Palestina kufungua ubalozi vatican

chrissleon

Senior Member
Jul 22, 2015
147
89
Raisi wa Palestina akutana na Papa Francis Vatican city

_93568618_papafrancisnamahmoudabbas.jpg


Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akutana na papa Francis mjini Vatican


Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, anakutana na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis huko Vatican, kabla ya kufungua ubalozi wa Palestina huko.

Ubalozi huo unafunguliwa miaka minne baada ya Vatican kulitambua taifa la Palestina.

Bwana Abbas anatarajiwa kuzungumza na Papa kuhusu wasiwasi kuwa rais mteule wa Marekani Donald Trump anapanga kuhamisha ubalozi wa Marekani nchini Israel kutoka Tel Aviv, na kuupeleka Jerusalem jambo ambalo Wapalestina wanasema, litaharibu uwezekano wa kupata makubaliano ya amani kufuatia majadiliano na Israel.

Swala la Jerusalem ni miongoni mwa maswala yanayovutia hisia kali na tata katika mzozo wote wa mashariki ya kati.

Palestina inalichukulia eneo la mashariki mwa Jeusalem kuwa mji wake mkuu wa taifa lake siku za usoni lakini Israel inalichukuwa eneo hilo lote kuwa mji wake mkuu.

Siku ya Jumapili Ufaransa itaandaa mkutano wa kimataifa mjini Paris ili kujaribu kuanzisha mazungumzo ya amani katika ya pande hizo mbili.

BBC News.
 
Hiyo imekaa vizuri sana. Vatican ni nchi inayotambuliwa na mataifa duniani na UN hivyo mataifa na mamlaka mbalimbali zenye hadhi ya nchi kuwa na balozi zao Vatican na Vatican kuwa na balozi zake nchi mbalimbali ni sahihi kabisa. Sio wale wajinga wengine wanaojenga hoja za kijinga za kujiunga na OIC kwa kigezo cha Vatican. Hivi OIC ingalipo jamani? Haisikiki sana siku hizi kama ilivyokuwa enzi zile za "harkati" Gaddafi, Idd Amin, na wengineo.
 
Back
Top Bottom