigo kuna wakat fulani walipitisha tangazo na kuonyesha ligi ya bongo na ujerumani iko kifurushi cha elfu 20

kile cha 13000 hakitakuwa na azam sport 1 na 2

kwa maneno mepesi wamepandisha vifurushi kwa zile chanel muhimu na kushusha kifurush kwa zile chanel za ovyo
 
Me nikajua channels zimebaki kama zilivyo.....
 
Me nikajua channels zimebaki kama zilivyo.....
Wameongezea bei na sio kushusha bei mfano ili kuweza kuangalia azam 1&2 ulitakiwa ulipie sh. 10,000 Lakini kuanzia tarehe 1 /12/2020 utalipia 13000 ndio uone azam1&2

ligi bongo ili kuiangalia unatakiwa sh.18,000 kuanzia disemba mosi utatakiwa ulipe sh. 20,000

pamoja na kupandisha nawapongeza wanajitahidi sana
 
hapa sasa watuongezee na michezo sasa........
 
Hili ni jibu kutokaa Azam
Screenshot_20201121-221932_Lite.jpg
 
Azam wamefanya kauhuni hivi, mpira wameongeza bei (2,000/=).

Ila tunashukuru kwa kuleta Antena
 
Back
Top Bottom