Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Kuna paka na mbwa hapa nyumbani kwangu, Sina tatizo na gharama za mbwa kwa sababu ana msaada kiasi kwenye swala la ulinzi.

Kwa huyu paka huwa inanifikirisha sana maana hatuna tatizo la panya ila watoto wangu kwa kuwa wanapenda paka nikaamua niwarusu wamfuge.

Kimbembe kipo huku mama yao (mke wangu) amekuwa akiteketeza pesa kwenye matumizi ya huyo paka.

Bili ya maziwa imeongezeka kwa sababu paka nae anahesabiwa, anapewa maziwa asubuhi na jioni.

ananunuliwa samaki hawa wadogo wadogo kama chakula.

Matibabu nayo baada ya miezi kadhaa check up, n.k

Kuna paka waliwahi kumfuga ila alikufa, haikuchukua hata siku 2 akaletwa mwengine, Kiukeli hawa paka kazi pekee wanayojua ni kupumzika na kujizungusha chini ya miguu, Mbaya zaidi wanahisi wanakutawala ukiwaendekeza kuwapa wanachohitaji

Hii imekaaje
 
Mbwa siku zote hua ana behave Kama mtumwa lakin Paka yeye anajionaga Don.

Ndo maana wanasema hamna rafiki mzuri Kama mbwa lakin sio li Paka

Paka haridhiki na hana imani, unampa chakula na anashiba vizuri ila akikuona na wewe unaanza kula tu anaanza kukudolea mimacho siyapendi mapaka
Ila Mbwa tofauti ana shukurani na akishiba analala zake wala hakusumbui
 
Kuna paka na mbwa hapa nyumbani kwangu, Sina tatizo na gharama za mbwa kwa sababu ana msaada kiasi kwenye swala la ulinzi.

Kwa huyu paka huwa inanifikirisha sana maana hatuna tatizo la panya ila watoto wangu kwa kuwa wanapenda paka nikaamua niwarusu wamfuge.

Kimbembe kipo huku mama yao (mke wangu) amekuwa akiteketeza pesa kwenye matumizi ya huyo paka.

Bili ya maziwa imeongezeka kwa sababu paka nae anahesabiwa, anapewa maziwa asubuhi na jioni.

ananunuliwa samaki hawa wadogo wadogo kama chakula.

Matibabu nayo baada ya miezi kadhaa check up, n.k

Kuna paka waliwahi kumfuga ila alikufa, haikuchukua hata siku 2 akaletwa mwengine, Kiukeli hawa paka kazi pekee wanayojua ni kupumzika na kujizungusha chini ya miguu, Mbaya zaidi wanahisi wanakutawala ukiwaendekeza kuwapa wanachohitaji

Hii imekaaje
Kwa experience nilizokutana nazo na tabia za ajabuajabu za Wanadamu, sometimes ni bora umhudumie Paka kuliko wanadamu washenzi wasio na shukrani
 
Back
Top Bottom