Paka atolewa nduki na panya buku Mtwara vijijini

Paka atolewa nduki na panya buku Mtwara vijijini

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
kweli duniani hakuishi viroja. Kuna tukio la ajabu limetokea Mtwara Vijijini juzi mchana baada ya wanakijiji kushuhudia kwa macho yao Paka akitolewa nduki na Mapanya Buku watatu.

Tukio hili lilivuta hisia za watu wengi kwani paka alikua anakimbia akilia na mdomoni kabeba mnofu wa nyama na inaelekea aliwaibia hawa jamaa kitoweo chao na huku wale panya buku wakionekana kupania zaidi kumkamata kwa kumtangizia kwa pembeni yaani bampa tu bampa.

Salama ya paka ilikuja pale wanakijiji walipoamua kuwafukuza wale panya buku.Taarifa hii nimepewa na jamaa yangu anayeishi maeneo hayo. Jamani wataalamu wa wanyama tuelewesheni hii kitu inakuaje hapa?
 
Nimecheka sana japokuwa nina mawazo sana baada ya masaidada kunikataa live.
 
lukelo sakafu habari yako ni riwaya wanazotungaga watoto wa darasa la3!
 
Last edited by a moderator:
inawezekana kabisa maana panya buku alivokua mkubwa dah.... ila ingependeza ingekuwa na picha
 

Attachments

  • 1433494907671.jpg
    1433494907671.jpg
    9.6 KB · Views: 222
Wataalamu wa wanyama au mazingara @ kusin tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom