Pale Prof. Shivji anapogongana na Ahmed Rajab

Pale Prof. Shivji anapogongana na Ahmed Rajab

Mzenji73

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
341
Reaction score
92
PROFESA Issa Shivji na mimi tumetoka mbali. Kwangu, yeye ni kama ndugu. Sote ni waumini wa falsafa ya umajumui wa Kiafrika na tunaitetea kwa nguvu hoja ya umuhimu wa kuungana kwa bara la Afrika.
Isitoshe sote tunaamini kwamba tunapoichambua jamii tunapaswa tuichambue kitabaka kwani kwa kufanya hivyo tu ndipo tunapoweza kuwatetea kwa haki wanyonge wa dunia hii.
Shivji, ambaye ni Mwenyekiti wa Wataalamu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na pia Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mtu mwenye kuheshimika ndani na nje ya nchi kwa michango yake ya kitaalamu. Ameandika mengi na kusema mengi kuhusu masuala ya kikatiba ikiwa ni pamoja na suala la Muungano wa Tanzania na uhalali wake.
Miaka kama minne iliyopita aliandika kitabu alichokiita ‘Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.’ Maudhui ya kitabu hicho yalikuwa ni kuangalia nini kilichochochea kuundwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mafunzo gani tunayoweza kujifunza kutokana na Muungano huo.
Wiki iliyopita Shivji alishiriki katika mjadala uliofanywa Dar es Salaam wa nafasi ya vyombo vya habari katika Muungano. Kwenye mjadala huo aliueleza kinaganaga msimamo wake juu ya Muungano. Kwa bahati mbaya gazeti moja nchini liliyapotosha aliyoyasema na kudai kwamba aliupinga Muungano. Taksiri hiyo ya uandishi ikampa Shivji fursa ya kuyakanya hayo na kuueleza tena msimamo wake katika makala aliyoandika katika hilo gazeti lililomnukuu sivyo.
Ama mimi nilishangazwa mno na aliyoyasema kwenye mjadala na aliyoandika kwenye makala. Nilishangazwa kwa sababu baadhi ya matamshi yake si matamshi ya kusemwa na mtu wa kipaje chake. Nilishangazwa pia kwa sababu msimamo wake wa juzi unanikanganya na sasa sijui ni upi msimamo wake halisi kuhusu Muungano — huu wa juzi au ule aliouainisha katika kitabu chake cha miaka minne iliyopita?
Hayo ya juzi yanakinzana na aliyoyaandika kitabuni alipokuwa anauchambua uhalali wa Muungano. Humo kitabuni aliandika kwamba lau Tanzania ingekuwa na mahakama huru basi Katiba ya Jamhuri ya Muungano ingefutwa kama hoja ya kufanya hivyo ingepelekwa mbele ya Mahakama hiyo.
Shivji alikuwa na sababu ya kuhoji hivyo na sababu yenyewe ni kuwa katiba hiyo ilianza kama katiba ya muda na ilifanywa na mtu mmoja yaani Rais wa Tanzania bila ya hata kumshirikisha Rais wa Zanzibar. Hiyo ndiyo hatimaye ikawa katiba ya kudumu kutoka mwaka 1977 ilipoidhinishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kinyume na utaratibu uliokubaliwa na Hati ya Muungano ya 1964.
Utaratibu uliokubaliwa ni kuwa katiba ya Tanganyika itatumika kuwa katiba ya muda kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba katiba ya kudumu itatungwa na Baraza Maalumu la Kutunga Katiba ambalo litapendekezwa na pande zote mbili za Muungano na ambalo litakuwa na idadi sawa ya wawakilishi wa Zanzibar na wa Tanganyika.
Kwa vile hilo halikutendwa na badala yake chama ndicho kilichotunga katiba ya Jamhuri ya Muungano labda ndiyo maana Shivji akasema kwenye kitabu chake ya kwamba Mahakama huru ingeifutilia mbali katiba ya sasa ya Tanzania. Hayo yanaingia akilini.
Kinachokanganya akili ni kumuona Shivji akiuvuka mstari wa kuwa mwanasheria, tena mwanasheria mahiri, na kujifanya msemaji wa wale wenye kuwatisha Wazanzibari. Ninasema anawatisha kwani amenukuliwa kuwa aliyasema yafuatayo mwenye mjadala wa wiki iliyopita: “Wazanzibari wengi wanafanya kazi na kufanya biashara Tanzania Bara, kwa hiyo wanaposema Muungano uvunjwe italeta athari kubwa sana kwa sababu itabidi wafukuzwe.”
Kwa nini itabidi wafukuzwe? Na hivi Shivji anakuwa anasema kwa niaba ya nani anapowatisha hivyo Wazanzibari kuwa ukivunjika Muungano watafilisiwa mali zao na kufukuzwa kutoka Bara?
Hapo kuna mambo mawili matatu ambayo Shivji anayasahau. Kwanza, anasahau kwamba siku hizi kuna utawala wa sheria katika sehemu zote mbili za Muungano: Tanzania Bara na Zanzibar.
Vilevile anasahau kwamba Watanganyika nao wana rasilimali zao nyingi Zanzibar. Kwa mfano, wao ndio wenye kuyamiliki takriban mabenki yote yaliyopo Zanzibar isipokuwa People’s Bank of Zanzibar.
Kadhalika, wanamiliki mengi ya mashirika ya bima na mabaa yalioko Zanzibar, mjini na mashambani. Kuna Wabara wanaohodhi biashara za utalii hasa katika Mji Mkongwe. Kuna waliopewa ekari tatu tatu za ardhi na serikali ya Zanzibar na kuna waliojaa katika mashamba na mjini na kuna Wabara wanaofanya kazi Zanzibar hasa katika sekta ya utalii na kuna mamia ya wafanya biashara wadogo wadogo kutoka Bara.
Shivji aliendelea kuwatisha Watanzania wote kwa kuandika kwenye makala yake ya wiki iliyopita kwamba: “Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo.”
Sijui kwa upande wa Watanganyika lakini kwa upande wa Wazanzibari dai la kutaka mfumo mbadala wa Muungano si dai la kuwabagua Watanganyika. Ni dai la kutaka kuuimarisha kidhati Muungano wa nchi zetu. Shivji hajitendei haki hata yeye mwenyewe pamoja na utaalamu wake anapoligeuza dai hilo na kulisingizia kuwa ni kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari.
Hali kadhalika, kauli yake kwamba Muungano umeleta tija ya kiuchumi kwa pande zote mbili na kwamba ukivunjika wananchi watateseka ni kauli ya kichekesho ukizitathmini hali zetu za kiuchumi na mfumo tulionao wa uchumi tegemezi.
Swali linalostahili kuulizwa ni: Je, wananchi wapi walionufaika na Muungano? Ni walala hoi walio wengi na wenye kazi pevu ya kujitafutia riziki au ni wafanyabiashara wachache na wale wanaopata natija kutokana na mfumo uliopo wa utawala?
Na wala si sahihi kusema kama asemavyo Shivji kwamba kuwapo kwa Muungano kumesaidia kuunganishwa kwa chumi za pande mbili za Muungano. Kwanza, hakutoa ushahidi wenye kuonyesha faida waliopata wengi wa wananchi wa Tanganyika na wa Zanzibar kutokana na kuwapo kwa Muungano katika kipindi cha miaka 48 iliyopita.
Pili, ukweli wa mambo ni kwamba uchumi wa Tanganyika na ule wa Zanzibar hazikuunganishwa ingawa kuna sarafu moja na mfumo mmoja wa utozaji kodi na ushuru.
Ukitembelea soko la Zanzibar utaona kwamba kuna bidhaa nyingi zitokazo China na hata Ghuba ya Arabuni kuliko bidhaa zitokazo Bara. Kwa upande wa Bara nako hakuna biashara ya maana inayofanywa kati yake na Zanzibar.
Takriban biashara ya pande mbili inahusisha biashara ya nje. Kwa mfano, kuku hapa Zanzibar wanatoka Brazil, maziwa yanatoka Arabuni, kahawa inatoka Brazil na Kenya na chai inatoka huko huko Kenya ingawa Tanzania Bara ni taifa lenye kusafirisha kahawa na chai.
Shivji anapendekeza ubadilishwe muundo wa uongozi kwa kuwekwa rais mmoja na waziri mkuu mmoja ambapo kati yao hao mmoja atakuwa anatoka Tanzania Bara na mwengine Zanzibar. Ni haki yake kupendekeza alivyopendekeza. Lakini ikiwa yeye ana haki ya kupendekeza hivyo kwa nini anawanyima wengine haki ya kupendekeza mfumo wa aina yoyote wa Muungano ikiwa wa katiba au wa mkataba, haki ambayo wanapewa Wazanzibari na katiba zote mbili za Tanzania na Zanzibar?
Watanzania wote wanahakikishiwa haki hiyo kwa mujibu wa sheria zinazohusika na mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya ya Tanzania na mwongozo uliotolewa na Jaji Joseph Warioba kwamba wananchi wana haki ya kutoa mapendekezo yoyote yale wayatakayo hata ikiwa ni ya kutaka Muungano uvunjwe. Sasa tumsikilize nani: Shivji au Warioba?
Kwa hakika wanaotaka Muungano wa Mkataba hawasemi kuwa wanataka kuuvunja Muungano. Wanachosema ni kuwa wanataka kuuimarisha na kuufanya uwe na maana kwa kuugeuza badala ya kuwa wa kikatiba na kuufanya uwe wa mkataba.
Wanachodai ni mfumo mbadala wa Muungano, mfumo ambao utakuwa kivutio cha kuzivutia nchi nyingine za Kiafrika zijiunge nao kwa moyo wa umajumui wa Kiafrika.
Kuhusu mada hii Shivji anakosea anapodai kwamba chama kimoja Zanzibar (anakusudia chama cha CUF) ‘kinapandikiza’ pendekezo la Muungano wa Mkataba. Huu ni upotoshaji wa ukweli. Misimamo rasmi ya vyote viwili vikuu Zanzibar inajulikana. CCM ina msimamo wa kutaka mfumo wa sasa wa serikali mbili uendelezwe ila ufanyiwe marekebisho; CUF ina msimamo wa kutaka pawepo serikali tatu.
Dai la kutaka Muungano wa Mkataba ni dai linalosukumwa na wananchi kwa jumla bila ya kujali misimamo ya vyama vyao na linaungwa mkono na hata baadhi ya viongozi wa vyama hivyo lakini si msimamo wa chama chochote hapa Zanzibar. Na wala si kweli kwamba wenye kuutetea Muungano wa Mkataba hawakueleza waziwazi maana yake. Wameeleza kwa kina.
Jingine la kushangaza alilosema Shivji ni kwamba wanaotaka Muungano wa mkataba wana ajenda ya siri. Lakini iweje ya siri ilhali zoezi zima la kuratibu maoni ya Wazanzibari na ya Watanganyika linaendelea kwa uwazi na utulivu?
Isitoshe si siri kwamba hadi sasa wengi wa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakitoa maoni ya kupendekeza mfumo mbadala wa Muungano wa kutaka pawe na Muungano wa mkataba baada ya kuona madhara yaliyoipata nchi yao hasa katika sekta za uchumi na ustawi wa kijamii.
Bila ya shaka kwa vile Shivji si Mzanzibari haishangazi kuona kuwa hana uchungu na Zanzibar. Lakini kwa vile anasifika kwa kipaje chake cha uchambuzi katika taaluma ihusiyo katiba tunamtarajia kwamba angalau ataendelea kulitendea haki suala hili kama ilivyokuwa tabia yake.
Ama mimi ninambembeleza Shivji alifanyie taamuli suala hili kwa kukisoma tena kitabu chake kwa makini. Lakini kwa namna alivyobadili maoni yake nachelea asije akageuka na kukirarua rarua kitabu chake mwenyewe.
 
Huyu pro ameanza kuzeeka ndiyo maana anajipinga mwenyewe. Halafu kama kweli hazungumzi kwa niaba ya watu ni nani kamwambia kwa serikali 3 Wazanzibari watafukuzwa? Hii haikupaswa kutoka kwa msomi kama yeye.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
prof. Shivji wako wangapi?

Yuko mmoja ila huyu Shivji wa sasa anapinga yale aliyoyaandika yeye mwenyewe wakati uliopita. Kwa hiyo ni Shivji anampinga Shivji.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Huyo shivji amewekeza tanganyika ana hofu na mali zake.
 
Naona hata Shivji anataka kuwa baba wa taifa eti baadaye tuseme aliona mbali, alishasema, n.k.
Sikupenda kabisa mawazo yake ya utabiri. Nadhani labda ameyumba kiuchumi sasa anaanza kupewa vijisenti na chama tawala ili akisemee. Yoote aliyosema ni ya\le ya akina Mwigulu, ya kupinga serikali 3.

Mbona alipoombwa aseme mfumo anaouna unafaa alikosa la kusema? Aende zake!
 
Andika vizuri basi kwa kupanga vizuri uzi wako ukizingatia aya ili kuvutia usomaji!
 
Huyu Prof Shivji bado ana U-Nyerere kuwa anachosema ndio kifuatwe Kama Mungu mtu
 
huyu hujifanya mungu mtu kila kitu ndio yeye tu uuuuuu mpumbavu sana shivji ni hovyoo
 
hiyo heading umeandika mwenyewe au umeandikiwa?rekebisha ikae mkao mzuri
 
Huyu Prof Shivji bado ana U-Nyerere kuwa anachosema ndio kifuatwe Kama Mungu mtu

Mkuu hayo ni Maoni yake nawewe na mimi kila mmoja anamaoni yake na wakati ukifika kilammoja wetu atapiga kura kwa mtazamo ataka ona anafaa .Tunatakiwa kuvilaumu vyombo vya habari ambavyo vinakuza kishabiki maoni ya baadhi ya watu na havitoi kwa usawa fursa ya kutangaza ,kutafiti,na kuripoti maoni ya wananchi wa kawaida.

Iwe serikali Tatu,Muungano wa Mkataba au Serikali Moja na Hata ikibidi kuvunja Muungano kama ndiyo uamuzi wa wananchi acha iwe hivyo. Muungano huu hakufanywa kwa utashi wa wananchi hivyo tuna haki na wajibu wakuhoji,kuamua na kubadili jambo lolote ambalo linaukakasi katika kuleta tija kwa mahusiano yetu.Hoja nyingi zinazotolewa za kuulinda na kuutetea Muungano kwa Sura yake ya sasa zinajikita katika kutetea nafasi za Viongozi na siyo maslahi ya uma wa watanzania.
 
Ahmed Rajab ni 'Mwanamkataba', ndio hawa ambao Shivji amewaongelea hapa chini kwenye mhadhara wake pale UDSM;

