PAmBAnO LA nGUmI KAti yA "WEMA VS WOLPER" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PAmBAnO LA nGUmI KAti yA "WEMA VS WOLPER"

Discussion in 'Entertainment' started by bampami, Jul 6, 2012.

 1. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,849
  Likes Received: 1,288
  Trophy Points: 280
  Bondia Francis Cheka (katikati) akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchakaza mpinzani wake Japhet Kaseba. Wolper (kulia) akijitapa kuwa atamtwanga mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani). Kocha wa Wema, Rashid Matumla (wa tatu kushoto) akizungumza kwa niaba ya Wema (ambaye hakuwepo) kwenye mkutano huo. Nahodha wa Bongo Fleva, H Baba (kulia) akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na (kutoka kushoto) kocha wa bondia Francis Cheka (Abdalah Saleh Komando), Francis Cheka, meneja wa mfuko wa elimu (Charles
  Kapima), mmoja wa waratibu wa tamasha hilo (Luqman Maloto), promota wa pambano hilo, Kaike Silaju, bondia Japhet Kaseba na mwisho ni meneja wa Kaseba (Idd Bakari). Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo. WAKATI homa ya mapambano ya ndondi yanayosubiriwa kwa hamu kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba pamoja na wakali wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper, ikizidi kupanda, baadhi ya mabondia hao wametoa tambo kuwa watawachakaza
  wapinzani wao siku hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums jijini Dar, Jacqueline Wolper alitamba kumpiga vibaya mpinzani wake siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Matumaini pale Uwanja wa Taifa. “Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kuhusu mimi kwenye TV. “Nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga" alisema Wolper. Nae Bondia Francis Cheka alitamba kuwa kama kawaida yake atamchachafya mpinzani wake katika tamasha hilo.
  Source>Michuzijr
   
 2. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  NANI KAPIGWA WEMA vs WOLPER?
   
 3. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wametoka sare na wamepigana raundi mbili tu.Huu ndio mpambano wenye raundi ndogo kuwahi kutokea duniani.
   
 4. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  du ilikua comedy
   
 5. M

  Mundu JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Comedy at its peak...
   
 6. stineriga

  stineriga JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 2,033
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Du, pambano lilikuwa kumbe la raundi mbili tu!!
   
Loading...