Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

Kuna kipindi niliona rais wa Ireland anahojiwa nje ya nyumba yake uwanjani anakocheza na mbwa. Rais yuko anahutubia mbwa yuko anamvuta anamuonesha mpira ili wacheze, rais hakumfukuza wala kukerwa na raia walipenda.

Raia wanajua yule mbwa wa rais wao ana wivu hata wakija wageni wa kimataifa hapendi wapewe attention zaidi yake. Anataka yeye ndio awe karibu na rais. Wazungu wanaamini ukipendwa na wanyama unakuwa na roho nzuri. Huwezi kuwa unapiga mawe mbwa ukawa na utu. Humanity inaakisiwa kwa unavyowatreat wanyama
Acha mawe tu mi nawabutuaga Paka kwa Sana tu yaani Ile Kinyama.Na Nina utu kishenzi kwny mambo ya msingi lkn sio utu wa kubebishana na wanyama wakuda Kama Paka kisa tu wazungu wanaamini nikipendwa na wanyama nakua na roho nzuri automatically.
 
Acha mawe tu mi nawabutuaga Paka kwa Sana tu yaani Ile Kinyama.Na Nina utu kishenzi kwny mambo ya msingi lkn sio utu wa kubebishana na wanyama wakuda Kama Paka kisa tu wazungu wanaamini nikipendwa na wanyama nakua na roho nzuri automatically.
Nenda hospital Kacheki kichwa mapema
 
Paka! Ni mnafki sana.

Paka anatumika hata na viumbe visivyoonekana kwa macho.

Nakumbuka kuna tajiri mmoja ( sitamtaja ) ana paka na kuku pale kwenye Yard yake masaki.

Huyo paka kwanza ni mkubwa ki umbo, yaani, yule mpuuzi ana Sofa lake na ana kitanda chake, yule paka amewekewa mfanyakazi.

Jengo ni kubwa sana na Tajiri haishi pale bali pale ana ofisi ndogo mle ndani. Wanaoishi pale ni huyo paka, kuku, njiwa na mfanyakazi.

Maisha ya mule ndani ( Boss Paka ) ukiingia kuna Sofa moja kubwa sana la langi ya dhahabu( sofa hili ni la huyo paka, ole wako ukaenda kukaa atakukata jicho hilo alafu haogopi yaan atawaka apo mpaka utainuka, jikoni yamejaa makopo ya chakula chake na cha kuku. Yaani yule paka ( sijui mm mpaka leo siamini kama kuna paka anayeishi kitajiri kama yule mpuuzi na kwanza mpaka hapa siamini kama ni paka ama Power Bank ya yule Tajiri wa mabasi.


Saa asubuhi anakula Samaki wa mchemsho, mchana kuna mavyakula wanachanganya ni vya kopo na maziwa.

Jioni saa kumi, anakula tena Nyama choma na maziwa, kisha anaenda zake kulala chumbani kwake, paka ni kauzu sana kauzu kupitiliza yaani hataki mgeni mle ndani ana jicho baya kinyama yaani mkiangaliana tu unajua huyu hafurahishwi na ujio wangu.

Saa kumi hiyo pia ni Muda wa kuku na njiwa kula.

Hawa wanapewa mikate 10, mbegu za bangi na mtama..huu mtama ni kilo 5. Kila siku..lakini hii si kesi kesi ipo pale kwa Paka Paka ana roho mbaya sana, nilijaribu kudodosa yule mfanyakazi anasema yule paka kwa sikuanatumia 40 kwenye chakula...


Kwa anayemjua Boss yoyote mwenye mabus ambaye ofisi yake ipo Masaki na Profile yake ktk whatsapp kaweka picha ya Boonge la Paka kuubwa, basi ajue huyo paka anakula elfu 40 kwa Siku, kila siku namaanisha. *****
 
Ninavyompenda,
FB_IMG_16334558012524924~2.jpg
 
Uchoyo na roho mbaya vinakusumbua, Paka anakula kilo ngapi ama ana kunywa lita ngapi hadi uone anavuruga bajeti yako,

Unaona choyo familia yako ina furaha sababu ya Paka, yaan baba zima unamuonea wivu Paka!!!!

Astaghafirullah! Wewe nyumbani kwako wageni wanakunywa hata maji kweli!!?

Ndoa hizi!!! Mola atustiri walai.
Kwetu tunapaka yaani katoroka kwao kahamia kwetu,,,,
 
Jumamosi nilitoka na jamaa flani kwenda kwa Mhindi mmiliki wa kampuni flani kubwa. Baada ya kazi yetu tunataka kuondoka wafanyakazi wakatuita tule, sasa tumekaa sebuleni na paka yuko pale pale hasogei wala hatuachii seat kama paka wa kwetu uswahilini. Yule jamaa akamfukuza ila paka hatishiki nikamkaripia yule bro nikamkumbusha yule paka yuko kwao sisi ndio walugaluga tumedowea tu msosi. Paka mwenyewe anaelewa Kihindi afu jamaa anamuita pussy, nyau wala harespond

 
Back
Top Bottom