"Nilisema kwamba ninavyodhani mimi, masharti mengi ya Rasimu yalikuwa maamuzi ya maelewano kwa maana ya compromise na sio mwafaka kwa maana ya consensus. Baada ya uchambuzi wangu, ninadiriki kusema kwamba muundo wenyewe wa serikali tatu uliopendekezwa ni compromise kati ya wale waliosimamia serikali mbili na wale waliopigania muungano wa mkataba, kwa maneno sahihi, kuuvunja muungano. Wanaserikali mbili waliona afadhali kuwa na Muungano, hata kama ni wa serikali tatu, badala ya kuuachia uvunjike; wakajifariji kwa matumaini ya dhamira ya wananchi na nia ya viongozi. Wana-mkataba wakaona kuwa kwa wakati huu wakubali serikali tatu wakijua fika kwamba muundo wa serikali tatu hautadumu na vyovyote vile utavunjika. Nilisema pia kwamba compromise inazaa uamuzi legelege. Compromise juu ya muundo, kwa maoni yangu, imezaa muundo wa muungano legelege. Kuna maeneo mengi nimechambua na kudhihirisha kwamba yatazaa migogoro ambayo hatimaye inaweza kuuvunja Muungano. Kero za Muungano zitaendelea, safari hii kutoka pande zote mbili. Muungano ukivunjika hakuna mwananchi atakayenusurika, awe wa Tanganyika au wa Zanzibar" - Issa Shivji (2013), Ukurasa wa 37-38, ​
Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya: Mhadhara wa Kuaga Kigoda cha [Taaluma cha] Mwalimu [Nyerere Chuo Kikuu cha Dar es Salaam]
 
