Pamoja na ada Kidato cha Tano kufutwa bado tumelipia

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Tuombe ufafanuzi kwa hili,

Baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kutangaza kuwa kuanzia sasa hakutakuwepo ada kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2022/2023 sisi wazazi katika kumwandaa mtoto na mahitaji yake tumepambana na kipengele cha ada katika fomu za kujiunga.

Baada ya kuhoji uongozi wa shule wanasema kuwa bado hawajapata Waraka wa Serikali, hivyo tumetakiwa kulipa ada kawaida.

Tuiombe Serikali kupitia Wizara ya Elimu kulisimamia hili ili turejeshewe ada tuliyolipa ambayo serikali imeishaifuta.
 
Tuombe ufafanuzi kwa hili
Baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kutangaza kuwa kuanzia sasa hakutakuwepo ada kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga...
Kwa nyie kabisa kwa 'Upopoma' wenu mliamini kuwa kuna cha bure ndani ya Tanznania hii ya Muigizaji na Mtemi Mkuu?
 
Tuombe ufafanuzi kwa hili,

Baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kutangaza kuwa kuanzia sasa hakutakuwepo ada kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2022/2023 sisi wazazi katika kumwandaa mtoto na mahitaji yake tumepambana na kipengele cha ada katika fomu za kujiunga.

Baada ya kuhoji uongozi wa shule wanasema kuwa bado hawajapata Waraka wa Serikali, hivyo tumetakiwa kulipa ada kawaida.

Tuiombe Serikali kupitia Wizara ya Elimu kulisimamia hili ili turejeshewe ada tuliyolipa ambayo serikali imeishaifuta.
Simple tuu nenda kamlipoti huyo mkuu wa shule kwa DC hapo, kesho hutomkuta kazini.

Yeye ni nani hadi apingane na Rais? Kama ni ada za mwaka huu lazima ulipe ila kama ni za mwaka ujao wa Fedha hapana.
 
Tuombe ufafanuzi kwa hili,

Baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kutangaza kuwa kuanzia sasa hakutakuwepo ada kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2022/2023 sisi wazazi katika kumwandaa mtoto na mahitaji yake tumepambana na kipengele cha ada katika fomu za kujiunga.

Baada ya kuhoji uongozi wa shule wanasema kuwa bado hawajapata Waraka wa Serikali, hivyo tumetakiwa kulipa ada kawaida.

Tuiombe Serikali kupitia Wizara ya Elimu kulisimamia hili ili turejeshewe ada tuliyolipa ambayo serikali imeishaifuta.
Bajeti ya serikali inaamza Julai 1. Kwa sasa lipa
 
Mimi nadhani lingekuwa jambo jema serikali ingefuta michango yote ya mashuleni kama godoro, fagio ndoo nk halafu ikaacha ada, hilo ni wazo langu tu.
 
Neti godoro na fagio pia vilified na serikali naona kama hapatakuwa na uwajibikaji kwa wazazi na kwa wanafunzi pia wacha tulipie tu
 
Tuombe ufafanuzi kwa hili,

Baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha kutangaza kuwa kuanzia sasa hakutakuwepo ada kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2022/2023 sisi wazazi katika kumwandaa mtoto na mahitaji yake tumepambana na kipengele cha ada katika fomu za kujiunga.

Baada ya kuhoji uongozi wa shule wanasema kuwa bado hawajapata Waraka wa Serikali, hivyo tumetakiwa kulipa ada kawaida.

Tuiombe Serikali kupitia Wizara ya Elimu kulisimamia hili ili turejeshewe ada tuliyolipa ambayo serikali imeishaifuta.
Wakuu naomba kutoa ufafanuzi! Kuhusu kufuta ada lilikuwa ni pendekezo la waziri, hivyo bado hata badget haijapitishwa mpo? Acha na walimu wapige malundo
 
Ukisoma nyuzi kama hizi ndio unagundua uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo mepesi kwa watanzania wengi ni finyu sana

Alichokisema waziri ni mapendekezo ya bajeti mwaka wa fedha 2022/2023 ambao unaanza mwezi July.
Na hiyo itafanyika tu endapo bajeti hiyo na pendekezo hilo litaridhiwa na bunge kwa kuunga mkono bajeti.

Sasa Jiulize huyo mwanao umemlipia ada lini? Je ulipolipa ada na unavyoandika uzi huu ni mwaka wa fedha 2022/2023?
Yani ni sawa sawa na kuanza kudai mambo ya mbinguni wakati bado uko duniani hapo vingunguti
 
Back
Top Bottom