Pambano la Mayweather vs. Logan

Jingine la kujifunza ni influence ya youtube na instagram ambayo kibongobongo tuna tabia ya kudharau. Nakumbuka posts za mwanzo kabisa za mayweather vs logan walitaja namba zao kwenye insta.
Yes, tunachukulia poa mitandao ya kijamii ila hao jamaa ukiambiwa mkwanja wanaopiga kupitia YouTube pekee unabaki kushangaa. Ndio maana namuheshimu sana Millard Ayo hapa bongo
 
60 Billion kwa ile exhibition?..ma.mae watu wanatengeza dola bhana
Kwa kukumbatiana Round 8 , unaambiwa Floyd siku moja kabla hajapanda ulingoni alikuwa ashaingiza $ 30 mil, baada ya pambano atakuwa kapiga mpunga mwingi maana hapo anajumlisha na mauzo ya PPV.
 
Iko hivi, hawa 'YouTubers' waliovamia kwenye boxing (Logan Paul,Jake Paul na KSI) wametokea kukamata headlines sana kutokana na majina yao kuwa makubwa kwenye social medias na wana mashabiki wengi hivyo wakiandaa mapambano yanauza sana, na kwavile boxing imepoteza mvuto promoters wanavutiwa kuwatumia hawa kumake easy money kuliko kutumia nguvu nyingi kupromote real boxers ambao hawana majina hivyo kupigwa hasara. Real boxing fans/Real boxers wengi wanachukia kuona hawa watu wanapata sportlight kubwa kuliko wapiganaji wa kweli ambao wamewekeza akili zao na nguvu kwenye huu mchezo kwa miaka mingi ila hawapewi sapoti kihivo, mmojawapo ni no1 p4p boxer CANELO ALVAREZ aliwahi kuongelea hii na kuonyesha kuchukizwa. Lakini kwa upande mwingine wachambuzi/wadau wengine wa ndondi wanasapoti uwepo wa hawa watu kwa vile wanatengeneza mashabiki wapya wa boxing hivyo kuifanya boxing kuwa alive (wanawavutia casual fans). Baada ya kueleza hivyo nijibu hoja yako ya why UFC fighters wanahamia kwenye boxing;

1. UFC fighters waliopigana kwenye boxing sio wengi kama unavyofikiria, mi ninaowakumbuka ni Conor McGregor aliyepigana na Mayweather, na Ben Askrem aliyepigana na Jake Paul miezi kadhaa iliyopita kama kuna wengine niliowasahau niambie

2. Boxing ina malipo mazuri zaidi ukiwa na jina kuliko UFC ambapo kina Dana White wanawakamua sana fighters wao kwa kigezo cha kuwapa promo. UFC ni wazuri kwenye branding, wamefanikiwa kutengeneza majina makubwa kwenye combart sports kwa miaka hii kuliko boxing ila shida wanawabana kwenye malipo, ukitaka kuamini hili angalia hata following kwenye social medias, UFC fighters wengi wenye majina makubwa wana following kubwa kuliko boxers

3. Ni rahisi UFC fighter (MMA) kwenda kucheza boxing kuliko boxer kwenda kucheza MMA kutokana na kwamba MMA fighter anajifunza vingi, boxing ni part ya Martial Arts. Ila boxer kwenda kwenye MMA itamchukua muda mwingi sana ili aweze kufanya ushindani, maana itabidi ajifunze kucheza mateke, grapping, wrestling, n.k. in short MMA is very close to streetfight. Boxer smart hawezi kukubali kwenda kuwa embarrassed kwenye ring ya Octagon, kuna boxer kadhaa walijaribu kufanya hivyo wakaishia kudharirishwa vibaya. Msearch James Toney utaelewa

4. Kwa hawa YouTubers wanapendelea kupigana na hawa UFC fighters kwa vile wanajua ni rahisi kuwapiga kwenye boxing ring, maana wana basics tu za boxing hawako deep sana huko. Jake Paul anatarajia kupigana na Retired UFC champion anaitwa Woodley hapo mwezi wa nane na watauza sana, maana Woodley ana jina kubwa na hana cha kupoteza, na Jake Paul now ni hotcake kushinda hata top boxing champions. If it makes dollars it makes sense, so hongera kwa Paul Brothers

Izi exhibition matches zina haribu boxing kama ilivo taka kuharibu mpira ile super league
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom