Palipotoboka panazidi kuvuja!

Ila hapo cov 19 ipo Tz ni propaganda ya kitoto sana
Sijui wanataka kutengeneza taharuki eti tusahau ya 29oct?
Not propaganda nakupa siku 90 kuanzia tangazo la covid 19 litoke utaniambia kitakacho tokea...!

Nikukumbushe tu pengine umesahau ni covid 19 iliyo pita na Dk. Kijazi...

Hiyo hiyo ndio ilipita na mzee Magufuli...

Ebu tuone hii ya sasa Itapita na kina nani na nani...!

Ni mwendo wa mnyukano ukizubaa UMEUAWA​
 
Propaganda hizo mkuu.
 
Ramli
 
Kwa hiyo ukiwa na mafua tu ni covid 19?
So this time unaanzia Tz halafu utasambaa dunia nzima?
 
Unadhani wanajali? Ilimradi wanaamka wanakunya wanakula wanajamba Kwao mwisho hiyo hawajui kingine chochote
 
Tukae mwendo wa kutulia wadau. Soga boy anatupambania kwa madili ya kimafia zaidi.
Si mnaelewa wahisani walishazingua na vijisenti vyao?
So by any means lazima tusonge wadau. Tulianzia Kongo kuteka madini tumefeli, tumejaribu na dili la mapouder limebauzi. Yaani mwaka wa shetani ni washetani tu wadau.
 
Kwamba hadi sisi Watumishi wa Mungu tutulie tu tusubiri hela za Mapouda. Mkuu tutake radhi aisee. Ai kanti brithi🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Damu isiyo na hatia huwa iandai. Tusijidanganye damu hata kama umeua mtu mmoja na ukaficha, no way ipo siku utaropoka tuu. Jaribu kufuatilia hata historia, hata kwenye jamii zetu. Yaani afadhali hata dhambi ya kuiba, lakini siyo kumwaga damu. Huwa natafakari sijui kuna siri gani katika damu na laiti viongozi tungejua hili. Nimeapa maisha yangu sitaimwaga damu isiyo na hatia bora nibaki na umaskini wangu kuliko damu isiyo na hatia
 
Utekaji ni sera ya taifa katika kuliponya Taifa letu.
Biashara ya ngada/unga ni mbadala wa kukosa pesa baada ya vikwazo vya mataifa mbalimbali.
Mama anatosha tukutane 2030.
 
 
Huwa natafakari sijui kuna siri gani katika damu na laiti viongozi tungejua hili. Nimeapa maisha yangu sitaimwaga damu isiyo na hatia bora nibaki na umaskini wangu kuliko damu isiyo na hatia
 
Marehemu awa shahidi😀🙌🏿🏃🏿
 
MAREHEMU KUWA SHAHIDI KESI YA LISSU?

Baada ya kuona mitandao habari, hii ikabidi pia nami nijiridhishe kwa kutembelea ukurasa wa Facebook wa Mkamiti Mohamedi! Ameandika maneno haya katika ukurasa wake:

"Huyu ndie Amin Said Mahamba ni marehemu mume wangu amefariki mwaka 2021 akiwa [ni] SACP sio ACP kama inavyotajwa kwenye kesi ya Tundu Lissu. Huyo wanayemtaja huko sijui ni yupi, mume wangu amefariki na cheti cha kifo kipo nimechoka kupigiwa simu kuulizwa. Kama Jamhuri inatumia jina la mume wangu nitawashitaki kabisa wala sitokaa kimya maumivu ninayoyapata Mungu ndiye anayejua. Naomba muacheni mume wangu apumzike kwa amani miaka aliyotumikia Jeshi la Polisi inatosha"!

Baada ya kusoma ujumbe huo nami nimeamua kujitia purukushani kuandika maneno haya:

1. Kwa mujibu wa Lissu, maelezo ya Mahamba yalisomwa wakati wa ukabidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

2. Jamhuri inataka kuongeza maelezo mengine ambayo hayakusomwa wakati wa ukabidhi pale Kisutu ili kuingiza masuala ya vurugu za tarehe 29 - 31 Oktoba 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

3. Kuna mahali nilisoma kuwa Jamhuri ilisema kuwa huyo Mahamba ni mpelelezi aliyekuwa akipeleleza matukio ya kabla, wakati na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025. Jambo ambalo pia limetafsiriwa na Lissu kuwa inataka kumtupia zigo la 'virugu na mauaji ya 29 Oktoba 2025'!

4. Mtu aliyetambulisha kama alikuwa mke wa Mahamba amejitokeza na kusema mume wake alifariki dunia. Hii inaleta tafsiri kuwa Jamhuri inatumia marehemu kama mashahidi dhidi ya Tundu Lissu.

5. Baadhi ya watu wanahoji pengine hiyo ndiyo sababu Jamhuri iliomba kuwaficha mashahidi wake.

6. Sasa huyo mama kuchoma kichaka kilificha chatu, chui na nyegere.

Mengine tunamuachia Lissu. Maana kitendo cha kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kuomba 'marehemu' atoe ushahidi kutakuwa kimeongeza changamoto mpya katika kesi za jinai katika mahakama zetu.

Nahitimisha kwa kuuliza maswali machache: Je, ulikuwa unamfahamu huyo Mahamba? Je, ni kweli alifariki? Alifariki lini na alizikwa wapi?
Je, ni mtu wa wapi? Je, ulihudhuria maziko ya Mahamba? Je, alifariki kwa ugonjwa au ajali? Je, alifia hospitali gani? Je, unamfahamu huyo aliyejitaja kama mke wake? Je, unawafahamu ndugu wengine au watoto wa Mahamba?

Kama kweli Mahamba ni marehemu, inajenga taswira gani kuhusu mashahidi wote wa kificho walioletwa napua watakaoletwa katika kesi ya Lissu? Je, hii inajenga taswira gani kwa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kuhusu uwezo wake na uwezo wa watumishi wa Ofisi yake yote? Je, hii inajenga taswira gani pia kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Idara yake yote?

Je, ni kweli Mahamba yuko hai lakini familia yake ilifichichwa na kupewa 'cheti feki' ya kuwa amefariki na wakazika 'kanyaboha' lakini yeye Mahamba anaendelea kuitumikia hii 'jamhuri'?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 28 Februari 2026; Saa 5:40 asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…