Pale Pesa inapozidi vipaji

Pale Pesa inapozidi vipaji

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,074
Ndio, hakuna namna nyingine unayoweza kuelezea soka la sasa zaidi ya hii, Ni katika kipindi hichi ambapo inawezekana kumuona Luke Shaw akiwa na miaka 19 tu akiuzwa kwa zaidi ya paundi 25, zaidi ya bilioni 68 za kitanzania, kama hiyo haitoshi anaweka kibindoni zaidi ya paundi laki moja kila wiki, nilikuwa nikimwambia mshkaji wangu mmoja kuhusu hili nalolisema hapa akanibishia sana, akasema ni sababu ya uingereza wake, kuna ukweli kuhusu hilo lakini vipi kuhusu Lukas Moura? naye huyu ni mwingereza? vipi kuhusu David Luiz na paundi milioni 50 zake?

Nakubaliana na ukweli kwamba maisha yamepanda bei na kila kitu kimeongezeka thamani tofauti na miaka 15 au 20 iliyopita lakini kwa hili naona sio sawa, ni upungufu wa vipaji vya soka tofauti na miaka iliyopita.

Unawezaje kumnunua golikipa sasa kwa paundi milioni 25? ungemnunua shilingi ngapi Oliver Kahn? Je ungehitajika kutoa shilingi ngapi kwa Claudio Taffareli au Peter Schumichel? Kama tunaweza kumnunua Joao Moutinho kwa zaidi ya paundi milioni 30, umewahi kufikiri ungehitaji kuwa na kiasi gani kuipata huduma ya maestro Clarence Seerdorf au Andrea Pirlo wa miaka 25.

Hapa ndipo napokuja kugundua tunawaonea fifa na uefa bure kwenye utoaji wa tuzo, ni katika kipindi hichi ambapo nominees wa fifa ballorn d or ukiacha Messi na Ronaldo (robben, Iniesta, Muller,? kwa nini Ronaldo na Messi wasiendelee kujizolea tuzo? nakuhakikishia wasingeweza kufanya hivi miaka 15 au 20 iliyopita, wangewezaje?

utahitaji mwaka mzima kuniaminisha wangeweza, ni maajabu ngoja nikuonyeshe kitu, Seerdorf, Shevchenko na Pirlo wako na Milan, Raul, Ronaldo phenomenon, Figo, Zizzou wanakipiga na madrid ni katika dunia hiyo hiyo pia wanacheza chogo Thierry HEnry, Oliver Kahn, David beckham na Michael Owen, nani hapa angekuruhusu uchukue ballorn d or mara 4 mfululizo? Messi angeweza kufunga magoli 91 kwa mwaka mmoja tu lakini nani angeruhusu barcelona kushinda mataji mawili ya ulaya ndani ya miaka 4 na kuingia fainali watakavyo, kumbuka ni katika kipindi hicho ambapo AC milan na JUve walikuwa hawakamatiki kutoka Seria A, Liverpool na man u kutoka premier league, bayern wa bundesliga, madrid na barcelona wa la liga, ni katika kipindi hiki Ajax amsterdam na wakina Nottigham forest walikuwa wanapiga mbungi hadi wanawakalisha vigogo na kuchukua vikombe vya ulaya.

Hakika vipaji vilikuwa vingi mno ila pesa haikuwepo, vijana chezeni soka, hela kwenye kandanda ni nyingi na vipaji ni vichache mno, Je unajua Yanga walimlipa Emanuel Okwi milioni 90 na hakuwafungia zaidi ya goli tano wala kucheza zaidi ya mwaka, sasa kwa nini usicheze mpira.......kwa makala nyingine za kisoka tembelea sokaupdates.blogspot.com
 
Ndio, hakuna namna nyingine unayoweza kuelezea soka la sasa zaidi ya hii, Ni katika kipindi hichi ambapo inawezekana kumuona Luke Shaw akiwa na miaka 19 tu akiuzwa kwa zaidi ya paundi 25, zaidi ya bilioni 68 za kitanzania, kama hiyo haitoshi anaweka kibindoni zaidi ya paundi laki moja kila wiki, nilikuwa nikimwambia mshkaji wangu mmoja kuhusu hili nalolisema hapa akanibishia sana, akasema ni sababu ya uingereza wake, kuna ukweli kuhusu hilo lakini vipi kuhusu Lukas Moura? naye huyu ni mwingereza? vipi kuhusu David Luiz na paundi milioni 50 zake? Nakubaliana na ukweli kwamba maisha yamepanda bei na kila kitu kimeongezeka thamani tofauti na miaka 15 au 20 iliyopita lakini kwa hili naona sio sawa, ni upungufu wa vipaji vya soka tofauti na miaka iliyopita.

Unawezaje kumnunua golikipa sasa kwa paundi milioni 25? ungemnunua shilingi ngapi Oliver Kahn? Je ungehitajika kutoa shilingi ngapi kwa Claudio Taffareli au Peter Schumichel? Kama tunaweza kumnunua Joao Moutinho kwa zaidi ya paundi milioni 30, umewahi kufikiri ungehitaji kuwa na kiasi gani kuipata huduma ya maestro Clarence Seerdorf au Andrea Pirlo wa miaka 25.

Hapa ndipo napokuja kugundua tunawaonea fifa na uefa bure kwenye utoaji wa tuzo, ni katika kipindi hichi ambapo nominees wa fifa ballorn d or ukiacha Messi na Ronaldo (robben, Iniesta, Muller,? kwa nini Ronaldo na Messi wasiendelee kujizolea tuzo? nakuhakikishia wasingeweza kufanya hivi miaka 15 au 20 iliyopita, wangewezaje? utahitaji mwaka mzima kuniaminisha wangeweza, ni maajabu ngoja nikuonyeshe kitu, Seerdorf, Shevchenko na Pirlo wako na Milan, Raul, Ronaldo phenomenon, Figo, Zizzou wanakipiga na madrid ni katika dunia hiyo hiyo pia wanacheza chogo Thierry HEnry, Oliver Kahn, David beckham na Michael Owen, nani hapa angekuruhusu uchukue ballorn d or mara 4 mfululizo? Messi angeweza kufunga magoli 91 kwa mwaka mmoja tu lakini nani angeruhusu barcelona kushinda mataji mawili ya ulaya ndani ya miaka 4 na kuingia fainali watakavyo, kumbuka ni katika kipindi hicho ambapo AC milan na JUve walikuwa hawakamatiki kutoka Seria A, Liverpool na man u kutoka premier league, bayern wa bundesliga, madrid na barcelona wa la liga, ni katika kipindi hiki Ajax amsterdam na wakina Nottigham forest walikuwa wanapiga mbungi hadi wanawakalisha vigogo na kuchukua vikombe vya ulaya.

Hakika vipaji vilikuwa vingi mno ila pesa haikuwepo, vijana chezeni soka, hela kwenye kandanda ni nyingi na vipaji ni vichache mno, Je unajua Yanga walimlipa Emanuel Okwi milioni 90 na hakuwafungia zaidi ya goli tano wala kucheza zaidi ya mwaka, sasa kwa nini usicheze mpira.......kwa makala nyingine za kisoka tembelea sokaupdates.blogspot.com
En nino wadau watakaa kimya lakini uliyoyasema yanaukweli !vipaji vimeadimika na timu zinanyang'anyang'ana wachache waliopo! aha mpira unazidi kupendwa huku ukizidi kufa!hivi sasa kila mtu ni mtabiri unajua kabisa kuwa leo fulani atafungwa au timu fulani kwa kuwa fulani hayupo basi ni kichapo tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom