paksat 1R @38'E na amos 5 @ 17'E

paksat 1R @38'E na amos 5 @ 17'E

nictbb

Senior Member
Joined
May 18, 2012
Posts
119
Reaction score
9
Wandugu,nna madish 2ya ft 6,na receiver ya strong 4653x,nataka kuset satellite hizo hapo,naanzaje?mi najua tu dstv ipo 36'E,na hiyo paksat iko karibu yake au?na vp kuhusu amos 5,nani amewahi kuipata au kuitumia?maji yamezid unga na mimi nna ham ya ugali sitaki uji jamani
 
Mmmh!! Kaka hapo katika Paksat hata mi mwenyewe shaa wai kukomaa saana kupata chaneli hizo,maana pande za huku kwetu wapo wawekezaji wakipakistani ili nilichemka na ukiona hata beam katika Paksat 38 E ni C-band ambayo inaturuhusu hata Tanzania kupata chaneli hizo,hata katika Map coverage na Tanzania ipo katika shadow.Ila komaa utanipa matokeo maana hata mi bado sijaikatia tamaa kabisa tarudia tena.

Toka Burton sat shop.
 
sawa kaka,tuko pamoja sana tu,satellite nyingine zp umewahi kujaribu ukafanikiwa kaka?
 
Ni nyingi ila mbali ya zilizopakana na Intelsat 906 at 64.2 'E ni Thaicom 5 at 78.5 'E,Intelsat 10A at 10'E,Astra 4A at 4.0'E,SES 5,Arabsat 5C at 20'E na nyingine ila nyingi zinanizingua ambazo zina chaneli nzuri saana kwa mapenzi yangu na wateja wangu.

Toka Burton sat shop.
 
Wandugu,nna madish 2ya ft 6,na receiver ya strong 4653x,nataka kuset satellite hizo hapo,naanzaje?mi najua tu dstv ipo 36'E,na hiyo paksat iko karibu yake au?na vp kuhusu amos 5,nani amewahi kuipata au kuitumia?maji yamezid unga na mimi nna ham ya ugali sitaki uji jamani

Kwanza mkuu tuanze na 38°E — Paksat 1 C-band R ...cha msingi ni wewe uko wapi kwa Tanzania,kwa mfano kama uko Tanga basi dishi lako lielekeze straght upande wa kaskazini..then settings yako ya ELEVATION ANGLE ni 84.6 na LNB TILT (Dish size =210cm)

36°E — Eutelsat 36A Ku-band ambayo umeiita Dstv....hii vipimo vyake ni ELEVATION ANGLE 82.5° na LNB TILT 24.7°(Dish size = 85 cm)
dishi lako linakuwa kushoto kidogo kwa sababu iko karibu sana na Paksat 1 kama ukiweza kupata Standard C/KU Band LNB 13K (lnb hii ni mbili kwa moja)nadhani kwa position ya Paksat unaweza kupata 36°E — Eutelsat 36A

17°E — Amos 5 Ku-band Dish lako inabidi ulielekeze Northwest...ELEVATION ANGLE ni 63.8° ....LNB Tilt 74.6° (Dish size ni 110cm)

NB: Muhimu sana utapoweka dish lako siku zote tumia Plumb na hakikisha una drill sehemu itengenezee zege na tumia carpenter's level kuhakikisha plumb yako iko sawa na kama utaweza kupata compass itakusaidia sana.
 
kaka hongera,hiyo thaicom uliipata kwa kutumia dish la ukubwa gani kaka?mi nko dar,na eutelsat 10 dish yake saiz gani kaka
 
nimekupata kaka,ila unapozungumzia lnb tilt,hapo ndo umeniacha mbali sana kaka
 
kumbe ni mvumilivu mwenzangu,haya kaka,watumia dish la ukubwa gani kupat thaicom kaka?vp kwa bayern tutatoka kaka
 
Kama unaitaka amos 5 at 17e ni vizuri ungezitaja chanel unazozitaka kwa sababu kuna za C band kwa mfano muvi tv, muvi tv afrika (zambia) na optima sport na za KU band kama Etv, oromia tv (Ethiopia), family tv 1,2 na nyingine nyingi. Ila kwa ushauri wangu KU band ndio nzuri, na unatakiwa uwe na dish la ku (offset dish) la cm 90 na kuendelea kwa sababu utapata signal ya eutelsat at 16E ambayo nayo kama utakuwa na reciever ya MPEG 4 utapata chanel nyingi sana zaidi ya 100.
 
nimekupata kaka,ila unapozungumzia lnb tilt,hapo ndo umeniacha mbali sana kaka

Mkuu pale unafunga lnb inatakiwa kuwa sawasawa ambapo inakuwa 0° na ndio maana nikakushauri utumie campass au ikiwa lazima tumia saa......simama nyuma ya Dish lako ukizungusha LNB kushoto ni - kulia ni +...tazama mfano huu

LNBF%20SKEW%20GUIDE.gif


fastsatfinder_dish_alignment_module.png
 
kaka,mi naitaka optima sports,nlisikia yaonyesha premier,na ptv katika paksat ir nayo nasikia yaonyesha premier,sasa hapa kuna kitu sijaelewa,paksat 1r nayo dish yake yatazama juu kama dstv au?maana iko karibu na dstv kwa angle,maana kuna siku nliona fund ametumia 6ft kupatia dstv,likawa limetazama juu sana,swali lingine,angle 17e naipatia wap,kulia kwa dish la mbc la engle saba au?
 
Kama mbc ya 7e umeshawahi kuipata nirahisi sama kupata amos 5 inabidi dish lako liinuke juu kama nyuzi 10' tu.
 
kaka,mi naitaka optima sports,nlisikia yaonyesha premier,na ptv katika paksat ir nayo nasikia yaonyesha premier,sasa hapa kuna kitu sijaelewa,paksat 1r nayo dish yake yatazama juu kama dstv au?maana iko karibu na dstv kwa angle,maana kuna siku nliona fund ametumia 6ft kupatia dstv,likawa limetazama juu sana,swali lingine,angle 17e naipatia wap,kulia kwa dish la mbc la engle saba au?

Mkuu soma vizuri post #6 majibu yako karibu yote yapo hapo,labda nikuongezee kidogo ukizingatia vipimo nilivyo andika hapo juu basi Dish linakuwa sehemu yake na kwa jinsi satelite zilipo kwa mtu wa Tanzania Dish linaelekea juu kwa kuwa satelite zipo juu yetu ila mbele kidogo na jinsi ya kupata engles kuna Uzi aliuanzisha Arselona ngoja nikupe link utafaidika kwa mengi,nakumbuka niliwahi post jinsi gani unaweza kupata kufika mfano unataka kwenda 17°E.

https://www.jamiiforums.com/tech-ga...um/274391-ulimwengu-wa-fta-sattelite-tvs.html

Soma post #147
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom