Kabakabana
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 5,551
- 1,160
- Thread starter
-
- #21
Lol.. Jitahidi na paja uwe unakula huko huko jikoni mwisho utazoea... Ila usianze leo manake mgeni atakosa!
Kwa ndugu zangu. . .
Sisi watoto tulikua tunakula kwanza, na minofu minofu ilikua inatuhusu.
wewe umemuelewa?nieleweshe
mlikuwa na huo utamaduni pia?
Nita ku-PM....Ni kauli tata sana
Zamani ilikuwa hivyo katika baadhi ya familia zetu ,mara ooh firigisi ni la wanaume ..
lakini sasa watoto wetu ndio tunawapa first priority ..
makubwa
Hapana,ila nimeuona kwenye familia nyingi sana....sisi kwetu vegetarians...hatuli nyama!
Mah......hutaki kujuzwa? Haya mwaya
basi wewe ni wale wa familia A.
Hahahahaha. . . Wala.
Sema tu watoto tulipewa kipaumbele, kama ambavyo inatakiwa. Sio baba zima linakunywa maziwa na mayai pembeni wakati watoto wana mwaka hawajaonja hata chai ya maziwa. Ni ubinafsi wa ajabu sana.
Mnanikumbusha mbali nyie,kulikuwa na tabia ya aliechinja kuku ni lazima ale shingo. Basi kuna siku nilichinja kuku na shingo sikupewa,niliitisha kikao cha kifamilia ili niambiwe kulikoni. Tulikuwa hatuli pilau mpaka siku ya sikukuu au siku ya sherehe.Mpaka leo nishaathirijka kisaikolojia kwani nikiona mtu anapika pilau najiuliza kama kuna sikukuu au sherehe. Vilevile sipati ladha ya pilau kwa siku za kawaida hata mpishi awe mtaalam sana. MAZOEA YANA TABU.
wewe ni rasta mamie?
Ndio mamie....tangu utoto!
kweli,utakuwa umetoka kwenye familia inayojiweza.Tatizo sio ubinafsi ni kwamba hata baba nae anakuwa hajala kuku siku nyingi.Kuhusu maziwa nimeyakuta ukubwani
Well kama kujiweza ni kuafford milo mitatu kwa siku then I guess you are right.
Tukirudi kwa baba kumiss kuku bado nasema ni ubinafsi, kwasababu hua haitokei mara moja au kwenye kuku tu. Familia ya aina hiyo inaongozwa na kauliza "ule wali wa baba uko wapi?" haisemwi chakula kiko wapi kwasababu kuna viwili, jumapili asubuhi "yale mayai/maini ya baba bado tu?". . . . Yani kila kitu baba baba. Watu wanaishia kukomba sufuria na kula ukoko wa wali.
ha haa haaa
Lizzy, ule uyoga wa baba vipi?