Pale Bunge linapokuwa genge la wahuni.

Pale Bunge linapokuwa genge la wahuni.

Antony Fereji

Member
Joined
Sep 29, 2016
Posts
46
Reaction score
63
Huwa nakereka sana pale mbunge, tena mtu mzima badala kuongelea musuala ya msingi, anaanza kuongea masuala binafsi, mipasho, na majungu.

Mfano, mtu anakurupuka, "Mh naibu spika tutoe ile sanamu Posta tuweke ya Diamond". Haya nimatope au akili?

Tabia nyingine chafu, utakuta mtu anasimama, " Mh naibu spika, mke wangu ni mvumilivu sana, alizaa mtoto wa kwanza akafa, akazaa wapili akafa, huyu watatu nitampa jina lako" (nge nge nge) wabunge wakigonga meza utafikiri hoja ya muhimu. Mtu kama huyu si angekwenda kwenye kituo cha redio akatoe historia yake? Sio bungeni.

Kuna tabia ya wabunge wa "ndiooooo", hawa huwa hawaonekani kabisa, lakini linapokuja suala linalohusu kupitisha masuala muhimu ya taifa utasikia " ndiooo". Huu ni umbea, ni ukasuku.

Saizi hata wasomi waliopo bungeni wameweka usomi wao pembeni wamejawa na umbea tu. Watu tumewaamini, badala yakujadili mambo ya msingi, yanaanza kufanya mipasho, shit!!
 
Hivi zile milioni kumikumi walizogawana walizitoa wapi....huenda ikawa ndo zile pesa zetu za rambirambi tulizochanga
 
Serukamba huwa hana wazo jipya hata siku moja,yeye huvizia wapinzani watoe hoja ili apinge
Maji Marefu anamzidi sana busara hata kama elimu yake ndogo
 
10 m sio nchezo, zimewatoa ufahamu wote wa upande ule wamekuwa kama propesa li pumb
 
Back
Top Bottom