Paka wengine si mchezo.

KOKUTONA

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2011
Posts
8,651
Reaction score
6,110
Jamaa mmoja alimchukua paka wake na kwenda kumtupa mbali, ailiporudi nyumbani alimkuta paka amekwisharudi.

Jamaa alikasirika sana! Siku ya pili akamchukua na kwenda naye zaidi ya kilometa 50, akapita chochoro za kutosha kisha akamtupa akaanza safari ya kurudi nyumbani, baada ya muda akampigia simu mkewe..."Vipi mke wangu huyo paka yupo?"

Mke akajibu, Ndiyo mume wangu yuko hapa tena ametulia imekuaje? Jamaa: hebu mpe simu anielekeze njia!
 
Mmmh ndo maana sipendi kabisa hawo wadudu wana mambo ya ajabu.
 
Hata ukrukrudia tena hk kituko kesho lazma nicheke,my fvrt
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…