Hii imekaa vyema!!! Huyu Ahmed kweli ni mweledi, nitakuwa nasoma mada zake. Nachukizwa sana na baadhi ya watu ambao humu ndani ya forum hawapendi kupata ujumbe badala yake wanaanza sema ooh mbona uzi wako hauna para mara umekosea maneno?????? sawa ni vizuri kuwa makini lakini pia haijalishi maana ujumbe wa uzi ndio hasa lengo la mwandishi, hii sio barua ya mapenzi na sio lazima mtu atoe comment humu kama huna pitaaa!!!! Ok Ushauri wa bure kwa Mh. Prof. Shivji;- Namuaona mara kadhaa sasa anachemsha, nahisi amezeeka au la Ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka, tunamheshimu sana, apumzike. Awaachie vijana la sivyo atamaliza muda wake vibaya kwa kuharibu yoote mazuri alokwisha kufanya.
PROFESA Issa Shivji na mimi tumetoka mbali. Kwangu, yeye ni kama ndugu. Sote ni waumini wa falsafa ya umajumui wa Kiafrika na tunaitetea kwa nguvu hoja ya umuhimu wa kuungana kwa bara la Afrika. Isitoshe sote tunaamini kwamba tunapoichambua jamii tunapaswa tuichambue kitabaka kwani kwa kufanya hivyo tu ndipo tunapoweza kuwatetea kwa haki wanyonge wa dunia hii. Shivji, ambaye ni Mwenyekiti wa Wataalamu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na pia Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mtu mwenye kuheshimika ndani na nje ya nchi kwa michango yake ya kitaalamu. Ameandika mengi na kusema mengi kuhusu masuala ya kikatiba ikiwa ni pamoja na suala la Muungano wa Tanzania na uhalali wake. Miaka kama minne iliyopita aliandika kitabu alichokiita ‘Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.’ Maudhui ya kitabu hicho yalikuwa ni kuangalia nini kilichochochea kuundwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na mafunzo gani tunayoweza kujifunza kutokana na Muungano huo.Wiki iliyopita Shivji alishiriki katika mjadala uliofanywa Dar es Salaam wa nafasi ya vyombo vya habari katika Muungano. Kwenye mjadala huo aliueleza kinaganaga msimamo wake juu ya Muungano. Kwa bahati mbaya gazeti moja nchini liliyapotosha aliyoyasema na kudai kwamba aliupinga Muungano. Taksiri hiyo ya uandishi ikampa Shivji fursa ya kuyakanya hayo na kuueleza tena msimamo wake katika makala aliyoandika katika hilo gazeti lililomnukuu sivyo.Ama mimi nilishangazwa mno na aliyoyasema kwenye mjadala na aliyoandika kwenye makala. Nilishangazwa kwa sababu baadhi ya matamshi yake si matamshi ya kusemwa na mtu wa kipaje chake. Nilishangazwa pia kwa sababu msimamo wake wa juzi unanikanganya na sasa sijui ni upi msimamo wake halisi kuhusu Muungano — huu wa juzi au ule aliouainisha katika kitabu chake cha miaka minne iliyopita?Hayo ya juzi yanakinzana na aliyoyaandika kitabuni alipokuwa anauchambua uhalali wa Muungano. Humo kitabuni aliandika kwamba lau Tanzania ingekuwa na mahakama huru basi Katiba ya Jamhuri ya Muungano ingefutwa kama hoja ya kufanya hivyo ingepelekwa mbele ya Mahakama hiyo.Shivji alikuwa na sababu ya kuhoji hivyo na sababu yenyewe ni kuwa katiba hiyo ilianza kama katiba ya muda na ilifanywa na mtu mmoja yaani Rais wa Tanzania bila ya hata kumshirikisha Rais wa Zanzibar. Hiyo ndiyo hatimaye ikawa katiba ya kudumu kutoka mwaka 1977 ilipoidhinishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kinyume na utaratibu uliokubaliwa na Hati ya Muungano ya 1964. Utaratibu uliokubaliwa ni kuwa katiba ya Tanganyika itatumika kuwa katiba ya muda kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba katiba ya kudumu itatungwa na Baraza Maalumu la Kutunga Katiba ambalo litapendekezwa na pande zote mbili za Muungano na ambalo litakuwa na idadi sawa ya wawakilishi wa Zanzibar na wa Tanganyika.Kwa vile hilo halikutendwa na badala yake chama ndicho kilichotunga katiba ya Jamhuri ya Muungano labda ndiyo maana Shivji akasema kwenye kitabu chake ya kwamba Mahakama huru ingeifutilia mbali katiba ya sasa ya Tanzania. Hayo yanaingia akilini.Kinachokanganya akili ni kumuona Shivji akiuvuka mstari wa kuwa mwanasheria, tena mwanasheria mahiri, na kujifanya msemaji wa wale wenye kuwatisha Wazanzibari. Ninasema anawatisha kwani amenukuliwa kuwa aliyasema yafuatayo mwenye mjadala wa wiki iliyopita: “Wazanzibari wengi wanafanya kazi na kufanya biashara Tanzania Bara, kwa hiyo wanaposema Muungano uvunjwe italeta athari kubwa sana kwa sababu itabidi wafukuzwe.”Kwa nini itabidi wafukuzwe? Na hivi Shivji anakuwa anasema kwa niaba ya nani anapowatisha hivyo Wazanzibari kuwa ukivunjika Muungano watafilisiwa mali zao na kufukuzwa kutoka Bara?Hapo kuna mambo mawili matatu ambayo Shivji anayasahau. Kwanza, anasahau kwamba siku hizi kuna utawala wa sheria katika sehemu zote mbili za Muungano: Tanzania Bara na Zanzibar.Vilevile anasahau kwamba Watanganyika nao wana rasilimali zao nyingi Zanzibar. Kwa mfano, wao ndio wenye kuyamiliki takriban mabenki yote yaliyopo Zanzibar isipokuwa People’s Bank of Zanzibar. Kadhalika, wanamiliki mengi ya mashirika ya bima na mabaa yalioko Zanzibar, mjini na mashambani. Kuna Wabara wanaohodhi biashara za utalii hasa katika Mji Mkongwe. Kuna waliopewa ekari tatu tatu za ardhi na serikali ya Zanzibar na kuna waliojaa katika mashamba na mjini na kuna Wabara wanaofanya kazi Zanzibar hasa katika sekta ya utalii na kuna mamia ya wafanya biashara wadogo wadogo kutoka Bara.Shivji aliendelea kuwatisha Watanzania wote kwa kuandika kwenye makala yake ya wiki iliyopita kwamba: “Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo.” Sijui kwa upande wa Watanganyika lakini kwa upande wa Wazanzibari dai la kutaka mfumo mbadala wa Muungano si dai la kuwabagua Watanganyika. Ni dai la kutaka kuuimarisha kidhati Muungano wa nchi zetu. Shivji hajitendei haki hata yeye mwenyewe pamoja na utaalamu wake anapoligeuza dai hilo na kulisingizia kuwa ni kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari.Hali kadhalika, kauli yake kwamba Muungano umeleta tija ya kiuchumi kwa pande zote mbili na kwamba ukivunjika wananchi watateseka ni kauli ya kichekesho ukizitathmini hali zetu za kiuchumi na mfumo tulionao wa uchumi tegemezi.Swali linalostahili kuulizwa ni: Je, wananchi wapi walionufaika na Muungano? Ni walala hoi walio wengi na wenye kazi pevu ya kujitafutia riziki au ni wafanyabiashara wachache na wale wanaopata natija kutokana na mfumo uliopo wa utawala?Na wala si sahihi kusema kama asemavyo Shivji kwamba kuwapo kwa Muungano kumesaidia kuunganishwa kwa chumi za pande mbili za Muungano. Kwanza, hakutoa ushahidi wenye kuonyesha faida waliopata wengi wa wananchi wa Tanganyika na wa Zanzibar kutokana na kuwapo kwa Muungano katika kipindi cha miaka 48 iliyopita. Pili, ukweli wa mambo ni kwamba uchumi wa Tanganyika na ule wa Zanzibar hazikuunganishwa ingawa kuna sarafu moja na mfumo mmoja wa utozaji kodi na ushuru. Ukitembelea