Nimeamka majira ya saa kumi usiku nikatoka nje.
Wakati nafungua mlango,nimekutana na paka mweusi mwenye madoa kama ya chui.
Sio mara yakwanza nakutana na huyu paka,mara yakwanza nimekutana nae maeneo tofauti kabisa nakwangu pindi natoka kazini majira ya saa 7 usiku.
Nikachukulia poa.Chakushangaza usiku huu nilipofungua mlango,paka huyu hakustuka ila alinikazia macho makali yakung'aa nami nikamkazia macho,mwili wangu ulisisimka,nikahisi sio paka wa kawaida,sikujaribu kufanya lolote ila kumtazama tu kwa takribani dakika moja naye akageuka taratibu nakuondoka,nikamfatilia mpaka alipopata upenyo ukutani akapanda akaondoka.
Mimi nimejaa uwoga kwan,siku zote nawaona hawa mapaka wala sitaharuki,ni leo tu,nashangaa kuona leo mwili wangu umesisimka kupita maelezo nilipomwona huyu paka.Nahisi ni kitu cha ajabu wala sio paka wakawaida.
Naombeni mnijuze ni kitu gani hasa nilichokiona,coz sina raha kabisa.