soko la Zanzibar utaona kwamba kuna bidhaa nyingi zitokazo China na hata Ghuba ya Arabuni kuliko bidhaa zitokazo Bara. Kwa upande wa Bara nako hakuna biashara ya maana inayofanywa kati yake na Zanzibar.Takriban biashara ya pande mbili inahusisha biashara ya nje. Kwa mfano, kuku hapa Zanzibar wanatoka Brazil, maziwa yanatoka Arabuni, kahawa inatoka Brazil na Kenya na chai inatoka huko huko Kenya ingawa Tanzania Bara ni taifa lenye kusafirisha kahawa na chai.Shivji anapendekeza ubadilishwe muundo wa uongozi kwa kuwekwa rais mmoja na waziri mkuu mmoja ambapo kati yao hao mmoja atakuwa anatoka Tanzania Bara na mwengine Zanzibar. Ni haki yake kupendekeza alivyopendekeza. Lakini ikiwa yeye ana haki ya kupendekeza hivyo kwa nini anawanyima wengine haki ya kupendekeza mfumo wa aina yoyote wa Muungano ikiwa wa katiba au wa mkataba, haki ambayo wanapewa Wazanzibari na katiba zote mbili za Tanzania na Zanzibar?Watanzania wote wanahakikishiwa haki hiyo kwa mujibu wa sheria zinazohusika na mchakato mzima wa kutafuta katiba mpya ya Tanzania na mwongozo uliotolewa na Jaji Joseph Warioba kwamba wananchi wana haki ya kutoa mapendekezo yoyote yale wayatakayo hata ikiwa ni ya kutaka Muungano uvunjwe. Sasa tumsikilize nani: Shivji au Warioba?Kwa hakika wanaotaka Muungano wa Mkataba hawasemi kuwa wanataka kuuvunja Muungano. Wanachosema ni kuwa wanataka kuuimarisha na kuufanya uwe na maana kwa kuugeuza badala ya kuwa wa kikatiba na kuufanya uwe wa mkataba. Wanachodai ni mfumo mbadala wa Muungano, mfumo ambao utakuwa kivutio cha kuzivutia nchi nyingine za Kiafrika zijiunge nao kwa moyo wa umajumui wa Kiafrika. Kuhusu mada hii Shivji anakosea anapodai kwamba chama kimoja Zanzibar (anakusudia chama cha CUF) ‘kinapandikiza’ pendekezo la Muungano wa Mkataba. Huu ni upotoshaji wa ukweli. Misimamo rasmi ya vyote viwili vikuu Zanzibar inajulikana. CCM ina msimamo wa kutaka mfumo wa sasa wa serikali mbili uendelezwe ila ufanyiwe marekebisho; CUF ina msimamo wa kutaka pawepo serikali tatu.Dai la kutaka Muungano wa Mkataba ni dai linalosukumwa na wananchi kwa jumla bila ya kujali misimamo ya vyama vyao na linaungwa mkono na hata baadhi ya viongozi wa vyama hivyo lakini si msimamo wa chama chochote hapa Zanzibar. Na wala si kweli kwamba wenye kuutetea Muungano wa Mkataba hawakueleza waziwazi maana yake. Wameeleza kwa kina.Jingine la kushangaza alilosema Shivji ni kwamba wanaotaka Muungano wa mkataba wana ajenda ya siri. Lakini iweje ya siri ilhali zoezi zima la kuratibu maoni ya Wazanzibari na ya Watanganyika linaendelea kwa uwazi na utulivu?Isitoshe si siri kwamba hadi sasa wengi wa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakitoa maoni ya kupendekeza mfumo mbadala wa Muungano wa kutaka pawe na Muungano wa mkataba baada ya kuona madhara yaliyoipata nchi yao hasa katika sekta za uchumi na ustawi wa kijamii.Bila ya shaka kwa vile Shivji si Mzanzibari haishangazi kuona kuwa hana uchungu na Zanzibar. Lakini kwa vile anasifika kwa kipaje chake cha uchambuzi katika taaluma ihusiyo katiba tunamtarajia kwamba angalau ataendelea kulitendea haki suala hili kama ilivyokuwa tabia yake.Ama mimi ninambembeleza Shivji alifanyie taamuli suala hili kwa kukisoma tena kitabu chake kwa makini. Lakini kwa namna alivyobadili maoni yake nachelea asije akageuka na kukirarua rarua kitabu chake mwenyewe.
 
KUNA JAMAA ALIKUWA ANATUMIA JINA LA mCHAMBUZI ALIKUWA ANADADAVUA MAMBO KAMA HAYA SIJUI SIKU HIZI KAPOTELEA WAPI
 
Andika vizuri basi kwa kupanga vizuri uzi wako ukizingatia aya ili kuvutia usomaji!
"nakubali mkuu, ila nimegundua kitu kimoja, nafikiria tatizo lipo kwenye huu ukurasa wa kuandikia wa jamiiforums, sijui wenzangu mmegundua?"
 
Ahmed Rajab amejaribu kuonesha namna gani Prof. Shivji alivyo kigeugeu katika makala yake mwenyewe aliyoandika, hotuba yake pale Nkrumah Hall, na kwenye kitabu chake, jinsi mawazo yake yanavyopingana na mengine.

Sasa ili uelewe msingi wa madai ya Ahmed Rajab katika makala yake, ni vema kwanza ukasoma hicho kitabu cha Prof. Shivji Pan-Africanism or Pragmatism?
Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union
, makala yake katika hilo gazeti alioandika na kuipitia hotuba yote ya pale Nkrumah.

Ukianisha yote, utafahamu ukigeugeu wa Prof. Shivji!
 
hiyo heading umeandika mwenyewe au umeandikiwa?rekebisha ikae mkao mzuri
mkuu heading ni "Pale Prof. Shivji anapogongana na Prof. Shivji ........... na Ahmed Rajab" nashangaa unosemea wewe imeingiaje!
 
mkuu heading ni "Pale Prof. Shivji anapogongana na Prof. Shivji ........... na Ahmed Rajab" nashangaa unosemea wewe imeingiaje!

Nadhani Mods watakua wame-hariri!
 
Back
Top Bottom